Posts

Showing posts from July, 2025

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es alaam Mhe Albert Chalamila amewataka wenyeviti wa Serikali za mitaa pamoja na watendaji wa Kata Mitaa Mkoani humo kusimamia ulinzi na usalama kwenye ngazi ya mitaa na kata ili kuhakikisha Mkoa huo unakua Salama bila uwepo wa matukio ya uvunjifu wa amani wakati wote. Akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika kikao kazi na Wenyeviti, Watendaji wa Kata na mitaa kilichofanyika kwenye ukumbi wa Diamomd Jubilee RC Chalamila amesema suala la ulinzi na usalama linapaswa kuanzia kwenye ngazi ya mitaa na kata hivyo amewataka viongozi hao wa mitaa kusimamia suala hilo kwani katika baadhi ya mitaa kumekua na matukio ya uvunjifu wa amani. RC Chalamila amewataka viongozi hao ngazi ya Mitaa na Kata kusaidia kutatua changamoto za wananchi na sio wao kuwa ni chanzo cha kuongeza changamoto kwa wananchi ambapo pia ametumia nafasi hiyo kuwataka wenyeviti na watendaji kutambua kuwa mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi hivyo waendelee kuhimiza wananchi kuanzia ngazi ya mtaa kushiriki ucha...

CCM Yavunja Rekodi ya Uchukuaji Fomu, Zaidi ya 20,000 Wajitokeza Kugombea Nafasi za Ubunge na Udiwani.

Image
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimetangaza kukamilisha kwa mafanikio makubwa zoezi la uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2025, huku zaidi ya wanachama  20,000 wakijitokeza kuwania nafasi hizo. Zoezi hilo lilianza tarehe  28 Juni  na kukamilika rasmi  Julai 2 , likihusisha nafasi za  Udiwani, Ubunge, Uwakilishi , pamoja na  Viti Maalum  kwa upande wa Tanzania Bara na Zanzibar. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam,  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Amos Makalla , alisema kuwa idadi hiyo kubwa ya waombaji ni ishara tosha kuwa CCM bado kinaaminiwa sana na Watanzania wa makundi yote. “Tumevunjwa rekodi. Hamasa imekuwa kubwa kuliko wakati wowote wa nyuma. Tumeshuhudia makundi mbalimbali yakijitokeza kwa wingi vijana, wanawake, wasanii, bodaboda, machinga, wakulima na wengineo. Hii ni dalili kuwa CCM ni chama imara, chenye sera thabiti na matumaini ya Watanzania,” alis...

Matarajio ya Hali Mbaya ya Hewa kwa Siku Tano.

Image
 

DIWANI MSTAAFU BENARD MWAKYEMBE ATIA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA TEMEKE.

Image
Na Fidea Masunga, Dar es Salaam Diwani mstaafu wa Kata ya Mtoni, Benard Mwakyembe, ametangaza rasmi nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Temeke kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),akiahidi kuleta mageuzi chanya katika sekta ya miundombinu, ajira kwa vijana, elimu na usimamizi wa fedha za maendeleo ya jamii. Akizungumza mara baada ya kurejesha fomu ya kugombea, Mwakyembe amesema kuwa endapo atapata ridhaa ya wananchi wa Temeke, atahakikisha kuwa miradi ya miundombinu hasa barabara, mifereji ya maji na huduma za kijamii inaboreshwa kwa kiwango kikubwa ili kurahisisha maisha ya wakazi wa jimbo hilo. “Jimbo letu lina changamoto nyingi, lakini kubwa zaidi ni ukosefu wa miundombinu bora, ajira kwa vijana, na usimamizi hafifu wa asilimia 10 ya mapato ya halmashauri yanayopaswa kwenda kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu. Nitahakikisha fedha hizi zinawafikia walengwa kwa wakati na kwa uwazi,” alisema Mwakyembe. Aidha, ameweka mkazo katika suala la elimu, akiahidi kushirikiana na wadau mbalim...

Tamko la TLS juu ya kushambuliwa kwa waumini wa Kanisa la Ufufuo na Uzima.

Image

IGP WAMBURA AWAVISHA CHEO MAAFISA WATATU WALIOPANDISHWA CHEO NA RAIS DKT. SAMIA.

Image
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Camillus Wambura amewavisha cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) maafisa watatu waliopandishwa kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) leo Julai 1, 2025. Maafisa waliopandishwa cheo ni pamoja na Mkuu wa Kikosi cha Polisi Wanamaji, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Moshi Nsabi Sokoro, Mkuu wa Kikosi cha Matengenezo ya Magari ya Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Tuntufye Absalome Mwakagamba na Mkuu wa Kikosi cha Bendi, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Msolo Hamis Msolo. IGP Wambura amewavisha cheo hicho baada ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, kuwapandisha cheo maafisa hao Julai 1, 2025.

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image

Dkt. Yonazi Atoa Wito kwa Watumishi Kujenga Tabia ya Kujifunza Ili Kuimarisha Uwajibikaji Serikalini.

Image
Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi, amewataka watumishi wa umma kujenga tabia ya kujifunza kwa bidii ili kuongeza ufanisi na uwajibikaji katika utekelezaji wa majukumu ya serikali. Dkt. Yonazi ametoa wito huo leo jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa PEPMIS yaliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Ngome. Akihimiza dhana ya kujifunza kwa kushiriki kikamilifu, Dkt. Yonazi alinukuu kauli maarufu ya Benjamin Franklin isemayo: “Niambie nisahau, nifundishe nitakumbuka, nishirikishe nijifunze.”   Alisisitiza umuhimu wa ushiriki wa kila mmoja akisema: “Tuchukue sehemu ya tatu ya kauli hiyo kwa sababu tunachohitaji ni kujihusisha ili tuweze kujifunza zaidi na kuimarisha utendaji wetu.” Aidha, Dkt. Yonazi aliwataka watendaji wote kuchangamkia fursa hiyo ya mafunzo ya PEPMIS ili kupata maarifa mapya yatakayosaidia katika kutathmini na kuboresha utendaji kazi wao wa kila siku. Kwa upande wake, Bw. Mutani Josephat Manyama...

BASHUNGWA ACHUKUA FOMU KUTETEA UBUNGE JIMBO LA KARAGWE..

Image
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), Innocent L. Bashungwa amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya kutetea nafasi ya Ubunge katika Jimbo la Karagwe, mkoani Kagera kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM). Bashungwa amechukua fomu hiyo na kuirejesha kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Karagwe, Ndugu Anatory Nshange, leo tarehe 01 Julai 2025. Bashungwa amekuwa mwakilishi wa wananchi wa Jimbo la Karagwe kwa vipindi viwili mfululizo kuanzia mwaka 2015 hadi 2020 na 2020 hadi 2025, ambapo ameaminiwa kushika nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama na Serikali ikiwa ni pamoja na Naibu Waziri wa Kilimo; Waziri wa Viwanda na Biashara; Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo; Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo; Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI; Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa; Waziri wa Ujenzi; na kwa sasa ni Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.