Posts

Showing posts from June, 2026

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

BARAZA JIPYA LA NIT LATAKIWA KUIMARISHA TAFITI NA MAFUNZO YA UCHUKUZI

Image
Waziri wa Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, ameliagiza Baraza la 13 la Uongozi la National Institute of Transport kuhakikisha linasimamia kwa ufanisi mafunzo na tafiti zinazolenga kutatua changamoto za sekta ya usafirishaji na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizindua baraza hilo mkoani Morogoro, Prof. Mbarawa amesema chuo kina wajibu mkubwa wa kuisaidia Serikali katika kuandaa sera na mikakati madhubuti ya maendeleo ya sekta ya uchukuzi nchini. Amesema utekelezaji wa jukumu hilo utawezesha chuo kufikia malengo ya mpango wake wa miaka mitano unaolenga kuboresha ubora wa elimu na mafunzo, kukidhi mahitaji ya soko la ajira la kisasa pamoja na kuimarisha miundombinu ya kujifunzia ikiwemo maabara, maktaba na matumizi ya teknolojia za kisasa. Prof. Mbarawa ameongeza kuwa maandalizi ya awali ya Sera Mpya ya Taifa ya Uchukuzi yameanza kuzingatia mifumo mipya ya usafiri kama Cable Transport na Space Transport, hivyo akalitaka baraza hilo kuandaa wataalamu watakaoweza kuhudumia maeneo ...

MAMIA YA WATANZANIA TABORA KUNUFAIKA NA UPASUAJI WA MTOTO WA JICHO BILA MALIPO

Image
Serikali kupitia Wizara ya Afya kwa kushirikiana na wadau wa sekta ya afya, ikiwemo Helen Keller International, imeanzisha kambi maalum ya uchunguzi na upasuaji wa mtoto wa jicho katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora, ambapo takribani wananchi 700 wanatarajiwa kunufaika na huduma hizo bila malipo. Miongoni mwa wanufaika ni Henry Machibya (62), mkazi wa Simbo wilayani Igunga, ambaye amesema tatizo la macho lilianza mwaka 2023 na kuendelea kuathiri uwezo wake wa kuona hadi kupoteza kabisa uwezo wa kuona kwa macho yote mawili katika miezi ya hivi karibuni. Machibya amesema hali hiyo ilimlazimu kuacha shughuli zake za kilimo ambazo zilikuwa chanzo chake kikuu cha mapato na kujikuta akitegemea msaada wa watu wa karibu katika kutekeleza mahitaji ya msingi ya kila siku. “Nilikuwa nikitegemea kilimo kwa ajili ya kujikimu na kuhudumia familia yangu, lakini hali ya macho yangu ilibadilisha maisha yangu kabisa,” amesema. Aidha, amesema changamoto nyingine alizokumbana nazo n...

KILLOLO DC YAVUTIA UTALII IKOLIJIA KILOMBERO, DAS BI. NYAKAJI AONGOZA KAMBI CHUI CAMPSITE.

Image
Kilombero Nature Reserve, Iringa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kilolo, ikiongozwa na Katibu Tawala wa Wilaya hiyo, Bi. Nyakaji Etanga, imehimiza wananchi na watumishi wa umma kutumia fursa za utalii ikolojia zilizopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Kilombero (Kilombero Nature Forest Reserve), baada ya kufanya ziara na kupiga kambi katika kituo cha utalii cha Chui Campsite kilichopo Udekwa. Ziara hiyo iliyofanyika kuanzia Juni 3 hadi Juni 4, 2026 ilihusisha viongozi wa kamati hiyo waliopata fursa ya kufanya kambi ndani ya hifadhi, hatua iliyolenga kuhamasisha utalii wa ndani na kuongeza uelewa wa uhifadhi wa mazingira kupitia uzoefu wa moja kwa moja wa vivutio vilivyopo. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Nyakaji Etanga alisema ameridhishwa na mandhari ya kipekee ya Chui Campsite pamoja na fursa mbalimbali za kiutalii zilizopo ndani ya hifadhi hiyo, akisisitiza umuhimu wa wananchi kushiriki kikamilifu katika utalii ikolojia kama njia ya kuchochea maendeleo ya kiuch...

