Posts

Showing posts from March, 2025

Walimu watakiwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu.

Image
MKUU wa Shule ya Sekondari Juhudi Happynes Pallangyo, amewataka Walimu kutenga muda kwa ajili kusaidia watoto wa makundi maalum na yatima kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Mwalimu Pallangyo alisema hayo wakati wa futari maalum aliyoandaa kwa ajili ya Walimu  wake ambapo walifuturu pamoja shuleni hapo kama sehemu ya utaratibu wake endelevu kila mwaka anakula futari na walimu wake. "Nawaomba walimu wangu tujenge tabia ya kusaidia watoto wa makundi maalum na watoto yatima kwa ajili ya kuwasaidia na wao waweze kujiona sawa kama jamii nyingine wenye Wazazi waweze kufurahi"alisema Pallangyo.   Alisema kila mwaka analisha futari walimu wake ni sehemu ya mikakati ya kazi kujenga mahusiano pamoja na kushirikiana katika kuongeza ufaulu shuleni ambapo walimu wana kutana pamoja kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamano.  Alisema kila mwaka katika shule ya sekondari Juhudi ufaulu unaongezeka miaka mitatu mfululizo wanafunzi wanafaulu kwa asilimia 100. Kat...

USHIRIKIANO WA TANZANIA NA KOREA KULETA MAGEUZI SEKTA YA MADINI NCHINI

Image
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa mahitaji na matumizi ya Madini Muhimu duniani, Tanzania ina dhamira ya dhati ya kuendeleza Sekta ya Madini ikiwa ni pamoja na Madini Mkakati hapa nchini kwa kuimarisha ushirikiano na Nchi ya Korea ya Kusini kwa lengo la kuleta mageuzi yenye kuleta tija zaidi kupitia sekta hiyo. Ameyasema hayo leo Machi 25, 2025 jijini Seoul, Korea Kusini wakati akizungumza katika Mkutano wa Madini Muhimu kati ya Tanzania na Korea yaliyoandaliwa jijini humo.  Dkt. Kiruswa amesema kuwa, kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la Kimataifa la Nishati (IEA) ya mwaka 2023, matumizi ya lithiamu yameongezeka kwa asilimia 30, huku mahitaji ya nikeli, kobalti, kinyewe (graphite), na madini adimu yakiongezeka kati ya asilimia 8 hadi 15  na kwamba hali hiyo inatoa fursa kubwa kwa Tanzania kushirikiana na mataifa yenye teknolojia za kisasa kama Korea katika uchimbaji, uongezaji thamani, na biashara ya madini haya. Aidha, Dkt. Kirus...

RC CHALAMILA AMTAKA MKANDARASI BARABARA YA KITUNDA, KIVULE, MSONGOLA KUANZA KAZI MARA MOJA

Image
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 24, 2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kitunda, Kivule Msongola na Majohe njia 4 ambayo toka mkataba wa ujenzi usainiwe mwaka jana mpaka sasa Mkandarasi amejenga Camp tu na vifaa vya ujenzi havionekani licha ya kuwa alishalipwa sehemu ya fedha za kuanza ujenzi huo. RC Chalamila amemtaka Mkandarasi kuanza ujenzi huo mara moja, atakapokuja tena aone mabadiliko makubwa la sivyo hatakuwa na uvumilivu tena vilevile amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya llala kumuandalia Mkutano wa hadhara ili aweze kuongea na wananchi wamueleze kero zao.  "Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo barabara ili kuwa na jamii venye ustawi hivyo wakazi wa eneo hilo wakae mkao wa kula" Alisema Chalamila. Vilevile RC Chalamila amesisitiza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni wa kipekee kila kitu kihitaji pesa na ili upate pesa lazima uhangaik...

MEYA KUMBILAMOTO KUTATUA KERO YA MAJI VINGUNGUTI.

