Posts

Showing posts from February, 2026

TRC YAANZA RASMI USAFIRISHAJI WA MIZIGO KWA KUTUMIA CONTAINER CARRIERS SGR.

Image
Shirika la Reli Tanzania (TRC) limeanza rasmi usafirishaji wa makasha kwa kutumia reli ya Standard Gauge, hatua inayolenga kupanua wigo wa biashara, kupunguza msongamano wa mizigo bandarini na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda mikoa ya kati ya nchi. Akizungumza wakati wa kuanza safari ya treni ya kwanza ya makasha kutoka Pugu kuelekea Ihumwa mkoani Dodoma, Kaimu Mkurugenzi wa Usafirishaji wa TRC, Focus Makoye Sahani, amesema treni hiyo inasafiri umbali wa takribani kilometa 420 kutoka Dar es Salaam. Amesema hatua hiyo ni mwanzo wa usafirishaji wa makasha baada ya TRC kuanza kusafirisha abiria pamoja na mizigo mbalimbali ikiwemo kichele kuanzia mwezi Julai, pamoja na saruji inayopakiwa Pugu. “Leo tumeongeza wigo wa biashara kwa kupakia makasha. Kama mnavyoona, treni yetu ya kwanza ya makasha kwenda Ihumwa, Dodoma, leo imeanza safari zake na tuna ofa ya kutosha kutoka kwa mteja wetu wa kwanza,” amesema Sahani. Ameeleza kuwa treni hiyo ina mabehewa 50 yanayobeba jumla ya makasha 1...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

WAZIRI NDEJEMBI AKABIDHI MAGARI KWA MAMENEJA WA TANESCO - TABORA

Image
Waziri wa nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amekabidhi vitendea kazi vya usafiri kwa mameneja wa TANESCO wa Wilaya za Skonge, Urambo na Igunga Mkoani Tabora  ili kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi na kutatua changamoto zao kwa wakati. Akizungumza wakati akikabidhi magari hayo kwa Meneja wa TANESCO wilayani Urambo kwa niaba ya wengine, Mhe. Ndejembi amempongeza Mkurugenzi Mtendaji Bw. Lazaro Twange kwa kuchukua hatua za haraka kwa ajili ya kuhakikisha mwananchi anafikiwa bila kujali mazingira aliyopo. Amesema hatua hiyo  ya kununua vitendea kazi ni kuyaishi maono ya Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan juu ya utendaji kazi katika Mashirika ya umma ambapo TANESCO imeonesha mfano na sasa wateja takribani milioni 5.6 watapata umeme wa uhakika na kuhudumiwa kwa wakati.  ‘’Ninatamani kuona mnafanya mabadiliko makubwa katika kumfikia mteja kwa haraka, eneo la kumsikiliza na kumuhudumia mteja tunafanya vizuri sana, sasa tukaongeze nguvu ya kutatua changamoto za wateja kwa wakati k...

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 70 ZIMEKUSANYWA KUPITIA MRADI WA EACOP- MHE.SALOME

Image
Serikali imekusanya zaidi ya shilingi bilioni 70 kupitia tozo, ada na ushuru mbalimbali zitokanazo na utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), na inatarajia kukusanya zaidi ya shilingi trilioni 2.3 mradi utakapoanza kuingia katika hatua ya uendeshaji. Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema hayo tarehe 16 Februari 2026 wakati wa ziara ya Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba katika mradi wa EACOP mkoani Tanga. Mhe. Salome amesema mradi huo ambao umefikia asilimia 81  ulianza kutekelezwa mwaka 2022 na unahusisha ujenzi wa bomba lenye urefu wa kilomita 1,443 pamoja na miundombinu mingine ikiwemo matenki na gati la kupakia mafuta. Amefafanua kuwa mradi unatekelezwa kwa gharama ya dola za Marekani bilioni 5.649, huku Serikali ya Tanzania ikichangia dola milioni 374 sawa na asilimia 15 ya hisa. Katika sekta ya ajira, amesema mradi umezalisha jumla ya ajira 10,000 katika kipindi cha ujenzi, ambapo asilimia 75 sawa na ajira 7,500 zimenufaish...