Serikali Kupeleka Umeme Katika Mitaa 14 Iliyosalia Tarime Mjini

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema Serikali kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) imepanga kupeleka umeme katika mitaa 14 iliyosalia bila huduma hiyo katika Mji wa Tarime, kwa kuhakikisha mitaa yote inafikiwa na umeme. Mhe. Salome amesema hayo leo, Juni 8, 2026, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mhe. Ester Matiko, Mbunge wa Tarime Mjini, aliyetaka kujua ni lini umeme utafika katika mitaa yote isiyo na umeme katika Mji wa Tarime. Amesema Mji wa Tarime una jumla ya mitaa 81, ambapo mitaa 54 ina umeme na mitaa 27 haina umeme. Amefafanua kuwa kati ya mitaa 27 isiyo na umeme, mkandarasi anaendelea na kazi katika mitaa 13 na hadi sasa ameshasimamisha nguzo huku akijiandaa kuanza kufunga nyaya. Aidha, Mhe. Salome amesema Serikali kupitia TANESCO imepanga kupeleka umeme katika mitaa iliyosalia kulingana na upatikanaji wa fedha, kwa lengo la kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kila mtaa nchini umefikiwa na huduma ya umeme. Kadhalika, Mhe. Salome ametumia nafasi...

TANZANIA YASHIRIKI JUKWAA LA UTALII, BIASHARA NA UWEKEZAJI KATI YA TANZANIA NA MISRI

Image
Cairo, Misri, Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Hassan Abbasi leo Juni 8, 2026 ameshiriki Ufunguzi wa Jukwaa la Utalii, Biashara na Uwekezaji kati ya Tanzania na Misri linalofanyika jijini Cairo, likiwakutanisha viongozi wa Serikali, taasisi za utalii, wafanyabiashara, wawekezaji na wadau mbalimbali kutoka nchi hizo mbili kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na kukuza fursa za biashara, uwekezaji na utalii. Jukwaa hilo limeandaliwa chini ya kaulimbiu inayohamasisha uhusiano kati ya Bahari ya Mediterania na Bahari ya Hindi kupitia masoko, utalii, biashara na uwekezaji, likitoa fursa kwa wadau kujadili maeneo mbalimbali ya ushirikiano yenye manufaa kwa pande zote mbili. Katika jukwaa hilo, Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki mjadala ambapo washiriki walijadili fursa za ushirikiano katika sekta za utalii, biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Misri.  Aidha, washiriki walipata fursa ya kushuhudia video mbalimbali za kutangaza...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

TPDC YAKABIDHI KARAKANA YA KISASA YA CNG KWA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM.

Image
Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limekabidhi rasmi Karakana ya kuongeza mfumo wa matumizi ya gesi asilia Iliyoshindiliwa kwenye vyombo vya usafiri (CNG Conversion Workshop) kwa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), hatua inayotarajiwa kuimarisha matumizi ya nishati safi nchini pamoja na kukuza ujuzi wa kitaalamu katika teknolojia ya gesi asilia. Makabidhiano hayo yamefanyika jijini Dar es Salaam, ambapo TPDC iliwakilishwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mipango na Uwekezaji, Bw.Derick Moshi, kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC. Kwa upande wa UDSM, karakana hiyo ilipokelewa na Naibu Mkuu wa Chuo Prof. Bernadeta Kilian.  Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Bw. Derick Moshi alisema kuwa ujenzi wa karakana hiyo ni sehemu ya jitihada za TPDC katika kuunga mkono mkakati wa Serikali wa kuhamasisha matumizi ya nishati safi na nafuu kwa wananchi. “Kukamilika na kukabidhiwa kwa karakana hii ni hatua muhimu katika kukuza matumizi ya gesi asilia Iliyoshindiliwa (CNG) nchini. Mbali n...

