SERIKALI YATOA KIBALI CHA MUDA WA MWAKA MMOJA KWA WANANCHI KUREKEBISHA TAARIFA ZA USAJILI NIDA.


Na Fidea Masunga,Dar es Salaam.


Serikali kupitia Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) imetoa muda wa mwaka mmoja kwa wananchi wote waliojisajili katika mfumo wake kufanya marekebisho ya taarifa zao, hatua inayolenga kuhakikisha usahihi na uhalali wa taarifa za utambulisho wa Taifa.


Zoezi hilo limeanza rasmi Oktoba 2025 likiwalenga waathirika wa vyeti vya kughushi, waliotumia majina ya wengine kupata vyeti vya elimu, waliotoa taarifa za uongo wakati wa usajili, pamoja na raia waliodanganya kujisajili kama wakimbizi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa NIDA, James Kaji, alisema zoezi hilo ni fursa maalum ya kurekebisha taarifa na kuhakikisha kila Mtanzania anapata kitambulisho sahihi. 


Aidha Aliwashauri wananchi kujiandaa mapema na kwenda na nyaraka zote muhimu katika ofisi za NIDA za Wilaya, ikiwa ni pamoja na Nakala ya vyeti halisi vya elimu; Cheti cha Kuzaliwa kilichohakikiwa na RITA; Deed pool iliyosajiliwa na gazeti la serikali; na nyaraka nyingine yoyote itakayotakiwa na Ofisi za NIDA.


Kaji aliwasisitiza wananchi kutoa taarifa sahihi na za kweli ili kuepuka marekebisho ya mara kwa mara yasiyo ya lazima, akiongeza kuwa maombi yatakayofanyiwa kazi ni yale yanayokidhi masharti, taratibu na vigezo vilivyowekwa kisheria.


Aidha, NIDA imefafanua kuwa zoezi hilo linahusu mabadiliko halali tu, na si kwa wale wanaojaribu kurekebisha taarifa kwa udanganyifu au kufuata taratibu zisizo halali. 


Hatua hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali kuhakikisha mfumo wa usajili na utambuzi wa watu ni salama, sahihi, wa kuaminika na unaofuata sheria.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.