NGOME YA CHAUMA SEGEREA YABOMOKA WANACHAMA 200 WATIMKIA CHADEMA


WANACHAMA zaidi ya 200 wa CHAUMA  katika Jimbo la Segerea , wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, wamekihama  hicho na kurejea CHADEMA kwa madai ya kuto ridhishwa na mwenendo wa chama hicho.

Aidha, wamesema hiyo ni season ya kwanza ya  wanachama katika jimbo hilo kuhama  CHAUMA  na kujiunga na vyama vingine vya siasa bali zinakuja season  nyingi ambazo zitabeba wimbi zito la wanachama  kukihama  Chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam, leo Agosti 25,2025, kwa niaba ya wanachama hao walio hamia CHADEMA aliyekuwa Mwenyekiti wa  CHAUMA Kata ya Kinyerezi, Jimbo la Segerea,  Mndewa Mndewa ‘Dk. Timo’, ameeleza  wameamua kuhama kutokana na  mifumo mibovu.

“Tumegundua mifumo ya uongozi ndani ya CHAUMA siyo ya kikatiba ila chama kipo kwa masalahi binafsi ya baadhi ya watu,”ameeleza Dk. Timo.

Amewataka wananchi wa  Jimbo la Segerea kuto kuingia katika uchaguzi mkuu kwa mhemko  kwa kufuata wagombea wa vyama ambavyo havina mizizi hususan CHAUMA ambacho kimeanza kuonekana ndani ya miezi miwili tu.

“Huyu anayetaka kugombea  ubunge wa Segerea kwa tiketi ya CHAUMA  aliwahi kuwa mbunge  miaka mitano . Anatembea na sera ya mikopo .Miaka yote mitano iliyopita  mliwahi kumwona akija Jimbo la Segerea?”alihoji  Dk. Timo.

 Amemewataka wananchi wa Jimbo la Segerea kuwa makini na ahadi ya wagombea wa upinzania  kuwapa mikopo ya vikundi jambo ambalo haliwezekani.

“Anakuja mgombea anawakusanya wananchi na kuwaeleza waunde vikundi. Ndani ya miezi mitatu  atawapa mikopo. Miezi mitatu ni baada ya uchaguzi. Huu siyo uhuni?”alisema. 

Alionya viongozi wa CHAUMA  wa Jimbo la Segerea kuwa watulivu kwani ataanika mapungufu makubwa yakayo sambaratisha ngome nzima ya chama katika jimbo hilo.

Aliyekuwa Ofisa Habari ya wa CHAUMA  Kata ya Kinyerezi, Salumu Nasoro,   ambaye amehamia CHADEMA ameeleza   ameamua kurejea nyumbani kutokana na mfumo mbovu wa kiutendaji ndani ya chama hicho.

Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHAUMA  Kata ya Bonyokwa, Mohammed Mussa , ameeleza ameamua  kubwaga manyanga  na kurudi CHADEMA baada ya kutoridhishwa na mwenendo wa chama hicho.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.