Posts

Showing posts from November, 2025

ASKOFU GWAJIMA KURUDI HADHARANI: RAIS SAMIA ASITISHA AGIZO LA KUMKAMATA.

Image
WAZIRI MKUU Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameliagiza Jeshi la Polisi liache kumtafuta Askofu Dkt. Josephat Gwajima kama walivyokuwa wametangaza awali ili aweze kuendelea shughuli zake. Amesema baada ya kutoa msamaha kwa Kanisa la Ufufuo na Uzima, waumini wanahitaji wamuone kiongozi wao, hivyo anatakiwa ajitokeze hadharani aendelee na kazi yake. “Mwacheni ajitokekeze tujenge umoja wa kitaifa, tushikamane kurudisha umoja wa kitaifa. Tumekutana na TEC, viongozi wa dini, wa mila na viongozi mbalimbali; twendeni sote kwenye jambo hili, tujitokeze tuhamasishe Tanzania yenye amani, huu ndio wito wa kiongozi wetu wa nchi” Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Novemba 30, 2025) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Arumeru katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Magufuli Leganga, kata ya Usa River, wilayani Arumeru mkoani Arusha. Waziri Mkuu amewataka Watanzania wakatae kushawishiwa na wanaharakati wanaochochea vurugu kwani zinarudisha nyuma ma...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

PROF. SHEMDOE ATOA SIKU NNE HUDUMA YA MWENDOKASI KUREJEA KATIKA MAENEO YOTE YA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OWM–TAMISEMI), Mhe. Prof. Riziki Shemdoe, ameagiza kurejeshwa kikamilifu kwa huduma ya mabasi ya mwendokasi (DART) katika maeneo yote ya Jiji la Dar es Salaam ndani ya kipindi cha siku nne kuanzia leo. Prof. Shemdoe alitoa maelekezo hayo Novemba 29, 2025 wakati wa uzinduzi wa safari za mabasi ya mwendokasi kutoka Kituo cha Ubungo Maji kwenda Gerezani, safari ambayo imeanza upya baada ya kusimama tangu Oktoba 29, 2025 kufuatia vurugu zilizosababisha uharibifu wa baadhi ya miundombinu ikiwemo vituo vya mabasi katika maeneo kadhaa ya jiji. Akizungumza katika ziara hiyo, Prof. Shemdoe alisema kurejea kwa huduma hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, aliyetoa muda wa siku 10 kuhakikisha usafiri huo muhimu unarejea kwa wananchi. Hata hivyo, Prof. Shemdoe alibainisha kuwa utekelezaji huo umefanyika kwa kasi zaidi kuliko ilivyotarajiwa. “Mhe. Waziri Mkuu alituelekeza ndani...

WAKAZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM WAENDELEA KUMIMINIKA KATIKA KAMBI YA UCHUNGUZI NA MATIBABU BILA MALIPO INAYOTOLEWA NA HOSPITALI YA AMANA NA GSM FOUNDATION.

Image
Mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na maeneo ya jirani wameendelea kujitokeza kwa wingi katika kambi maalum ya uchunguzi na matibabu ya kibingwa na ubingwa bobezi inayoendeshwa bila malipo na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana kwa ushirikiano na GSM Foundation. Hii ni siku ya pili mfululizo tangu kuzinduliwa kwa huduma hizo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja. Wananchi wameonekana kuthamini kwa kiasi kikubwa uwepo wa kambi hiyo, ambayo imekuwa mkombozi kwa watu wa kada mbalimbali, hususan wale wasioweza kumudu gharama za huduma za kibingwa.  Huduma zinazotolewa zimegusa maeneo muhimu ya afya ikiwemo uchunguzi na matibabu ya macho, afya ya kinywa na meno, magonjwa ya akina mama na afya ya uzazi, magonjwa ya ngozi, uchunguzi wa magonjwa yasiyoambukiza kama kisukari na shinikizo la damu, matumizi sahihi ya dawa, huduma kwa watoto, pamoja na magonjwa ya masikio, pua na koo. Aidha, kambi hii imekuwa fursa muhimu kwa wananchi kupata elimu ya afya, ikiwemo namna ya kujikinga dhidi ya ...

