Posts

Showing posts from August, 2025

Mpina, Mluumbe waenguliwa kwenye kinyang’anyiro cha urais

Image
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetengua uteuzi wa wagombea wa nafasi ya urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waliokuwa wamepitishwa na vyama vyao. Wagombea waliotenguliwa ni  Bw. Wilson Elias Mluumbe  wa Chama cha  Alliance for Democratic Change (ADC)  na  Bw. Luhaga Joelson Mpina  wa  ACT–Wazalendo . Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa    na Msajili, imesema hatua hiyo imechukuliwa baada ya kupitia vielelezo na ushahidi uliowasilishwa na pande husika, na kubaini kuwa mchakato wa uteuzi ndani ya vyama hivyo ulikiuka  Sheria ya Vyama vya Siasa (Sura 258) , pamoja na Katiba na Kanuni za vyama husika. Msajili amesisitiza kuwa, kwa mujibu wa kifungu cha 6A(2) cha Sheria ya Vyama vya Siasa, vyama vinapaswa kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia Katiba ya Nchi, Sheria, pamoja na Katiba na Kanuni zao. Aidha, alionya kuwa wagombea wa nafasi mbalimbali lazima wapitishwe kwa njia halali na ya kidemokrasia ili kulinda  utawala wa sheri...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 zijazo.

Image
 

WAZIRI MKUU ALIPONGEZA JESHI LA MAGEREZA URASIMISHAJI UJUZI KWA WAFUNGWA.

Image
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amelipongeza Jeshi la Magereza Tanzania kwa kufanya urasimishaji wa ujuzi wanaoupata wafungwa kupitia VETA na kuwawezesha kupata ajira au kuanzisha biashara zao baada ya kumaliza kifungo.   Ameongeza kuwa kupitia mitaala mipya ya mafunzo ya amali na stadi za kazi, jeshi hilo limefanikiwa kuwanufaisha zaidi ya wafungwa 5,000 ambapo baadhi yao wameweza kujiajiri au kuajiriwa baada ya kumaliza vifungo vyao.   Ametoa pongezi hizo leo Jumanne (Agosti 26, 2025) wakati aliposhiriki katika maadhimisho ya kilele cha miaka 64 ya Jeshi la Magereza Tanzania yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania, Ukonga jijini Dar es Salaam.   “Ninatoa pongezi za dhati kwa jeshi la magereza kwa mafanikio haya, huu ni mpango kazi wenu, na tumeona faida na vijana hawa waliokuja hapa wameeleza namna ambavyo wamenufaika na kazi hizi”   Kwa Upande wake, Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Jumanne Sagini amelipongeza Jeshi la Magereza kwa ...

AHUKUMIWA MIAKA SABA JELA KWA KOSA LA KUUA BILA KUKUSUDIA.

Image
Mahakama Kuu Kanda ya Morogoro imewahukumu kifungo cha miaka saba jela Shigela Washa Buhimila (32), mkazi wa Tuliza Moyo, Wilaya ya Ulanga, baada ya kukiri kosa la kuua bila kukusudia wakati wa tukio la wizi wa mifugo. Hukumu hiyo imesomwa na Mheshimiwa Jaji Stephen Magoiga, Agosti 25, 2025, katika Mahakama Kuu iliyoketi Wilayani Kilombero. Tukio hilo lilitokea usiku wa Desemba 23, 2024, katika eneo la Makingi, Kitongoji cha Popoto, Kijiji cha Mavimba, Kata ya Milola, Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga. Shigela na mwenzake aliyefahamika kwa jina la Malege (ambaye bado hajakamatwa) walimvamia na kumuua kwa kumkata sehemu mbalimbali za mwili Marehemu Ntungwa Jiria Kitoga (50), mkazi wa kijiji hicho, wakati wakitekeleza wizi wa ng'ombe 22. Ng'ombe hao walikutwa kwa mshtakiwa Shigela baada ya kukamatwa, na ushahidi dhidi yake uliweza kuthibitishwa mbele ya Mahakama. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amesema Jeshi la Polisi linaendelea na juhudi za kutoa elim...

DCP MISIME AWATAKA POLISI KATA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA MAADILI NA USHIRIKIANO KATIKA KATA ZAO.

