Serikali Kupitia Wizara ya Mawasiliano Yajipanga Kupanua na kuboresha Mawasiliano Vijijini.
Na Fidea Masunga,Dar es Salaam. Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari imesema imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania, awe mjini au kijijini, anapata huduma bora na za uhakika za simu pamoja na usikivu mzuri wa redio. Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo, Salome Kessy , alisema hayo alipofungua mafunzo ya ndani kwa wataalamu wa Mradi wa Miundombinu ya Mawasiliano Vijijini yanayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Septemba 29 hadi Novemba 7, 2025. Mafunzo hayo yamelenga kuwajengea uwezo wa kiufundi katika usimamizi wa mitandao ya simu vijijini, uendeshaji wa miundombinu ya mawasiliano, pamoja na utatuzi wa changamoto zinazohusu huduma za simu na intaneti. Kwa mujibu wa Kessy, kufikia Juni 2025 Tanzania ilikuwa na zaidi ya laini za simu milioni 92 , sawa na upenyo wa asilimia 136. Aidha, kulikuwa na watumiaji wa intaneti milioni 54 , sawa na upenyo wa asilimia 79. Alisema huduma za intaneti ya kasi zimewafikia wananchi ...