Posts

Showing posts from October, 2025

POLISI: HALI YA USALAMA NI SHWARI, TAARIFA ZA MITANDAONI NI UZUSHI.

Image
Jeshi la Polisi nchini limewahakikishia wananchi kuwa hali ya usalama ni shwari kuelekea siku ya kupiga kura kesho, Oktoba 29, 2025, na kwamba hakuna tishio lolote la kiusalama. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, jeshi hilo limeeleza kuwa maandalizi yote muhimu ya kiusalama yamekamilika na askari wapo tayari kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu. Jeshi hilo limeonya kuhusu kundi la watu wanaoandaa na kusambaza picha na taarifa za matukio ya zamani au ya kutungwa kwa nia ya kupotosha umma na kuleta taharuki. Baadhi ya taarifa hizo zimekuwa zikionekana kwenye mitandao ya kijamii zikiwa na sauti au maandishi yanayoashiria kuwa yametokea hivi karibuni, ilhali si kweli. Aidha, imeelezwa kuwa wapo watu wanaotengeneza video na picha zenye sura za viongozi na kuzihariri kwa kuziweka sauti na maneno ya kupotosha ili ionekane ni kauli halisi za viongozi hao. Jeshi la Polisi limewataka wananchi kupuuza taarifa za aina hiyo,...

HOSPITALI YA BENJAMIN MKAPA NA INTERBURNS YA UINGEREZA WAKUBALIANA KUBORESHA HUDUMA ZA MATIBABU YA MAJERAHA YA MOTO.

Image
Dodoma. Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) kwa kushirikiana na Interburns Society ya Uingereza zimesaini hati ya makubaliano (MoU) yenye lengo la kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa wenye majeraha ya moto, ikiwemo kuanzisha kitengo na wodi maalumu kwa ajili ya huduma hizo. Hati hiyo imesainiwa jijini Dodoma, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, kama sehemu ya mpango wa kuimarisha utoaji wa huduma za kibingwa na kuongeza uwezo wa kitaalamu katika matibabu ya majeraha makubwa ya moto nchini. Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Benjamin Mkapa, Prof. Abel Makubi, alisema makubaliano hayo yatachangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha huduma kwa wagonjwa na kukuza ujuzi wa wataalamu wa afya. Kwa upande wake, Afisa Mtendaji Mkuu wa Interburns Society, Bi. Tina Bajec, alieleza kuwa taasisi yake imejipanga kushirikiana na Tanzania katika kuboresha huduma za afya, hususan kwa wagonjwa walioungua moto. Naye, Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moto hospitalin...

MWARUBAINI DHIDI YA UKATILI MTANDAONI WAPATIKANA.

Image
Na Mwandishi Wetu. Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Kitengo cha Makosa ya Kimtandao kimechukua hatua madhubuti kukabiliana na matukio ya ukatili mtandaoni kwa kutumia vifaa maalum vya kisasa vya uchunguzi, kutoa elimu kwa umma, na kushirikiana na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi zinazoratibu matumizi salama ya mitandao ya kijamii. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo hicho, matukio ya ukatili mtandaoni yameendelea kushuhudiwa nchini, yakiwemo vitendo vya udhalilishaji, matusi, vitisho, na uenezaji wa taarifa za uongo. Waathirika wakubwa wa vitendo hivyo ni wanawake, vijana na watu mashuhuri katika jamii. Aidha, Jeshi la Polisi limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya ukatili mtandaoni na hatua za kuchukua pindi matukio hayo yanapotokea, likihimiza matumizi chanya ya mitandao kwa kuijenga jamii badala ya kuieneza chuki. Vilevile, jeshi hilo limeitaka jamii kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya ukatili huo kwa kuripoti matukio yote ya ukatili mtand...

CWT MANYARA YATOA WITO KWA WALIMU KUJITOKEZA KUPIGA KURA KESHO

Image
Na Mwandishi Wetu, Manyara. Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Manyara kimetoa wito kwa walimu wote mkoani humo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kikatiba la kupiga kura litakalofanyika kesho, Oktoba 29, 2025, kwa ajili ya kuwachagua viongozi wanaowataka. Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Manyara, Mwalimu Theofil Joseph Amo, ametoa wito huo leo, akisisitiza umuhimu wa walimu kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa amani na utulivu. Amo amewataka walimu kupuuza waraka unaosambaa mitandaoni unaodaiwa kutoka kwa chama hicho, akibainisha kuwa ni taarifa potofu na si kauli rasmi ya uongozi wa CWT. Ameongeza kuwa chama hicho kinaamini katika misingi ya uwazi, umoja na ushiriki wa kila mwanachama katika maamuzi muhimu, ikiwemo uchaguzi wa viongozi wao.