Image
Msemaji wa Jeshi la Polisi Naibu Kamishna wa Polisi (DCP)  David Misime amewataka Polisi Kata kuzingatia maadili na kushirikiana na Viongozi wa Serikali za Mitaa waliopo katika maeneo yao ili kuhakikisha wanatekeleza kwa usahihi misingi ya uanzishwaji wa falsafa ya Polisi Jamii kwa kuhakikisha wanabaini, wanazuia na kutanzua uhalifu katika maeneo yao. Kauli hiyo imetolewa leo Agosti 25, 2025 alipokuwa katika ziara ya kikazi ya kuzungumza na Maafisa wa Polisi Jamii na Polisi Kata wa Kanda Maalum Dar es salaam katika ukumbi wa bwalo la Polisi barabara ya Kilwa Temeke Dar es salaam. DCP Misime amesema " Jukumu lako wewe Polisi Kata ni kujenga na kuimarisha ushirikiano na maadili katika Kata yako kwa kuhakikisha mnashirikiana vizuri na Viongozi wa Serikali na kufanya kazi kwa kuzingatia kauli mbiu ya Jeshi letu la Polisi ya nidhamu haki weledi na uadilifu". DCP Misime alipata fursa ya kufafanua maudhui yaliyomo katika kitabu cha mwongozo wa mafunzo ya Polisi Kata chenye lengo ...

MAJALIWA: ELIMU YA WATU WAZIMA NI ZANA YA MAENDELEO ENDELEVU.

Image
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema elimu ya watu wazima sio tu elimu ya masomo ya kawaida, bali ni zana muhimu ya maendeleo endelevu, kwani inachangia kipato, ustawi wa kijamii, afya na ushiriki wa kiraia.   ameongeza kuwa uzoefu duniani unaonesha kwamba elimu ya watu wazima ni chombo muhimu cha maendeleo ya kijamii, kiuchumi na binafsi.   Amesema hayo leo Jumatatu (Agosti 25, 2025) alipofungua kongamano la kilele cha maadhimisho ya miaka 50 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.   “Elimu si tukio la muda bali ni safari endelevu ya kujifunza katika maisha yote, elimu ya Watu wazima si kwa ajili ya watu wazima pekee, bali hata kundi la vijana wanaweza kujiunga na kunufaika na program mbalimbali za ujuzi zinazotolewa na taasisi hiyo”.   Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Serikali inatambua kwamba katika kipindi cha nusu karne iliyopita, Taasisi ya Elimu ya W...

NGOME YA CHAUMA SEGEREA YABOMOKA WANACHAMA 200 WATIMKIA CHADEMA

Image
WANACHAMA zaidi ya 200 wa CHAUMA  katika Jimbo la Segerea , wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, wamekihama  hicho na kurejea CHADEMA kwa madai ya kuto ridhishwa na mwenendo wa chama hicho. Aidha, wamesema hiyo ni season ya kwanza ya  wanachama katika jimbo hilo kuhama  CHAUMA  na kujiunga na vyama vingine vya siasa bali zinakuja season  nyingi ambazo zitabeba wimbi zito la wanachama  kukihama  Chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari  Dar es Salaam, leo Agosti 25,2025, kwa niaba ya wanachama hao walio hamia CHADEMA aliyekuwa Mwenyekiti wa  CHAUMA Kata ya Kinyerezi, Jimbo la Segerea,  Mndewa Mndewa ‘Dk. Timo’, ameeleza  wameamua kuhama kutokana na  mifumo mibovu. “Tumegundua mifumo ya uongozi ndani ya CHAUMA siyo ya kikatiba ila chama kipo kwa masalahi binafsi ya baadhi ya watu,”ameeleza Dk. Timo. Amewataka wananchi wa  Jimbo la Segerea kuto kuingia katika uchaguzi mkuu kwa mhemko  kwa kufuata wagombea wa...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

