MWARUBAINI DHIDI YA UKATILI MTANDAONI WAPATIKANA.


Na Mwandishi Wetu.

Jeshi la Polisi Tanzania kupitia Kitengo cha Makosa ya Kimtandao kimechukua hatua madhubuti kukabiliana na matukio ya ukatili mtandaoni kwa kutumia vifaa maalum vya kisasa vya uchunguzi, kutoa elimu kwa umma, na kushirikiana na taasisi mbalimbali ndani na nje ya nchi zinazoratibu matumizi salama ya mitandao ya kijamii.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka kitengo hicho, matukio ya ukatili mtandaoni yameendelea kushuhudiwa nchini, yakiwemo vitendo vya udhalilishaji, matusi, vitisho, na uenezaji wa taarifa za uongo. Waathirika wakubwa wa vitendo hivyo ni wanawake, vijana na watu mashuhuri katika jamii.


Aidha, Jeshi la Polisi limeendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu madhara ya ukatili mtandaoni na hatua za kuchukua pindi matukio hayo yanapotokea, likihimiza matumizi chanya ya mitandao kwa kuijenga jamii badala ya kuieneza chuki.


Vilevile, jeshi hilo limeitaka jamii kushirikiana na serikali katika mapambano dhidi ya ukatili huo kwa kuripoti matukio yote ya ukatili mtandaoni na kutumia majukwaa ya kidijitali kwa uadilifu na uwajibikaji.


Jeshi la Polisi limesisitiza kuwa ukatili mtandaoni ni changamoto ya kijamii inayohitaji nguvu ya pamoja kati ya serikali, wananchi na wadau wote wa teknolojia ili kulinda usalama wa watumiaji wa mtandao nchini.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.