RC MRINDOKO: HALI YA USALAMA NI SHWARI, WANANCHI WAHIMIZWA KUWAHI VITUONI KUPIGA KURA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Mhe. Mwanamvua Mrindoko, ameendelea kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kushiriki katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho, tarehe 29 Oktoba 2025. Akizungumza katika mahojiano maalum kupitia kituo cha redio cha Mpanda FM, RC Mrindoko ametoa wito kwa wananchi wote wa Mkoa wa Katavi kuhakikisha wanawahi mapema katika vituo vyao vya kupigia kura, kwani vituo hivyo vitafunguliwa kuanzia saa moja asubuhi.  Amehimiza wananchi kutekeleza wajibu wao huo kwa amani, utulivu na uzalendo, ili uchaguzi uwe wa mfano wa demokrasia nchini. "Tunawahimiza wananchi wote wajitokeze mapema siku ya uchaguzi. Ni muhimu tushiriki kwa amani, tukidumisha mshikamano na upendo katika mkoa wetu," amesema RC Mrindoko. Amebainisha kuwa maandalizi yote muhimu kwa ajili ya uchaguzi yamekamilika, na vyombo vya ulinzi na usalama vimejipanga kuhakikisha zoezi hilo muhimu la kidemokrasia linafanyika kwa utulivu na usalama wa kutosha. Akizungumzia kata za Katum...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

NLD Yafunga Kampeni Handeni: Doyo Aahidi Serikali ya Uwajibikaji, Uwazi na Ufanisi.

Image
Handeni, Tanga Chama cha NLD leo kimefunga rasmi kampeni zake za urais katika mkutano mkubwa uliofanyika Misima, wilayani Handeni, mkoani Tanga. Akizungumza katika mkutano huo, Mgombea Urais wa NLD, Mhe. Doyo Hassan Doyo, amesema endapo wananchi watamchagua kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, serikali yake itakuwa serikali jumuishi, yenye uwajibikaji, uwazi na ufanisi, itakayoweka wananchi kwanza katika kila hatua ya maamuzi. Mhe. Doyo amesema serikali yake itaanza kwa kupunguza matumizi yasiyo na tija ili kuhakikisha kila shilingi ya umma inaleta matokeo chanya kwa wananchi.  “Serikali yangu itakuwa ya mfano. Nitaanza mimi mwenyewe kwa kuonyesha nidhamu ya matumizi na uwazi wa fedha za umma. Tutapunguza gharama zisizo na maana ambazo zimekuwa mzigo kwa wananchi,” alisema Mhe. Doyo. Amebainisha pia kuwa hana tatizo na wagombea wengine wanaonukuu au kutumia baadhi ya sera zake, akisisitiza kuwa sera za NLD zinatokana na utafiti wa zaidi ya miaka mitatu kupitia Ilani ya Cha...

TAHADHARI YA HALI MBAYA YA HEWA KWA SIKU TANO: MVUA NA MAWIMBI MAKUBWA INATARAJIWA KUANZA OCTOBER 27 – 31, 2025

Image

WATANZANIA WAMETAKIWA KULINDA AMANI KABLA NA BAADA YA UCHAGUZI.

Image
Na Fidea Masunga, Kibaha Wakati taifa likielekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Watanzania wametakiwa kuendelea kudumisha na kuilinda amani kabla, wakati na baada ya uchaguzi ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na utulivu na mshikamano wa kitaifa. Wito huo umetolewa na Mchungaji  John  Makomele ambae ni Mchungaji Kiongozi wa  Kanisa la Baptist  lililopo  Lulanzi, Kibaha mkoani Pwani , wakati wa maadhimisho ya  miaka tisa (9)  tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo. Akizungumza katika maadhimisho hayo, Mchungaji    Makomele alisema ni jukumu la kila Mtanzania kuhakikisha anachangia katika kudumisha amani kwa maneno, matendo na mwenendo unaoleta umoja, hasa kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. “Uchaguzi ni tukio la kidemokrasia linalopaswa kuleta umoja na siyo chuki. Tuwaheshimu viongozi wetu, tuombe kwa ajili ya taifa, na tuwe walinzi wa amani,” alisema Mchungaji Makomele. Aidha, aliwataka viongozi wa dini kuendelea kuhubiri upendo, uadilifu n...