MHE. NDEJEMBI AWAHAKIKISHIA WAKAZI WA KIGAMBONI UMEME WA UHAKIKA.

Image
Waziri wa Nishati Mhe. Deogratius Ndejembi amefanya ziara ya kikazi ndani ya Mkoa wa kitanesco wa Kigamboni na kuagiza kuchukuliwa hatua za haraka za kuhakikisha hali ya umeme katika Mkoa wa Kigamboni inaboreshwa na kuwapa wakazi wa eneo hilo huduma ya uhakika alipotembelea Kituo cha Kupokea, Kupoza na Kusambaza umeme cha Dege tarehe 29 Novemba, 2025. “Leo tumekuja kuona ni namna gani Shirika letu la TANESCO linaweza kutatua changamoto hii kwa haraka zaidi na wameweka mipango mizuri ya muda mrefu katika kuhakikisha wanawezesha kupatikana kwa umeme wa uhakika kwa kujenga na kukiongezea nguvu Kituo cha Dege kwa kuweka transfoma ya MVA 120”, ameeleza Mhe. Ndejembi.  Ili kukabiliana na changamoto ya huduma ya umeme iliyopo kwa haraka, Shirika limekuja na suluhisho la haraka kwa kujenga laini itakayosafirisha umeme kutoka Kituo cha Mbagala wa Megawati 22 kuja Kigamboni kuongeza upatikanaji wa umeme kwa Wananchi wa Kigamboni. “Kwa hatua za haraka TANESCO wamenihakikishia kwamba kuna lain...

ONGEZEKO LA JOTO KALI: TMA YATOA TAHADHARI KWA WANANCHI.

Image
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imetoa tahadhari kwa wananchi kuhusu ongezeko la joto katika baadhi ya mikoa nchini, hususan katika maeneo yanayopata misimu miwili ya mvua hali ambayo imesababishwa na mwelekeo wa Jua la Utosi sambamba na upungufu wa mvua katika maeneo husika. Kwa mujibu wa TMA, vipindi vya Jua la Utosi hufikia kilele mwishoni mwa Novemba pale jua linapokaribia Tropiki ya Kaprikoni na hujirudia Februari wakati jua linaelekea Tropiki ya Kansa. Ukaribu wa uso wa Dunia na miale ya jua husababisha ongezeko la joto, jambo linaloathiri hali ya anga na mwonekano wa hewa. Katika mwezi Novemba 2025, ongezeko la joto limeendelea kujitokeza katika baadhi ya mikoa ambapo ripoti za vituo vya hali ya hewa zinaonyesha Moshi (Kilimanjaro) ilifikia 35.7°C mnamo 21 Novemba, ongezeko la 4.2°C ukilinganisha na wastani wa muda mrefu. Ilonga (Morogoro) iliripoti 35.5°C mnamo 20 Novemba, ongezeko la 2.7°C, Morogoro 34.5°C mnamo 26 Novemba (ongezeko la 2.3°C), Ibadakuli (Shinyanga) 33.6...

SERIKALI YAZINDUA MIKAKATI YA KUWAPA FURSA VIJANA KATIKA UWEKEZAJI.

Image
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Prof. Kitila Mkumbo, ametoa mikakati mipya ya kukuza uwekezaji nchini, ikilenga hasa kuwapa fursa vijana na kuongeza ajira. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Maeneo Maalum ya Kiuchumi (TISEZA), Prof. Mkumbo alisema mikakati hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita, chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, za kusogeza uwekezaji karibu na wananchi. “Tunataka uwekezaji unaowasaidia wananchi, hasa kuwapa fursa vijana,” alisema. Serikali itazindua Kituo Maalumu cha Wawekezaji Vijana kinachotoa mafunzo na usaidizi kwa vijana, na pia kuwa na uwakilishi wa kitaifa. Vilevile, itazindua programu ya ardhi na viwanda kwa vijana waliomaliza vyuo, ili waweze kuwekeza katika maeneo maalumu kama Dodoma-Nala, Pwani-Kwala na Mara-Bunda. Huduma za uwekezaji zitasogezwa hadi kila mkoa ifikapo mwaka 2028 kupitia vituo maalumu vya uwekezaji. Aidha, TISEZA itashirikiana na sekta binafsi kujenga majengo ya viwan...