RC CHALAMILA AZINDUA UTOAJI HUDUMA ZA SHERIA BURE KWA WANANCHI.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Feb 16,2026 amezindua rasmi utoaji wa huduma bure za kisheria kwa wananchi wa Mkoa huo na Mikoa jirani katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam chini ya uratibu wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali. RC Chalamila akizindua huduma hiyo amesema kuwepo kwa huduma bure ya kisheria kutasaidia kupunguza mashauri au migogoro dhidi ya Serikali, malalamiko ya kisheria kutoka kwa wananchi, vitendo vya uonevu vinavyovunja sheria na taratibu pia kwa kuwa kuna kamati za mashauri ya kisheria nazo zitatoa elimu ya sheria kwa umma katika kushughulikia changamoto mbalimbali katika maeneo yao. Aidha RC Chalamila amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassani kupitia ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuandaa klinik hiyo ambayo inatimu ya Mawakili wabobevu ambao watakuwa wanatoa huduma za kisheria bila malipo kwa wananchi wote watakaohudhuria katika viwanja hivyo kwa wananchi wote wa Mkoa wa Dar ...

TUTATENGA FEDHA ZA KUJENGA BARABARA YA KUELEKEA KAMPASI YA MZUMBE TANGA- PROF. SHEMDOE.

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amewaahidi wananchi wa Mkinga kuwa katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha  2026/27 kupitia TARURA itatengwa fedha kwa ajili ya ujenzi wa   barabara yenye urefu wa kilomita 16 kwa kiwango cha changarawe, ambazo zitaunganisha Chuo cha Mzumbe Kampasi ya Tanga na barabara kuu ya TANROADS ili kuwezesha kampasi hiyo kufikika kwa urahisi. Prof. Shemdoe ametoa ahadi hiyo leo Februari 15, 2026 baada ya Mhe. Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Mchemba, kumtaka Prof. Shemdoe kueleza mkakati wa kutatua changamoto ya ubovu wa barabara hiyo iliyowasilishwa na Mbunge wa Mkinga Mhe. Twaha Said Mwakioja na uongozi wa chuo, wakati wa hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika Chuo Kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Tanga. "Mhe Waziri Mkuu ili kufika hapa Kampasi ya Chuo Kikuu cha Mzumbe kuna umbali wa kilomita 16 zinazoangukia TARURA kutoka ilipo barabara kuu ya TANROADS, katika bajeti mwaka wa fedha 2026/27 tutatenga fedha ya kujenga barabara hii...

KIWANDA CHA NGUZO ZA ZEGE TCPM – TABORA CHA SERIKALI SIO TISHIO KWA SEKTA BINAFSI: NDEJEMBI

Image
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM Tabora kinachomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania - TANESCO kupitia kampuni tanzu ya TCPM haukusudii kuathiri wala kudhoofisha uwekezaji wa sekta binafsi bali unaongeza uzalishaji wa nguzo za zege ili kukidhi mahitaji yaliyopo ambayo bado hayajatosheleza uhitaji wa nguzo hizo nchini. Ameeleza hayo Februari 15, 2026 wakati akikagua mradi wa ujenzi wa Kiwanda cha Kutengeneza Nguzo za Zege cha TCPM Tabora, ambao umefikia asilimia 95 ya utekelezaji. Kiwanda hicho kitakuwa na uwezo wa kuzalisha wastani wa nguzo za zege 120 kwa siku. “Kiwanda hiki si tishio kwa sekta binafsi; kinakuja kuongeza nguvu katika kazi ambazo tayari zilikuwa zinafanywa na sekta binafsi ya kuzalisha nguzo za zege,” amesema Ndejembi. Ndejembi amefafanua kuwa TANESCO kwa mwaka 2025 ilikuwa na uhitaji wa nguzo za zege 80,000, lakini zilizopatikana kupitia sekta binafsi ni nguzo 40,000 jambo lililosababisha kuto...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

WAZIRI NDEJEMBI AWASILI TABORA KWA ZIARA YA KIKAZI.

Image
Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi amewasili wilayani Urambo Mkoani Tabora kwa ziara ya Kikazi na kupokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Urambo, Dkt. Khamis Mkanachi, leo tarehe 14 Februari 2026. Katika Ziara hiyo Waziri Ndejembi atatembelea na kukagua Kituo cha kupooza na Kusambaza umeme wilayani Urambo pamoja na kutembelea na kukagua kiwanda kiwada cha kuzalisha Nguzo za Zege katika Manispaa ya Tabora.

Tanroads Dodoma yapokea bilioni 15.6 Kutoka Mfuko wa Barabara.