Image
MEYA wa Halmashauri ya jiji La Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti amesema anatatua kero za maji kata ya Vingunguti kwa kufunga matanki makubwa ili kumtua ndoo kichwani mama. Meya Kumbilamoto amesema hayo katika kikao cha kuelezea mikakati ya maendeleo na kutatua kero huku akiweka kipaumbele chake cha kusambaza maji ili aweze kumtua ndoo kichwani mama.  "Hichi kikao changu cha viongozi wa chama pamoja na wajumbe wa mashina dhumuni la kikao hichi kuondoa changamoto za maji kwa jamii ili nimtue ndoo kichwani mama katika kuakikisha maji yanapatikana kwa urais upo mpango wa muda mfupi ambapo kwa kushirikiana na DAWASA wataleta matanki makubwa ya maji safi ambayo yatasambazwa kila mtaa"alisema Kumbilamoto   Meya Kumbilamoto alisema wakati mpango huo unaandaliwa wa kuleta matanki unasubiriwa mpango mkubwa wa kufufua visima  pamoja na ule wa kuunganishwa kwenye mfumo mkubwa wa maji ya Ruvu. Aidha alisema kwa muda mrefu Vingunguti wamekuwa wakin...

Utabiri wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo.

Image
 

KAMATI ZA MAAFA HALMASHAURI YA KIGOMA UJIJI ZAPATIWA MAFUNZO YA KUKABILIANA NA MAAFA

Image
Maafisa wa Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu (Idara ya Menejimenti ya Maafa) kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa linaloshughulikia uhamaji (IOM) wameendesha semina ya kujenga uelewa juu ya upunguzaji wa madhara ya maafa katika jamii. Mafunzo hayo yamefanyika tarehe 25 Machi 2025 katika Manispaa ya Kigoma Ujiji ambapo yamehudhuriwa na washiriki 50 ikiwemo Watendaji wa Kata, Watendaji wa Vijiji, Watendaji wa Mtaa Kamati za Maafa za Kata na Vijiji pamoja na mtaa. Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kigoma Ujiji Bi.Petronila Gwakila ambaye ni Afisa Mazingira ndani ya Manispaa hiyo amesema, mafunzo hayo yameletwa wakati sahihi ambapo manispaa inatarajiwa kupata mvua ambazo mara nyingi mvua hizo husababisha maafa mbalimbali na kufanya wananchi kutofanya shughuli zao za kila siku za kuwapatia kipato hivyo mafunzo haya yataweza kuleta muamko katika kukabili maafa pindi yatakapotokea. "Kwa hiyo ndugu zangu tumepata wakufunzi h...

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YAPONGEZA UJENZI WA JENGO LA WIZARA YA NISHATI - MTUMBA.

Image
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekagua ujenzi wa jengo la Wizara ya Nishati katika mji wa Serikali Mtumba na kuipongeza Wizara kwa hatua ya ujenzi iliyofikiwa kwa asilimia 94. Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. David Mathayo amesema hayo tarehe 20 Machi 2025, wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa jengo hilo katika Mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma iliyohusisha Menejimenti ya Wizara na baadhi ya watumishi.  “Tumepita kila mahali katika jengo hilo kazi nzuri na kubwa imefanyika na mandhari ya ndani na ya nje zote zinavutia sana, nawapongeza sana Wizara ya Nishati kwa kazi hii, zaidi kamati inampongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana za kutekeleza ujenzi wa majengo mengi na mazuri ya serikali.” Amesema Mathayo Amepongeza Viongozi Wakuu na Menejimenti ya Wizara ya Nishati kwa kusimamia vyema ujenzi huo na kuhakikisha fedha za mkandarasi zinalipwa kwa wakati wakati wote. Aidha,amewasisitiza kukamilisha kazi ndogo zilizosalia ili watu...

MAJALIWA:HAKIKISHENI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI ZINAKIDHI VIWANGO.