DC Ilala Aipongeza GSM Foundation, Amana kwa Kutoa Huduma za Ubingwa Bobezi Bure

Image
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Edward Mpogolo, ameipongeza Taasisi ya GSM Foundation pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Amana kwa kuendesha kambi ya uchunguzi na matibabu ya ubingwa bobezi bila malipo, sambamba na kugawa bima za afya kwa wananchi 300 wakiwemo wanawake, watoto na wazee wasio na uwezo. Mhe. Mpogolo alitoa pongezi hizo alipotembelea kambi hiyo kwa lengo la kukagua hali ya utoaji wa huduma na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwa wingi kunufaika na huduma ambazo zimesogezwa karibu yao, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuhimiza Bima ya Afya kwa Wote na kusogeza huduma za afya kwa wananchi. Amesema kuwa huduma zinazotolewa na madaktari bingwa katika kambi hiyo ni za ubingwa bobezi ambazo kwa kawaida hupatikana kwa gharama kubwa, hivyo kutoa wito kwa wananchi wa maeneo hayo kujitokeza mapema ili kuchangamkia fursa hiyo muhimu inayogusa rika zote. “Nawapongeza GSM Foundation na Hospitali ya Amana kwa kutuletea h...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

TANZANIA YAVUNA ZAIDI YA TRILIONI 1 KUPITIA MADINI YA UJENZI NA VIWANDANI.

Image
Dar es salaam Imeelezwa kwamba, katika kipindi cha mwaka mmoja wa Fedha 2024/25 Madini Ujenzi na Viwandani yenye thamani ya zaidi ya shilingi Trilioni  Moja yalizalishwa. Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Madini Dkt.Steven Kiruswa wakati wa utoaji Tuzo za Ujenzi na Miundombinu za Afrika Mashiriki zilizotolewa Jijini Dar es Salaam. Dkt. Steven  Kiruswa alisema kuwa, kutokana na kukua na kuendelea kwa sekta ya ujenzi nchini hususan kwenye ujenzi wa miundombinu na ukuaji wa sekta ya viwanda  kimezalishwa kiasi hicho cha fedha kupitia wachimbaji wa madini hayo. Dkt. Kiruswa aliongeza kuwa, kwa kipindi kirefu mchango wa madini ya viwanda na ujenzi yamekuwa na uwanja mpana kwenye kuchangia uchumi wa Taifa ikiwa pamoja na kutoa ajira kwa jamii, kuunganisha mnyororo wa thamani madini  kupitia biashara na wawekezaji wa ndani kuanzia ngazi wilaya mpaka Taifa. Dkt.Kiruswa alifafanua kuwa Tanzania itaendelea kutumia  malighafi zake za  ndani kama vile mchanga, kokoto,...

DKT. KIJAJI AITAKA JAMII KUJIFUNZA HISTORIA YA TAZARA.

Image
Na Fidea Masunga, Dar es Salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji, amesisitiza umuhimu wa jamii kujifunza Historia ya Reli ya Tanzania–Zambia (TAZARA) ili kuimarisha uelewa wa urithi wa taifa na mchango wake katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi. Akizungumza katika hotuba yake  wakati wa uzinduzi wa onesho maalum la Historia ya TAZARA , lililofanyika katika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni jijini Dar es Salaam, Dkt. Kijaji alieleza kuwa onesho hilo litadumu kwa miezi miwili likiwa limelenga kutoa elimu endelevu kwa vizazi vya sasa na vijavyo kuhusu nafasi ya reli hiyo katika kuimarisha ushirikiano wa kikanda na juhudi za ukombozi wa mataifa ya Kusini mwa Afrika. Amebainisha kuwa TAZARA, iliyojengwa mwaka 1970 kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Serikali ya China, ni mfano muhimu wa mafanikio ya miundombinu barani Afrika na ishara ya kudumu ya ushirikiano wa kihistoria kati ya Afrika na China ambapo reli hiyo imekua ikichangia katika usafirishaji wa watu na bidha...