DKT. NCHIMBI ATEMBELEA BANDA LA REA

Image
    Dodoma Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi ametembelea banda la Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kilele cha Maonesho ya Siku ya Mazingira Duniani 2026 yanayofanyika jijini Dodoma.  Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi ametembelea banda la REA leo Juni 5, 2026 ambapo ameelezwa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Wakala maeneo ya Vijijini na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala Mha. Advera Mwijage. Halikadhalika, Mha. Mwijage amemueleza Mhe. Balozi Dkt. Nchimbi kuwa, kupitia miradi inayotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imesaidia kupunguza athari za uharibifu na uchafuzi wa mazingira. Maonesho ya mwaka huu yamepambwa na kauli mbiu isemayo: *Dira 2050: Tuwajibike Kukijanisha Tanzania*

NAIBU WAZIRI WA MAJI APONGEZA JUHUDI ZA TFS KULINDA VYANZO VYA MAJI

Image
Na Mwandishi Wetu, Dodoma Naibu Waziri wa Maji, Eng. Kundo Mathew, amepongeza juhudi zinazofanywa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kuhifadhi misitu na kulinda vyanzo vya maji nchini, akieleza kuwa uhifadhi wa misitu ni msingi muhimu wa upatikanaji endelevu wa maji kwa wananchi na shughuli za maendeleo. Eng. Kundo alitoa pongezi hizo Juni 4, 2026, alipotembelea banda la TFS na Idara ya Misitu na Nyuki katika Maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yanayoendelea jijini Dodoma. Akipokea maelezo kutoka kwa Afisa Uhifadhi Mwandamizi wa TFS, Filipo Mwampamba, Naibu Waziri huyo alitaka kufahamu kwa kina namna TFS inavyoshirikiana na Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zinazohusika na usimamizi wa mabonde ya maji katika kuhifadhi vyanzo vya maji vinavyotegemewa kwa matumizi ya nyumbani, kilimo, uzalishaji wa umeme na shughuli nyingine za kiuchumi. Akijibu, Mwampamba alisema TFS imekuwa ikitekeleza programu mbalimbali za kuhifadhi misitu ya vyanzo vya maji kwa kushirikiana n...

SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA MIUNDOMBINU YA BARABARA ZA WILAYA KUIMARISHA UCHUMI: MSIGWA

Image
Mwanza Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini kwa kupunguza barabara za changarawe na kujenga barabara za lami katika wilaya mbalimbali, hatua inayolenga kuwawezesha wananchi kuinuka kiuchumi kupitia shughuli za usafirishaji. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alipokuwa akizungumza na Maofisa Uhusiano na Mawasiliano Serikalini wakati wa Mkutano wa Mwaka wa Chama cha Maofisa Mawasiliano Serikalini (TAGCO) unaoendelea jijini Mwanza. Msigwa amesema maofisa Mawasiliano wanapaswa kuhakikisha wananchi wanapata taarifa sahihi kuhusu miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali kwa kuwa miradi hiyo ni ya manufaa kwa wananchi wenyewe. “Sisi ndiyo tunaobeba taswira ya Serikali. Tunapaswa kuwaonesha wananchi fursa zilizopo kutokana na uwekezaji mkubwa wa miundombinu unaofanywa na Serikali,” amesema. Ameongeza kuwa Serikali imejenga barabara za mzunguko zenye urefu wa kilomita 56 katika ...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

Dkt. Seif: Mazao ya Nyuki Ni Hazina ya Afya, Uchumi na Uhifadhi wa Mazingira.

Image
Na Mwandishi Wetu, Dodoma NAIBU Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI anayeshughulikia masuala ya Afya, Dkt. Jafari Rajabu Seif, amepongeza juhudi za Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kuendeleza sekta ya ufugaji nyuki na uzalishaji wa mazao yake, akisema sekta hiyo ina mchango mkubwa katika kuboresha afya za wananchi, kukuza uchumi na kuhifadhi mazingira. Dkt. Seif alitoa pongezi hizo leo June 03,2026 baada ya kutembelea banda la TFS katika Maonesho ya Wiki ya Mazingira yanayoendelea katika Viwanja vya Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma, ambako alipata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali zinazotekelezwa na wakala huo, hususan katika ufugaji nyuki na uchakataji wa mazao yatokanayo na nyuki. Akiwa katika banda hilo, Naibu Waziri huyo alivutiwa na bidhaa mbalimbali zilizokuwa zikionyeshwa, zikiwemo asali, nta na bidhaa nyingine za nyuki ambazo zimeendelea kupata soko kutokana na ubora wake pamoja na manufaa yake katika afya, lishe na uchumi wa wananchi. “Nimevutiwa sana ...

