Posts

Showing posts from June, 2025

DKT. KIMAMBO: MAAFISA USTAWI WA JAMII MUHIMBILI ZINGATIENI WELEDI, UPENDO NA MOYO WA HURUMA KWA WAGONJWA.

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,(MNH) Dkt. Delilah Kimambo, amewataka watumishi wa ustawi wa jamii hospitalini hapo kuzingatia weledi na kuonyesha moyo wa huruma na upendo wakati wa kuwahudumia wateja wanaofika kupatiwa huduma katika ofisi zao. Dkt. Kimambo ameyasema hayo leo Juni 27, 2025, wakati wa kikao cha pamoja na wafanyakazi wa idara hiyo, ikiwa ni sehemu ya mpango wake wa kuboresha mawasiliano ya ndani na kufanikisha uwajibikaji na uwazi katika utoaji wa huduma. "Tujishushe kwenye viwango vya hawa watu, tuwahudumie kwa kujali na kwa upendo. Tutajua kwa kina shida zao na jinsi ya kuwasaidia kuendana na mahitaji yao. Nyie ni kitengo muhimu sana, nyie ndio watetezi wa wateja wetu, mnatakiwa kuwa sauti yao pale wanapokosa nguvu, na kuwa faraja yao pale wanapokata tamaa," amesema Dkt. Kimambo. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Ukunga na Uuguzi, Bi Redemptha Matindi, amemshukuru Dkt. Kimambo kwa kutenga muda kuzungumza na wafanyakazi hao, na kusis...

WCF YAPONGEZWA KWA MAFANIKIO MAKUBWA NA MCHANGO KWA WATU WENYE ULEMAVU.

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Ridhiwani Kikwete, ameupongeza Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kipindi cha miaka 10 tangu kuanzishwa kwake. Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa vifaa saidizi kwa watu wenye ulemavu Juni 25, 2025 iliyofanyika katika Chuo cha Marekebisho kwa Watu Wenye Ulemavu cha Sabasaba mkoani Singida. Mhe. Kikwete alisema WCF imekuwa mfano wa taasisi zinazotekeleza kwa vitendo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kumlinda mfanyakazi na kukuza usawa kwa makundi yote ya jamii "Nitoe wito Kwa Taasisi nyingine kuiga mfano wa WCF wakurejesha Kwa jamii, iwe ni kwa huduma, vifaa au fursa mbambali" alisema Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, alishukuru Serikali kwa kuwezesha watu wenye ulemavu kupata nafasi zitakazowawezesha kushiriki kikamilifu katika shughuli za kiuchumi na kijamii bila kujali hali zao. Naye Dkt. Mduma amesema M...

Ndoa za Utotoni Zikome: Wadau Wanena kwa Sauti Moja.

Image
Na Fidea Masunga,Dar es Salaam Katika harakati za kulinda haki za mtoto wa kike na kuhakikisha ndoto zao hazikatizwi mapema, Mtandao wa Kutokomeza Ndoa za Utotoni Tanzania (TECMN) umefanya kikao maaalum cha kuthibitisha Mpango Mkakati wa Uchechemuzi na Mawasiliano kitakachotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitatu. Kikao hicho kilichofanyika jijini Dar es Salaam kimewakutanisha wadau kutoka mashirika ya kiraia, taasisi za kiserikali, viongozi wa dini pamoja na watoto wenyewe,sauti ambazo mara nyingi hazisikiki kwenye meza za maamuzi. Adeline na Adela, watoto wawili waliokuwa miongoni mwa washiriki, walitoa ushuhuda wa kugusa moyo kuhusu madhila ya ndoa za utotoni ambaoo Walisema watoto wengi hupoteza mwelekeo wa maisha kutokana na kuozeshwa mapema, huku wakiomba serikali kuchukua hatua kali dhidi ya wazazi wanaoruhusu vitendo hivyo. “Tunaomba tulindwe. Tunataka kusoma, sio kuolewa,”  alisema Adela. Nae mtoto Adeline aliiomba serikali na wanaharakati mbalimbali wakutetea haki za watoto...

WEATHER FORECAST FOR THE NEXT 24 HOURS STARTING AT 9.00 P.M DATE: 26/06/2025.

Image
 

TRC KUANZA USAFIRISHAJI WA MIZIGO KWA SGR KATI YA DAR ES SALAAM NA DODOMA.

Image
 

SERIKALI YAWAREJESHA WATANZANIA 42 KUTOKA NCHINI IRAN NA ISRAEL.

Image
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imefanikiwa kuwarejesha salama nchini Watanzania 42 kutoka nchini Israel na Iran kufuatia vita vilivyokuwa vikiendelea baina ya mataifa hayo mawili. Akizungumza mara baada ya kuwapokea Watanzania hao kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Samwel Shelukindo amesema zoezi la kuwarejesha Watanzania wote salama nchini ni utekelezaji wa agizo maalumu la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuhakikisha kwamba Watanzania wote waliopo katika mataifa hayo mawili wanarejeshwa nchini salama. Aidha Balozi Shelukindo amesema leo juni 25, 2025 wameingia Watanzania makundi mawili, kundi moja liliwasili mchana wa leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume na kwamba gharama zote za kuwarejesha Watanzania hao zimegharamiwa na serikali na kuongeza kuwa Watanzania wengine kutokea nchini Ir...