Image
Na Mwandishi Wetu,Dodoma.  Hadi kufikia Februari,2026 Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS, Mkoa wa Dodoma umepokea jumla ya shilingi bilioni 15.6,kutoka Mfuko wa Barabara ambapo fedha hizo ni sehemu ya bajeti ya shilingi bilioni 18.6 zilizotengwa kwa ajili ya kazi za matengenezo ya barabara kwa mwaka wa fedha 2025/26. Hayo yamesemwa na Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Dodoma, Mhandisi Colman Ramadhani, wakati wa ukaguzi wa barabara ya Dodoma-Mtera yenye urefu wa Km 140.6 uliofanywa na Wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (RFB). Ukaguzi huo ni sehemu ya ufuatiliaji wa kawaida wa utekelezaji wa kazi za matengenezo ya miundombinu ya barabara na tathmini ya maendeleo ya miradi ya matengenezo ya barabara inayoendelea. Akizungumza katika ukaguzi huo, Mhandisi Ramadhani, amesema fedha zilizopokelewa zimewezesha kuendelea na utekelezaji wa kazi za matengenezo katika mtandao wa barabara unaohudumiwa na wakala huo mkoani humo.  Aidha ameeleza kuwa upokeaji wa fedha hizo umeimarisha ka...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

DKT. MWIGULU AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA KUPOOZA UMEME-MKATA.

Image
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa Mradi wa kupooza umeme uliopo Mkata mkoani Tanga ambao chenye uwezo wa 2X60MVA 132/33kV,  pamoja na ujenzi wa njia za kusambaza umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 45 kutoka kituo cha Mkata kwenda kijiji cha Kwamsisi . Mradi huo unafadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa gharama ya Shilingi Bilioni 44.14 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme na Shilingi Bilioni 5.75 kwa ajili ya ujenzi wa njia ya kusambaza umeme. Mradi huo ni miongoni mwa miradi ya uimarishaji wa Gridi ya Taifa wenye lengo la kuimarisha upatikanaji wa umeme katika Wilaya za Handeni na Kilindi pamoja na kuimairisha hali ya upatikanaji wa umeme katika Migodi ya Graphite katika Kijiji cha Kwamsisi.

WANAHABARI: SAUTI MUHIMU KWENYE SULUHISHO LA MABADILIKO YA TABIA NCHI.

Image
Na Fidea Masunga. Mabadiliko ya tabianchi yanagusa kila mtu, na vyombo vya habari vina jukumu la kipekee kuhakikisha hatua za kukabiliana na mabadiliko haya zinafanyika kwa haki, zinashirikisha wananchi, na kuwahimiza viongozi kuwajibika . Hayo yamebainishwa kwenye kongamano la kimtandao la  Cross Border Science Café , lililoandaliwa na  Media for Environment, Science, Health and Agriculture (MESHA)  kwa kushirikiana na  International Development Research Centre (IDRC) . Kongamano hilo liliwakutanisha wanahabari na wadau kutoka nchi sita za Afrika kujadili mabadiliko ya tabianchi, jinsia, afya, na habari zenye matokeo chanya kwa jamii. Teresa Anderson, Kiongozi wa Kimataifa wa Haki ya Tabianchi wa  ActionAid International , alisema nishati safi ni suluhisho la kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi, lakini inahitaji mshikamano wa wadau wote, wakiwemo wanahabari, wakati wa utekelezaji wa sera za tabianchi. “Sera za tabianchi lazima ziwe sawa, zikihakikisha chakul...

RAIS WA CAF AWASILI TANZANIA.

Image
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Dkt. Patrice Motsepe, amewasili rasmi nchini Tanzania asubuhi ya leo kwa ajili ya kuhudhuria Mkutano wa Kamati Tendaji ya Shirikisho hilo. Mutsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, Terminal 1, jijini Dar es Salaam. Dkt. Motsepe ataongoza mkutano huo unaotarajiwa kufanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro. Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu. Kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni ishara ya nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.

NISHATI YA UMEME INACHOCHEA KASI YA MAENDELEO MKOANI SINGIDA - MEYA SINGIDA.

Image
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Singida, Mhe. Geofrey Mdama, amesema nishati ya umeme imekuwa na mchango mkubwa katika kusukuma maendeleo na kuongeza kasi ya ukuaji wa mkoa wa Singida, kutokana na umuhimu wake katika kuimarisha fursa za kiuchumi, sekta ya viwanda, na uwekezaji. Mstahiki Meya ameyasema hayo kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Singida, Februari 12, 2026, wakati akifungua kikao kazi kati ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na wenyeviti wa Serikali za Mitaa, watendaji wa kata pamoja na madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Singida.  Ameipongeza TANESCO kwa kutambua mchango wa viongozi hao, ambao ni ngazi muhimu katika kuwaelimisha wananchi kuhusu kazi zinazofanywa na Shirika hilo na umuhimu wa nishati ya umeme katika nyanja mbalimbali za kijamii na kiuchumi. “Naipongeza sana TANESCO kwa kutambua umuhimu na mchango wa viongozi hawa, kwa kuwa wanaishi karibu na wananchi. Kupitia wao, ni rahisi zaidi kuifikia jamii. Vilevile, tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Sulu...