MHA. MRAMBA NA BENKI YA DUNIA WAJADILI UIMARISHAJI WA GRIDI YA TAIFA

Image
Dar es Salaam,  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati anayeshughulikia Umeme na Nishati Jadidifu, Mha. Felchesmi Mramba,  amekutana na wawakilishi wa Benki ya Dunia (WB) kujadili matokeo ya utafiti uliofanyika chini ya ufadhili wa benki hiyo ukilenga kuimarisha mfumo wa Gridi ya Taifa nchini. Utafiti huo umebainisha maeneo muhimu ya utekelezaji yatakayosaidia kuimarisha Gridi ya Taifa ili kuhakikisha mfumo wa umeme nchini unakidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye. Akizungumza katika kikao hicho, Mha. Mramba ameishukuru Benki ya Dunia kwa kuendelea kuunga mkono maendeleo ya sekta ya nishati nchini kupitia ufadhili na usimamizi wa tafiti mbalimbali zenye lengo la kuboresha miundombinu ya umeme na kuongeza ufanisi wa huduma kwa wananchi. Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kuweka mkazo katika utekelezaji wa mapendekezo yaliyotolewa kwenye ripoti hiyo ili kusaidia mipango ya uwekezaji, kuboresha uendeshaji wa mfumo wa umeme, kuendeleza usasa wa Gridi ya Taifa na kuongeza uimara wa hudum...

BEI YA PETROLI YASHUKA, SERIKALI YAWEKA RUZUKU KWENYE DIZELI

Image
Watumiaji wa petroli wamepata afueni mwezi Juni 2026 baada ya bei ya mafuta hayo kushuka ikilinganishwa na mwezi uliopita. Kwa Dar es Salaam, petroli sasa itauzwa kwa bei kikomo ya shilingi 4,086 kwa lita, hatua inayotarajiwa kupunguza gharama kwa watumiaji wa kawaida na baadhi ya shughuli za usafiri. Kwa upande wa dizeli, watumiaji wanakabiliwa na ongezeko dogo la bei, ambapo kwa Dar es Salaam bei kikomo imefikia Shilingi 4,333 kwa lita. Ongezeko hilo limechangiwa na kupanda kwa gharama za mafuta katika soko la dunia pamoja na kuongezeka kwa gharama za uagizaji wa bidhaa hiyo. Licha ya changamoto hizo za kimataifa, Serikali imeendelea kuchukua hatua za kulinda uchumi na wananchi kwa kuweka ruzuku ya Shilingi 534.91 kwa kila lita ya dizeli. Hatua hiyo imelenga kupunguza athari za ongezeko la bei kwa sekta muhimu kama usafirishaji, viwanda na huduma za kijamii. Mabadiliko haya yameathiriwa kwa kiasi kikubwa na vita vinavyoendelea Mashariki ya Kati, vinavyohusisha Marekani, Israeli na Ir...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

GOLDEN VALUE WAPATIWA ELIMU YA NISHATI KATIKA MAONESHO YA WIKI YA MAZINGIRA DUNIANI 2026

Image
Na Mwandishi Wetu, Meneja wa Shule ya Golden Value Bi. Nuru Nyundo, ameongoza wanafunzi wa darasa la nne na la sita kutembelea banda la Wizara ya Nishati pamoja na taasisi zake katika Maonesho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026 yanayoendelea katika katika Viwanja vya Jakaya Kikwete Convention Centre jijini Dodoma Ziara hiyo imelenga kuwapatia wanafunzi elimu kuhusu sekta ya nishati na mchango wake katika uhifadhi wa mazingira.  Wakiwa katika banda hilo, wanafunzi walipata fursa ya kujifunza kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia, nishati jadidifu na teknolojia mbalimbali zinazosaidia kupunguza uharibifu wa mazingira. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Bi. Nyundo amesema  kuwa kuwashirikisha wanafunzi katika maonesho hayo ni njia muhimu ya kuwajengea uelewa wa mapema kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kutumia nishati kwa njia endelevu ili kulinda afya na mazingira kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kwa upande wake, mwanafunzi Maria Yusuph wa darasa la sita amepong...

