MAMBO MUHIMU KUHUSU USALAMA BARABARANI.

 *MAMBO MUHIMU KUHUSU USALAMA BARABARANI*


1. *CHUKUA TAHADHARI DHIDI YA AJALI ZA BARABARANI* kwani:

(a)Duniani kote ajali za barabarani zinaua watu 1,190,000 kila mwaka, na zinaacha wengine zaidi ya milioni 50 wakiwa majeruhi;

(b)Ajali za barabarani ni chanzo nambari 12 cha vifo vyote ulimwenguni

(c)Ajali za barabarani zinachangia 24.4 ya vifo vyote ulimwenguni.

(d)Ajali za barabarani ni chanzo Na.1 cha vifo kwa watoto na vijana kati ya umri wa miaka 5-29.

(e)Ajali za barabarani zinaacha yatima, wajane, wagane, na kuleta simanzi kubwa katika familia

(f)Ajali za barabarani zinavunja ndoa, zinatenganisha familia.

(g)Ajali za barabarani zinaleta au kuongeza  umasikini katika familia

(h)Ajali za barabarani zinafifisha ndoto za watoto na vijana.

(i)Ajali za barabarani ni chanzo cha ulemavu mwingi wa ukubwani duniani.

(j)Maisha yako, viungo vyako havina spea; ukishakufa umekufa, ukishapoteza mguu, huwezi pata mguu mwingine kama uliokuwa nao awali. 


2. *FUNGA MKANDA*

Kufunga mkanda kuna faida zifuatazo:

(a)Kukufanya ubaki ndani ya gari ikitokea ajali, kwani 80% ya watu waliorushwa nje ya gari walikufa. Waliopona baadhi walipatwa na ulemavu wa kudumu.

(b)Kukuzuia usijigonge  na mwenzako au na kitu kingine ndani ya gari.

Mchubuko unaosababishwa na kubanwa na mkanda una afadhali kuliko jeraha jingine.

(c)Mkanda unazuia hatari ya kifo kwa 45-50% kwa abiria wa mbele na 25% kwa abiria wa siti za nyuma.

(d)Abiria wa nyuma wasipofunga mkanda wanahatarisha usalama wa abiria wa mbele. Kwani ikitokezea ajali, abiria wa nyuma wanaweza kurushwa kwenda kuwagonga vichwani wale wa mbele. Wanapokuwa kama mawe yanayoporomoka.

(e)Zipo shuhuda nyingi za watu waliopona kwenye ajali kutokana na kufunga mkanda, lakini pia waliokufa kutokana na kutofunga mkanda. 


3. *USINYWE POMBE NA KUENDESHA GARI (ULEVI)*

(a)Usiendeshe gari ukiwa umelewa

(b)5-35% ya vifo vyote barabarani husababishwa na pombe

(c)Ni kosa kuendesha gari la abiria au mizigo ukiwa na kilevi

(d)Ni kosa kuendesha gari lolote ukiwa na kilevi cha zaidi ya 0.08g/dl au 0.80gm/100mls za damu.

(e)Pombe inakupa ujasiri wa uongo barabarani na hivyo kupelekea kupata ajali. 


4. *VAA HELMETI*

(a)Vaa helmeti wakati wote ukiwa umepanda pikipiki

(b)Matumizi sahihi ya helmeti yanapunguza madhara kwa kuumia kichwa kwa 69% na vifo kwa 42%

(c)Usiegeshe helmeti kichwani 


5. *DHIBITI MWENDOKASI WAKO*

(a)Mwendokasi ni hatari, mwendo kasi unaua.

(b)Kila 1% ya ongezeko la spidi, linazalisha 4% ya ongezeko la hatari ya kifo kutokana na ajali na 3% ya kutokea kwa ajali.

(c)Kwa mwenda kwa miguu anayegongwa na gari kwa mbele (car front), hatari ya kifo inaongezeka mara 4.5 kutoka spidi ya 50kph hadi 65kph.

(d)Kwa magari yanayogongana upande na upande (car to car side impact),hatari ya kutokea kifo kwa waliomo ndani ya gari ni 85% kwa gari lililo katika spidi ya 65kph.

(e)Endesha kwa mwendo wa tahadhari na kwa kiasi cha 50kph katika maeneo yote ya makazi

(f)Walinde watoto wako dhidi ya magari yaliyoko katika mwendo

(g)Wanaokusifia kuendesha gari kwa kasi ya juu, hawatakuwa na wewe hospitali wala ukifa hawatalisha familia yako.

(h)Kila unapopunguza spidi kwa wastani wa 5% ya spidi uliyokuwa nayo unapunguza uwezekano wa kutokea vifo kwa 30%.

6. *TIKETI*

(a)Abiria kata tiketi yako mapema kabla ya safari

(b)Abiria tunza tiketi yako hadi mwisho wa safari

(c)Tiketi ni kielelezo muhimu kwenye madai ya bima iwapo utapata ajali. Tunakushauri upige picha tiketi yako na kuihifadhi kwenye e-mail au kurusha kwa mwenzio unaposafiri. Ili ukiipoteza uwe na nakala.

(d)Hakikisha una tiketi mtandao (e ticket)

(e)Fahamu namba za gari unalosafiria. 


7. *MLINDE MWANAO AKIWA NDANI YA GARI*

1.Usimweke mtoto wako katika siti ya mbele ya gari lako kwani akiwa mbele hana kitu kinachomzuia kurushwa nje

2.Mwekee mwanao kiti cha watoto (child restraint) kwenye siti ya nyuma ya gari lako. Na ikiwa huna kiti hicho ni vema ukamweka mwanao kwenye siti ya nyuma.

3.Kizuizi cha watoto kimethibitishwa kuzuia vifo kwa 45-59% kwa watoto.


Usalama Barabarani ni Jukumu Letu Sote.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.