RAIS MWINYI AKUTANA NA WANAFUNZI WATAKAOITEMBELEA NASA, MAREKANI NA KUHUDHURIA HACKATHON, OMAN

Image
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema kuwa Serikali itaendelea kuunga mkono juhudi za kuwaandaa vijana wengi zaidi wa Zanzibar kuwa wataalamu wa elimu ya anga. Dkt. Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na wanafunzi watano waliochaguliwa kutembelea makao makuu ya NASA yaliyopo Washington D.C., Marekani, pamoja na kushiriki katika mashindano ya NASA International Space Apps Challenge 2025 yatakayofanyika jijini Ibra, Oman. Mkutano huo umefanyika Ikulu Zanzibar leo tarehe 25 Agosti 2025. Fursa hiyo imetokana na uwezo mkubwa waliouonesha waliposhiriki katika programu ya Kimataifa ya IASC (International Astronomical Search Collaboration) inayohusu uvumbuzi wa asteroids kwa kushirikiana na NASA (National Aeronautics and Space Administration) ya Marekani. Jumla ya wanafunzi 22 kutoka Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Karume, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na Chuo Kikuu cha Abdulrahman Al-Sumait ambao walishiriki kwa utambulisho wa Zanzibar ...

SERIKALI YAWEZESHA HUDUMA ZA POSTA KIDIJITALI KUPITIA VIFAA VYA TEHAMA KUTOKA UCSAF

Image
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry Silaa, amesema Serikali ya Awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha huduma za msingi ikiwemo Posta, Mawasiliano, intaneti na huduma za kifedha za kidijitali zinawafikia wananchi wote bila kujali jiografia. Waziri Silaa aliyasema hayo jijini Dar es Salaam, Agosti 22, 2025, katika hafla ya makabidhiano ya vifaa vya kisasa vya TEHAMA kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) kwenda Shirika la Posta Tanzania. Akizungumza katika hafla hiyo, Mtendaji Mkuu wa UCSAF alibainisha kuwa makabidhiano hayo ni sehemu ya mkakati wa kuimarisha huduma za mawasiliano na kidijitali, hususan maeneo ya pembezoni, ili kuongeza kasi, ufanisi na ubunifu wa huduma za Posta na kulifanya Shirika la Posta kuwa daraja la biashara mtandaoni kwa Watanzania wote. Kwa upande wake, Postamasta Mkuu, Bw. Macrice Daniel Mbodo, aliishukuru UCSAF kwa ushirikiano thabiti na kusisitiza kuwa vifaa hivyo vitasambazwa mara moja katika mikoa yote ya Posta nchini ili wana...

RC CHALAMILA ATANGAZA ZAWADI NONO KWA TAIFA STARS.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ametangaza kutoa zawadi ya shilingi milioni 20 pamoja na viwanja viwili kwa timu ya Taifa la Tanzania (Taifa Stars) mara baada ya kufunzu hatua ya robo fainali huku akiahidi motisha zaidi kulingana na matokeo ya mchezo wa leo dhidi ya Morocco. Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Agosti 22, 2025 RC Chalamila amesema kila bao litakolofungwa katika mchezo huo litazawadiwa shilingi  milioni 5 ambapo mfungaji atapokea milioni 1 na mtoa pasi ya bao (assit) atapokea shilingi laki 5. Aidha amebainisha kuwa kipa atakayefanikisha kuzuia bao bila kuruhusu nyavu zake kuguswa atajinyakulia zawadi ya gari jipya aina ya Toyota Crown. Zawadi hizi ni ishara ya heshima kubwa kwa Taifa Stars kwa kuendelea kutuwakilisha vizuri, nawashukuru kwa kushinda michezo 3 mfululizo. "Nawasihi watanzania kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Benjamini Mkapa kushangilia timu yetu" Alisema RC Chalamila.

Doyo Hassan Doyo Akidhi Vigezo vya Uteuzi, NLD Yashukuru Wananchi.

Image
Chama cha National League for Democracy (NLD) kimeeleza shukrani zake kwa wananchi waliojitokeza kwa wingi katika mikoa 10 ya Tanzania Bara na Visiwani kumdhamini Mheshimiwa Doyo Hassan Doyo, mgombea wake wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Zoezi la kukusanya wadhamini lilianza rasmi tarehe 10 Agosti 2025, mara baada ya Doyo kuchukua fomu ya uteuzi ambapo zoezi  hilo limehitimishwa rasmi leo, 22 Agosti 2025 jijini Dar es Salaam. Vilevile Mh.Doyo  alikamilisha kiapo chake katika Mahakama Kuu ya Tanzania, hatua inayomwezesha kuendelea na mchakato wa uteuzi. Mgombea huyo wa Urais wa NLD anatarajia kurudisha fomu ya uteuzi rasmi tarehe 24 Agosti 2025, jijini Dodoma, kisha kusubiri uamuzi wa Tume Huru ya Uchaguzi. Akizungumza kwa niaba ya chama, Don Waziri Mnyamani, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Taifa, NLD, alisema kuwa chama kinathamini moyo wa uzalendo, mshikamano na imani iliyoneshwa na wananchi katika hatua hii muhimu ya kisiasa.  Aliongeza kuwa NLD itaendelea...