Mhe. Salome awahimiza Wanawake kuchangamkia fursa za Nishati Safi ya Kupikia.

Image
Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, amewahimiza wanawake na vijana nchini  kutumia fursa zilizopo katika sekta ya nishati safi ya kupikia ili kujiimarisha kiuchumi na kuchangia maendeleo ya taifa. Mhe. Salome amesema hayo wakati akishiriki harambee ya kutunisha mfuko wa Kikundi cha Wanawake na Mwalimu Nyerere  jijini Dodoma. Ameeleza kuwa katika maeneo mengi ya vijijini matumizi ya nishati safi ya kupikia  bado ni madogo, jambo linalotoa nafasi kwa wananchi kushiriki katika utoaji wa elimu, ubunifu wa teknolojia na uzalishaji wa bidhaa za nishati safi ikiwemo mkaa mbadala. “Nitoe wito kwa kikundi chenu kuangalia kwa makini eneo hili na kutumia fursa zilizopo ili kuinua uchumi wa wanachama  pamoja na kuchangia jitihada za Serikali za kulinda mazingira,” amesema.Mhe. Salome Katika kuendeleza juhudi za kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia, Mhe. Salome  amesema Serikali kupitia Wizara ya Nishati imetenga Shilingi bilioni 10 katika mwaka wa fedha...

KUHIFADHI MAZINGIRA NI WAJIBU WA KILA MTANZANIA” – MHE. KWAGILWA

Image
Na Mwandishi Wetu Naibu Waziri wa Mazingira, Mhe. Reuben Kwagilwa, ametembelea mabanda mbalimbali ya taasisi na wadau wanaoshiriki Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira Duniani 2026 yanayofanyika katika Ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Centre (JKCC), jijini Dodoma. Katika ziara hiyo, Mhe. Kwagilwa amepata fursa ya kujionea shughuli, huduma na teknolojia mbalimbali zinazochangia uhifadhi wa mazingira, matumizi endelevu ya rasilimali za asili pamoja na juhudi za kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi. Ametoa pongezi kwa taasisi na wadau wanaoshiriki maonesho hayo kwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kutunza mazingira na kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira katika shughuli za kila siku. Aidha, amesisitiza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi na wananchi ni muhimu katika kufanikisha juhudi za uhifadhi wa mazingira na kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya Taifa. Akiwa katika banda la Wizara ya Nishati na taasisi zake za TANESCO, REA na TPDC, Mhe...

WANAFUNZI 246,197 WALIOPANGIWA KUJIUNGA KIDATO CHA TANO WANAPASWA KURIPOTI SHULENI JULAI 04, 2026 - PROF. SHEMDOE

Image
Na OWM - TAMISEMI, Dar es Salaam Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM-TAMISEMI) Mhe. Prof. Riziki Shemdoe amesema jumla ya wanafunzi 246,197 wakiwemo wasichana 114,102 na wavulana 132,095 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano mwaka 2026 wanatakiwa kuripoti shuleni kuanzia Julai 04, 2026 hadi Julai 31, 2026 kwakuwa muhula wa kwanza wa masomo utaanza Julai 06, 2026.  Prof. Shemdoe amesema hayo leo Juni 01, 2026 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi Ndogo ya Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Magogoni Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa taarifa kwa umma kuhusu wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano na vyuo vya elimu ya ufundi kwa mwaka 2026. “Wanafunzi 172,114 sawa na asilimia 69.9 wakiwemo wasichana 85,987 na wavulana 86,127 wenye sifa wamechaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika shule  za sekondari za Serikali 856 zikiwemo shule za bweni 825, kutwa 25 na kutwa na bweni sita (06),” amefafanua Prof. Shemdoe. Aidha, Prof. S...