RC CHALAMILA AENDELEA KUCHANJA MBUGA WILAYA YA KINONDONI.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameendelea na ziara yake katika wilaya ya Kinondoni leo februari 12, 2026 ambapo amekagua kazi nzuri inayofanywa na sekta binafsi katika utoaji wa huduma ya afya hususani Hospital ya Shifaa iliyoko Hananasifu Kinondoni, ameridhishwa na uwekezaji uliofanyika katika hospitali hiyo na kumuagiza Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kutenga maeneo yauwekezaji na kuwakaribisha watu binafsi kuwekeza kwa masilahi mapana ya Wilaya, Mkoa na Taifa kwa ujumla. Aidha RC Chalamila amekagua mradi wa elimu shule ya ghorofa ya Sekondari Tarimba Abbas yenye vyumba vya madarsa 21, Maktaba 1, vumba 3 vya maabara, Jengo la utawala, computer lab, na matundu 44 ya vyoo ambapo ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo, huku akisisitiza maendeleo hayana chama hivyo amemshukuru Mhe Rais Dkt.Samia Suluhu Hassani kwa uwekezaji mkubwa katika sekta mbalimbali hapa nchini hususani sekta ya elimu. Ifahamike kuwa Mhe Mkuu wa Mkoa yuko katika ziara ya kukagua miradi ya m...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

KAMISHNA LUOGA ASISITIZA MAADILI NA UWAJIBIKAJI SEKTA YA NISHATI.

Image
Na Mwandishi Wetu Mwenyekiti wa Kamati za Maadili za Wizara ya Nishati na taasisi zake, ambaye pia ni Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga, amewataka wajumbe wa kamati hizo kuzingatia uwajibikaji, maadili, uwazi na ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao ili kuongeza ufanisi mahali pa kazi. Mhandisi Luoga ameyasema hayo Februari 3, 2026 mkoani Morogoro  akifungua kikao kazi cha wajumbe wa Kamati za Uadilifu kutoka Wizara ya Nishati, taasisi zilizo chini ya wizara hiyo pamoja na kampuni zake tanzu. Amesema kikao hicho kinalenga kuimarisha uwajibikaji na maadili kazini, kuongeza uelewa wa masuala ya kiutumishi pamoja na kutoa fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwa wajumbe. Kwa mujibu wa Kamishna Luoga, mafanikio ya sekta ya nishati yanategemea kwa kiasi kikubwa nidhamu kazini, matumizi sahihi ya rasilimali na uwajibikaji wa kila mtumishi wa umma, hivyo kamati za uadilifu zina wajibu mkubwa wa kusimamia misingi hiyo muhimu. Ameongeza kuwa kuimarish...

WADAU SEKTA YA HALI YA HEWA WAJADILI UTABIRI WA MASIKA 2026 .

Image
Wadau kutoka sekta mbalimbali nchini wamekutana kujadili utabiri wa msimu wa Masika 2026 na kutoa ushauri wa kisekta katika Mkutano wa 25   wa Wadau wa Sekta ya Hali ya Hewa katika msimu wa Masika uliofanyika tarehe 2/2/2026, Jijini Dodoma. Mkutano huo ni mwendelezo wa ushirikishwaji wa wadau katika utoaji wa taarifa za hali ya hewa kwa ajili ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini.  Mgeni Rasmi kwenye mkutano huo, Mh. Jaji  Mshibe Ali Bakari ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya TMA  alisema “msimu wa Vuli mwaka 2025 ulitawaliwa  na vipindi virefu vya ukavu katika maeneo mengi ya nchi, usahihi wa utabiri ulikuwa kwa asilimia 94.1, ikiwa ni kiwango kikubwa sana, natoa wito kwa wananchi waendelee kuiamini TMA, wazingatie taarifa zinazotolewa na kuzitumia katika shughuli zao za kila siku".   Aidha, alisisitiza kuwa majadiliano ya mvua za Masika kwa mwaka 2026, yazingatie kwa kina athari zinazoweza kujitokeza pamoja na kutoa ushauri wa hatua stahiki za kuchukua k...