RAIS WA CAF AWASILI TANZANIA.
Mutsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Airport, Terminal 1, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Motsepe ataongoza mkutano huo unaotarajiwa kufanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam, The Kilimanjaro.
Mkutano huo unatarajiwa kukutanisha viongozi mbalimbali wa soka barani Afrika kwa ajili ya kujadili masuala muhimu yanayohusu maendeleo ya mpira wa miguu.
Kuwa mwenyeji wa mkutano huo ni ishara ya nafasi ya Tanzania katika ramani ya soka barani Afrika, hususan katika kipindi hiki cha maandalizi ya mashindano ya AFCON 2027.




Comments
Post a Comment