Naibu meya John Ryoba Mrema afungua Barabara Kinyerezi .
Na Heri Shaaban( Dar es Salaam) NAIBU MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam John Ryoba Mrema afungua Barabara za mitaa ndani ya kata ya Kinyerezi Wilaya ya Ilala Naibu meya John Ryoba Mrema amefungua Barabara hizo Dar es Salaam leo katika mitaa yote ya kata ya Kinyerezi kwenye changamoto awali wananchi wake walikuwa wakipata shida katika huduma mbalimbali za usafiri . "Mimi ni Diwani wa kata ya Kinyerezi awali wakati naomba kura kuwatumikia wananchi nilieleza nitakapoingia madarakani nitatatua changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa Ilani ya chama kwa sasa nimeanza na miundombinu ya Barabara "alisema John Ryoba. Diwani Ryoba Mrema alisema kwa sasa barabara hizo za ndani zote zitaanza kupitika ukarabati umeanza sambamba na kuweka vifusi na karavati. Alisema awali Barabara hizo zilikuwa changamoto kina Mama Wajawazito kuzitumia kwa sasa mara baada kumalizika ukarabati zitatumika zote kwa huduma mbalimbali . Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa Sha...