Posts

Showing posts from December, 2025

KAULI ZA ASKOFU RUWA’ICHI ZIMEIBUA SINTOFAHAMU KATI YA WAUMINI.

Image
DAR ES SALAAM.  Kauli zinazodaiwa kuwa matusi na vitisho zilizotolewa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, wakati wa Misa ya Krismasi, zimeibua sintofahamu kubwa na wasiwasi kwa baadhi ya waumini. Waumini wanasema maneno hayo yamejeruhi imani yao na kuharibu mshikamano madhabahuni, huku wakitaka viongozi wa Kanisa kurejea kwenye misingi ya mafundisho ya Kikristo. Wakizungumza na wanahabari Desemba 27, 2025, waumini Mackdeo Shilinde na Gerald Abel wamesema maneno hayo yamekiuka misingi ya mafundisho ya Kikristo na maadili ya uongozi wa kiroho. Walisema badala ya kujibu hoja halali zilizowasilishwa kwa Balozi wa Vatican, Askofu alitumia mimbari kueneza lugha ya chuki, hofu na udhalilishaji. Waumini hao wamesisitiza kuwa mimbari ya Kanisa Katoliki ni mahali patakatifu patakapohubiriwa Neno la Mungu, kuimarisha imani, kuwafariji waumini na kuwaongoza katika njia ya upendo, uvumilivu na mshikamano. Wamesema mimbari haiwezi kuwa jukwaa la kusham...

BONDIA MWAKINYO KUIPEPERUSHA BENDERA YA TANZANIA KESHO KATIKA PAMABANO LA KIMATAIFA DHIDI YA MNAIJERIA STANLEY ERIBO.

Image
Bondia wa kimataifa Hassan Mwakinyo ataipeperusha bendera ya Tanzania dhidi ya mpinzani wake kutoka Nigeria, Stanley Eribo, katika pambano la Boxing on Boxing Day litakalofanyika kesho, Desemba 26, 2025, kwenye Ukumbi wa Warehouse, Masaki jijini Dar es Salaam. Mwakinyo, ambaye ameongoza mabondia wengine leo kupima uzito, amesema yuko tayari kikamilifu kwa pambano hilo, akiahidi ushindi kwa Watanzania. Akizungumza mara baada ya zoezi la upimaji uzito, Mwakinyo alisema, “Nimejiandaa vizuri sana kwa pambano hili. Nimemuandaa mpinzani wangu kikamilifu na nawahakikishia Watanzania ushindi mkubwa. Nitaingia ulingoni kuipigania heshima ya taifa.” Kwa upande wake, bondia wa Tanzania Hamadi Furahisha alisema maandalizi yake yamekamilika na yuko tayari kukabiliana na mpinzani wake kutoka Malawi, Hanock Phiri. “Najua ninampinzani mkali, lakini niko tayari kumpa pambano gumu na kuwaburudisha mashabiki,” alisema Furahisha. Naye bondia kutoka Nigeria, Stanley Eribo, alisema amekuja Tanzani...

DKT. MWIGULU NCHEMBA ATOA WITO KUDUMISHA AMANI, AWAHIMIZA VIONGOZI WA DINI KUPINGA MIGAWANYIKO.

Image
Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu ya umoja na amani, kupinga chuki, migawanyiko na vitendo vyovyote vinavyoweza kuvuruga mshikamano wa Taifa. Amesema vita au migogoro inayohusisha wananchi wa taifa moja haina mshindi, bali husababisha hasara kwa wote na kuacha majeraha ya kudumu katika jamii. Aidha, mgawanyiko wa kitaifa huathiri maendeleo na ustawi wa nchi kwa ujumla. Dkt. Nchemba ametoa wito huo leo, Alhamisi Desemba 25, 2026, aliposhiriki Ibada ya Sikukuu ya Krismasi iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiinjili la Kilutheri la Azania Front jijini Dar es Salaam. “Manufaa ya amani ni makubwa. Amani huleta maendeleo ya kiuchumi, huimarisha ustawi wa jamii na huwezesha kila Mtanzania kushiriki kikamilifu katika kujenga Taifa,” amesema. Ameeleza kuwa Serikali itaendelea kutekeleza wajibu wake wa kulinda amani na usalama wa nchi, huku ikiendelea kuwajengea Watanzania, hususan vijana, misingi ya uza...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

WAJASIRIAMALI DAR WALAANI MACHAFUKO YA OKTOBA 29, WASISITIZA AMANI NA MAENDELEO.

Image
Wajasiriamali wa kada mbalimbali kutoka wilaya zote tano za Mkoa wa Dar es Salaam wamelaani vikali machafuko ya  Oktoba 29 , wakisema yameathiri maisha ya wananchi, biashara, ajira na uchumi wa mkoa pamoja na Taifa. Wakiwasilisha tamko lao hilo kwa wanahabari    jijini Dar es Salaam kwa niaba ya wajasiriamali wa mkoa huo akiwemo Mohamed S. Mohamed wa Temeke, Hussein Bambe wa Ubungo, Zahra Sadicky wa Kigamboni, Bakari Sufiani Mofi wa Ilala na Sharifu Hassan wa Kinondoni wamesema machafuko hayo yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu ya umma, ikiwemo mabasi ya mwendokasi (BRT), hali iliyowalazimu wananchi kukosa huduma muhimu za usafiri huku watumishi wengi wakipoteza ajira au vyanzo vya kipato. Wamesema uharibifu huo umeiacha jamii na mzigo mkubwa wa kiuchumi, huku wafanyabiashara wengi wakipoteza mitaji na mali waliyojenga kwa muda mrefu ndani ya kipindi kifupi. Aidha, wajasiriamali hao wamesema uchomaji wa moto kwenye biashara na taasisi za kazi umesababisha wafany...

SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TNCC KUTENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAEKEZEZAJI NA SEKTA BINAFSI.

Image
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara yaahidi kushirikiana na Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC)  kutoa mazingira rafiki kwa wawekezaji na sekta binafsi , hatua inayolenga kufanikisha dira ya taifa ya mwaka 2050 ya kuwa na uchumi imara, shindani na jumuishi. Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb),wakati wa ziara yake katika Ofisi za TNCC Desemba 22, 2025, jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kuwa Serikali inalenga kuachana na uchumi unaotegemea rasilimali asilia na kuelekea kwenye uchumi unaojengwa juu ya uzalishaji, kuongeza thamani ya bidhaa za ndani, na kushindana kimataifa. Aidha, Mhe. Kapinga aliongeza kuwa  ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na sekta binafsi , kupitia TNCC, ni muhimu katika kuimarisha uzalishaji wa ndani, kuvutia uwekezaji, na kuhakikisha sekta binafsi inapata mazingira yanayochochea ushindani na ukuaji endelevu. Kwa upande wake, Rais wa TNCC, Bw. Vicent Minja, alisema chemba hiyo imeendelea kuw...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

NAIBU WAZIRI KATAMBI AIPONGEZA TIRDO, AAGIZA KUFUFUA VIWANDA VILIVYOKUFA.

Image
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Patrobas Katambi, ameliagiza Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kuchunguza viwanda vilivyokufa na kutoa  ushauri wa kitaalamu  ili viweze kurejea kwenye uzalishaji, kutoa ajira, na kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa. Akizungumza wakati wa ziara yake katika TIRDO Desemba 22, 2025, Katambi alisema kero kubwa kwa wananchi ni kuona viwanda vipo lakini havifanyi kazi, ilhali vinaweza kutoa ajira na kusaidia uchumi wa nchi. Aidha, Mhe. Katambi  aliipongeza TIRDO  kwa jitihada zake za kusaidia sekta ya viwanda nchini kupitia tafiti za teknolojia zinazofaa na kusambaza matokeo kwa wadau wa ndani na nje ya nchi. Alisisitiza kuwa juhudi hizo zinapaswa kuendelezwa ili kufanikisha matokeo chanya na kujenga uhimilivu wa viwanda. Naibu Waziri pia  aliitaka TIRDO  kutoa ushauri wa kitaalamu unaozingatia viwango vya sayansi na teknolojia, kusaidia viwanda kuwa na uhimilivu na kurahisisha ushindani katika m...

WAUMINI WA KANISA KATOLIKI WAIANDIKIA VATICAN WAKITAKA UCHUNGUZI WA MWENENDO WA PADRI KITIMA.

Image
DAR ES SALAAM  Waumini wawili wa Kanisa Katoliki nchini, Stanslaus Thobias Nyakunga na Elia Phaustine Kabote, wameiandikia Vatican kupitia Balozi wake nchini Tanzania, Archbishop Angelo Accattino, wakiomba kufanyika kwa uchunguzi wa kichungaji na kiutawala kuhusu mwenendo wa Padri Dkt. Charles Kitima, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), wakieleza hofu ya Kanisa kuonekana kuhusishwa na misimamo ya vyama vya siasa. Katika barua hiyo, waumini hao wameeleza kuwa kwa kipindi kirefu kumekuwapo mitazamo katika jamii inayodai kuwa Padri Kitima amekuwa akionekana kuingilia au kujihusisha na masuala ya siasa, hususan migogoro ya ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), jambo ambalo, kwa mujibu wao, halijajitokeza kwa kiwango kama hicho kwa vyama vingine vya siasa. Wamefafanua kuwa madai hayo, bila kujali kama yana ukweli au la, yameanza kuathiri taswira ya Kanisa miongoni mwa waumini na kwa umma, hali inayoweza kulifanya Kanisa lionekane kama linachukua upande w...

FCC YAPOKEA TUZO MAALUM KWA MCHANGO WAKE KATIKA KUIMARISHA SEKTA YA MANUNUZI NA UGAVI.

Image
TUME ya Ushindani (FCC) imetunukiwa tuzo maalum ya kutambua mchango wake katika maendeleo na uimarishaji wa Sekta ya Manunuzi na Ugavi nchini, ikiwa ni ishara ya kutambua juhudi zake katika kulinda na kusimamia ushindani wa haki, uwazi na ufanisi ndani ya sekta hiyo muhimu kwa uchumi wa Taifa. Tuzo hiyo ilikabidhiwa na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Mshamu Munde, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, na kupokelewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha FCC, Bi. Roberta Feruzi, katika hafla rasmi ya utoaji wa tuzo iliyofanyika jijini Arusha. Hafla hiyo iliambatana na Kongamano la 16 la Wataalamu wa Manunuzi na Ugavi, lililofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC), na kuandaliwa na Bodi ya Wataalamu na Mafundi wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), likiwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya manunuzi na ugavi kutoka ndani na nje ya nchi. Katika kongamano hilo, FCC ilishiriki kama mdau muhimu wa sekta ya manunuzi na ugavi, ambapo iliwasilisha mada kuhusu umuhimu wa kuzingatia us...