TANZANIA YAPOKEA UJUMBE WAFANYABIASHARA KUTOKA FALME YA SAUDI ARABIA Serikali ya Tanzania, ikiongozwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, pamoja na viongozi wengine wa serikali, imefanya kikao muhimu na ujumbe kutoka Falme za Saudi Arabia, Lengo likiwa ni kujadili fursa za uwekezaji na kukuza ushirikiano kati ya nchi hizi mbili. Ujumbe huu wa wafanyabiashara toka chemba ya uwekezaji kutoka nchini Saudi Arabia unaongozwa na Naibu Waziri wa Uchumi na Mipango wa Falme za Saudi Arabia, Mhe. Albara Alaskandarani, na Ujumbe huu umejumuisha wafanyabiashara 30 kutoka sekta mbalimbali, ikiwemo Nishati, Kilimo, Mifugo, Uvuvi, Viwanda, Biashara na Uchukuzi. Katika kikao hicho, Mhe. Albara Alaskandarani alitoa pongezi kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa juhudi za kukuza uchumi, na kuongeza kuwa hatua hii inatarajiwa kutoa suluhisho la kudumu kwa changamoto mbalimbali za kimaendeleo. Kwa upande wa Sekta ya Nishati uliwakilishwa na N...