*TUWAWEZESHE WAFANYAKAZI KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA- MAJALIWA.

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa wito kwa vyama vya wafanyakazi barani afrika kuweka mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya teknolojia duniani.   Amesema kwa kufanya hivyo kutawawezesha kupunguza hatari ya kupoteza ajira kutokana na ujio wa mashine pamoja na matumizi ya teknolojia mpya ikiwemo za akili mnemba.   Ameyasema hayo leo (Ijumaa 22 Agosti 2025,) Alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Afrika (OAUUT) uliofanyika Hoteli ya Johari Rotana Dar es Salaam.   Amesema kuwa, katika dunia ya sasa, imeshuhudiwa uwepo wa mabadiliko makubwa yanayochagizwa na mapinduzi ya kiteknolojia ikiwemo matumizi ya akili mnemba pamoja na utandawazi.   “Kuna hatari ya watu kupoteza ajira zao kadri mitambo na mifumo ya kisasa inavyochukua kazi ambazo kwa kawaida zingeweza kufanywa na wafanyakazi. Tunapaswa kuweka mpango wa kutoa mafunzo endelevu yanayoendana na mabadiliko ya teknolojia ili kuwandaa wafanyakazi na ain...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO

Image
 

BASHUNGWA AHIMIZA VYAMA VYA SIASA KUSHIRIKI KAMPENI ZA UCHAGUZI BILA KUHATARISHA AMANI.

Image
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Innocent Bashungwa amevihimiza Vyama vya Siasa pamoja na Wagombea wa Urais, Ubunge na Udiwani kunadi sera zao kwa Wananchi bila kutumia lugha ya matusi au kuanzisha vurugu zinazoweza kuhatarisha amani, pia amewasisitiza Wananchi kushiriki katika shughuli za kisiasa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu na kushiriki kupiga kura Oktoba 29, 2025. Bashungwa ametoa wito huo leo, tarehe 22 Agosti 2025, mara baada ya kuzindua jengo la Kituo cha Polisi Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa jukumu la ulinzi wa Taifa ni la Watanzania wote, siyo Serikali, Jeshi la Polisi au vyombo vingine vya ulinzi na usalama. “Wananchi wote muwe huru kushiriki katika shughuli za siasa hususan wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, zitakazoanza wiki ijayo pamoja nasiku ya kupiga kura Oktoba 29, 2025. Ni matumaini yangu kwamba vyama vya siasa na wagombea wao wa Uraisi, Ubunge, Udiwani watajielekeza kunadi sera zao, na sio matusi ama kusababisha vurugu na uvunjifu wa a...

WAZIRI KIKWETE: SERIKALI YA AWAMU YA SITA INAJIVUNIA USHIRIKIANO WA WATUMISHI.

Image
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Ridhiwani Kikwete ameipongeza Menejimenti na watumishi wa Ofisi hiyo kwa ushirikiano uliofanikisha Serikali ya Awamu ya Sita kupata mafanikio katika sekta za Kazi, Vijana, Ajira, Watu wenye Ulemavu na kinga ya Jamii. Ameeleza mafanikio hayo wakati wa kikao cha pamoja na watumishi wa Ofisi hiyo leo Agosti 21, 2025 ikiwa na lengo la kuwashukuru watumishi na kuwapongeza kwa kutekeleza shughuli kwa ufanisi na tija katika kipindi chote alicho hudumu na kuiongoza Ofisi. Mheshimiwa Ridhiwani amesema kuwa katika miaka minne ya Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi imepata mafanikio makubwa ikiwemo kupunguza kodi ya mishahara kutoka asilimia 18 hadi 9, kutoa vibali 55,642 kwa wageni waliokuja kufanya kazi na kupunguza muda wa utoaji wa vibali vya kazi kutoka miezi miwili hadi siku 14. Mafanikio mengine, Ofisi imefanikiwa kutoa mikopo nafuu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vij...