ELIMU YA NISHATI SAFI YA KUPIKIA YAWAFIKIA MAAFISA DAWATI NGAZI YA MIKOA NA HALMASHAURI

Image
Wizara ya Nishati imeanza kutoa elimu kuhusu Nishati Safi ya Kupikia     kwa     Maafisa Dawati wa Nishati Safi ya Kupikia ngazi ya mikoa na halmashauri     kwa lengo la kuwa na uelewa wa pamoja katika utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia pamoja na     kuwawezesha Maafisa Dawati kutambua majukumu yao katika utekelezaji wa mkakati.. Akifungua    mafunzo hayo, wilayani Kibaha mkoani Pwani,    Mwakilishi wa Katibu Tawala wa Mkoa wa    Pwani, Bi. Hadija Mruma ameipongeza Wizara ya Nishati kwa jitihada mbalimbali inazochukua kwa vitendo katika kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia nchini mojawapo ikiwa ni kuhakikisha elimu na vifaa vya nishati safi ya kupikia vinafika hadi ngazi za Mikoa, Halmashauri na Vijiji. Ameeleza kuwa Mkoa wa Pwani unachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kuwa wanachi wanatumia nishati safi ya kupikia katika ngazi ya taasisi, kaya n.k akitoa mfano kuwa asilimia 76 ya ta...

RC CHALAMILA "JITOKEZENI KWA WINGI KUPIGA KURA OCTOBA 29,2025 DAR NI SALAMA SANA.

Image
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi wakazi wa Mkoa huo kupuuza taarifa za uzushi zinazotolewa na baadhi ya watu kupitia mitandao ya kijamii kuwa uchaguzi utakua na vurugu badala yake wajitokeze kwa wingi kupiga kura kwani Mkoa huo uko Salama sana wakati wote kabla ya uchaguzi,wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi. Akizungumza Jijini Dar es Salaam katika mkutano na waandishi wa habari RC Chalamila amesema Mkoa huo una wapiga kura zaidi milioni nne na kwamba tayari    tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi imeshakamilisha miundombinu kwa ajili ya wananchi    kupigia kura ndani ya Mkoa huo hivyo amewataka wananchi kujitokeza kupiga kura bila kuhofia usalama wao kwani vyombo vya ulinzi vimejipanga vizuri kuimarisha amani. Aidha RC Chalamila amevionya vikundi vinavyotishia kuvuruga wakati wa uchaguzi kupitia mitandao ya kijamii na kubainisha kuwa vyombo vya dola viko macho kuchukua hatua dhidi ya mtu anayebainika kufanya au kutaka kuleta vurugu...

JESHI LA POLISI KANDA MAALUM YA DAR ES SALAAM LIMEMKAMATA NIFFER KWA TUHUMA ZA KUHAMASISHA VURUGU KATIKA UCHAGUZI MKUU 2025.

Image
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, chini ya Kamanda Jumanne Muliro, limekamata Jenifer Bilikwiza Jovin, anayejulikana kwa jina la umaarufu Niffer, kufuatia tuhuma za kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es Salaam.  Tukio hilo la kumkamata limefanyika katika eneo la Sinza, ikiwa ni sehemu ya jitihada za Jeshi la Polisi kudhibiti matukio ya uvunjifu wa amani yanayohusiana na maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Niffer, mkazi wa Masaki Peninsula, Kinondoni, mwenye umri wa miaka 26, anadaiwa kuhusika moja kwa moja katika kuhamasisha vurugu na kuharibu miundombinu ya umma, hususan katika siku za kuelekea uchaguzi.  Akizungumza na wanahabari, Kamanda Jumanne Muliro alisema kuwa uchunguzi unaendelea kwa kina ili kubaini kikamilifu ushiriki wa mtuhumiwa katika vurugu na uharibifu wa miundombinu ya umma. “Jeshi la Polisi linaendelea kuchunguza matukio yote yaliyoripotiwa. Hatua stahiki za kisheria zitachukuliwa kuhakikisha mtu yeyot...