KIKWETE APONGEZA CHUO CHA UTUMISHI WA UMMA KWA KUIMARISHA UTENDAJI NA UFANISI KATIKA SEKTA YA UTUMISHI WA UMMA.

Image
Na Fidea Masunga,Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, amekipongeza Chuo cha Utumishi wa Umma kwa mchango wake mkubwa katika kuboresha utendaji, uwazi na ufanisi wa watumishi wa umma nchini. Kauli hiyo ameitoa jijini Dar es salaam katika makao makuu ya Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania,wakati akizungumza na Menejimenti ya chuo hicho ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kujionea utekelezaji wa majukumu ya chuo. Mhe. Kikwete amesema kuwa chuo kina nafasi muhimu katika kutoa mwongozo wa kistratejia na kitaaluma kwa utumishi wa umma, hususan katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 huku akisisitiza chuo kuendeleza tafiti na mafunzo ya vitendo yanayolenga kuboresha ujuzi, utendaji na uzalishaji wa watumishi wa umma. Pia,Mhe. Kikwete ameahidi kuwa Wizara itaendelea kushirikiana na chuo ili kuhakikisha kinaendelea kutimiza majukumu yake kikamilifu na kuchangia moja kwa moja katika kuboresha...

SERIKALI YATOA KIBALI CHA MUDA WA MWAKA MMOJA KWA WANANCHI KUREKEBISHA TAARIFA ZA USAJILI NIDA.

Image
Na Fidea Masunga,Dar es Salaam. Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetoa muda wa mwaka mmoja kwa wananchi wote waliojisajili katika mfumo wake kufanya marekebisho ya taarifa zao, hatua inayolenga kuhakikisha usahihi na uhalali wa taarifa za utambulisho wa Taifa. Zoezi hilo limeanza rasmi Oktoba 2025 likiwalenga waathirika wa vyeti vya kughushi, waliotumia majina ya wengine kupata vyeti vya elimu, waliotoa taarifa za uongo wakati wa usajili, pamoja na raia waliodanganya kujisajili kama wakimbizi. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, alisema zoezi hilo ni fursa maalum ya kurekebisha taarifa na kuhakikisha kila Mtanzania anapata kitambulisho sahihi.  Aidha Aliwashauri wananchi kujiandaa mapema na kwenda na nyaraka zote muhimu katika ofisi za NIDA za Wilaya, ikiwa ni pamoja na Nakala ya vyeti halisi vya elimu; Cheti cha Kuzaliwa kilichohakikiwa na RITA; Deed pool iliyosajiliwa na gazeti la serikali;...

Waziri Kapinga Aipongeza TIRDO kwa Kuchochea Maendeleo ya Viwanda.

Image
Na Fidea Masunga,Dar es salaam.  Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), amelipongeza Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) kwa mchango wake mkubwa katika kukuza sekta ya viwanda na teknolojia nchini. Akizungumza wakati wa ziara yake ya kikazi katika shirika laTIRDO jijini Dar es salaam, Waziri Kapinga alitembelea maabara mbalimbali na kukutana na vijana wabunifu wanaosaidiwa na shirika hilo, wakiwemo wanaotengeneza magari ya umeme (KAYPEE Motors), wanaochakata plastiki (PREYO), na wabunifu wa vifaa vya kielektroniki (HOP). Waziri Kapinga alisema Serikali itaendelea kuisaidia TIRDO kufanya tafiti bunifu zitakazoongeza ajira kwa vijana na kuchochea ukuaji wa viwanda.  Alibainisha kuwa ushirikiano huo utaiwezesha TIRDO kubuni vyanzo vipya vya mapato, kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi, kuboresha mazingira ya biashara, na kuleta maendeleo endelevu. Aidha, Waziri Kapinga alibainisha kuwa mapato ya makaa ya mawe yaliyotokana na tafit...