MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA MANISPAA YA SUMBAWANGA, MIRADI YENYE THAMANI YA ZAIDI YA SH. BILIONI 335 YAZINDULIWA.


Mwenge wa Uhuru umepokelewa rasmi katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ukitokea Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ambapo unakimbizwa umbali wa kilomita 88.7.


Katika mbio hizo, Mwenge wa Uhuru umeweka mawe ya msingi na kuzindua miradi mbalimbali yenye thamani ya shilingi Bilioni 30.3, Miongoni mwa miradi hiyo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa Soko la Mazao Kanondo, ujenzi wa barabara kiwango cha lami kupitia mradi wa TACTIC, huduma za afya katika Hospitali ya Manispaa ya Sumbawanga, shule mpya ya msingi Pwela iliyojengwa kwa mapato ya ndani, pamoja na ofisi ya Wakala wa Misitu Tanzania. 



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Ismail Ali Usi, ameipongeza Manispaa ya Sumbawanga kwa utekelezaji wa miradi hiyo kwa viwango vya ubora vinavyowaletea wananchi maendeleo endelevu.

Kaulimbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 ni "Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu."



Manispaa ya Sumbawanga imesisitiza kuwa imeupokea Mwenge wa Uhuru kwa heshima kubwa na imetamba nao kama alama ya mshikamano na maendeleo ya wananchi wake huku wananchi wamehamasishwa kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.