Image
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za kudhibiti viwango nchini zihakikishe uzalishaji wa bidhaa zote zinazozalishwa zikiwemo za afya zinakidhi ubora unaotakiwa na kuweza kushindana katika masoko ya kimataifa. Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 20, 2025) baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mitambo ya kuzalisha oksijeni kwa matumizi ya hospitali, ambapo amesisitiza kuwa soko linatakiwa liwe na bidhaa salama, bora, na zinazokubalika kimataifa.  Mitambo hiyo inajengwa katika ofisi za TOL Gases, Temeke Dar es Salaam. Amesema mradi huo utakapokamilika utazalisha lita milioni 4.1 za oksijeni ya matibabu kwa mwaka kuanzia mwaka 2026.  "Hatua hii itaboresha upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na vituo vya afya, pamoja na kupunguza gharama za oksijeni ya matibabu kwa asilimia 35 katika hospitali na vituo vya afya kote chini, hivyo kuimarisha huduma za afya kwa wananchi". Aidha, Waziri Mkuu amesema mradi huu unaunga mkono juhudi endelevu za Serikali za kuhak...

Mfanyakazi wa ndani ashikiliwa na Polisi akijaribu kumtorosha mtoto mchanga mwenye umri wa miezi mitatu

Image
  Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia Binti mmoja aitwaye Christina Nashoni mwenye umri wa miaka 15 Mfanyakazi wa ndani Mkoani Tabora ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Malagarasi Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma kwa tuhuma ya kujaribu kutorosha Mtoto mchanga wa kike mwenye umri wa miezi mitatu kutoka kwa Mwajiri wake (Boss wake) aitwaye Beatrice Kiboma Mkazi wa  Cheyo B Manispaa ya Tabora. Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea jana March 19, 2025 ambapo Binti huyo alitoka nje na Mtoto kwa ajili ya kuanika nguo lakini hakufanya hivyo na badala yake alitoka nje ya geti ya nyumba hiyo na kujaribu kutoroka huku taarifa ya awali ya Jeshi la Polisi ikisema kuwa Binti huyo alitorosha Mtoto ili arudi nae kwao kwani wakati anaondoka kwao Kasulu alidanganya kuwa ni Mjamzito. RPC amesema "March 19,2025 majira ya saa tisa na robo katika maeneo ya kituo cha mafuta, Kata ya Kanyeye Mtuhumiwa Christina Nashoni alikamatwa na Wananchi wakishiri...

ANGALIZO LA HALI MBAYA YA HEWA KWA SIKU TANO KUANZIA LEO MARCH 20 HADI MARCH 24 2025.

Image
 

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO.

Image
 

DC ILALA EDWARD MPOGOLO AJITOJEZA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA.

Image
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo leo, ameshiriki zoezi la kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la mpiga kura Kata ya Ilala mtaa wa Karume.  Mkuu wa  Wilaya Edward Mpogolo alifika Mtaa wa Karume saa tatu asubuhi ambapo alipanga foleni kama mwananchi wa kawaida na kisha kujiandikisha katika daftari   hilo. "Wananchi wangu wa Wilaya ya Ilala nawaomba tuweze kujitokeza katika mitaa yetu na kata zetu kwa ajili ya kwenda kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura mkoa Dar es Salaam tumepewa wiki moja tuwe wote tumejiandikisha tuje kumpigia kura Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan  pamoja na Wabunge wake na madiwani katika uchaguzi mkuu mwaka huu 2025^alisema Mpogolo  Mkuu wa Wilaya alisema ili uweze kupata haki yako ya kupiga kura kila mmoja wetu awe amejiandisha  kwa kufuata taratibu  eneo analoishi awe ameenda kujiandikisha   Aliwataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa pamoja na Wajumbe wa Serikali za Mitaa kus...

Amana Hospitali Yaadhimisha Siku ya Kinywa na Meno kwa Kutoa Huduma Bure.

Image
Hospitali ya Amana leo imeungana na dunia nzima kuadhimisha  Siku ya Kinywa na Meno Duniani  yenye kaulimbiu  “Kinywa Chenye Furaha, Fikra Tulivu”  kwa kutoa huduma za bure za uchunguzi na matibabu ya meno kwa wananchi. Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Amana, Dkt. Elisia Mpango amesema kuwa lengo la maadhimisho hayo ni kuhamasisha wananchi kutunza afya ya kinywa na kuelewa umuhimu wake katika maisha ya kila siku. “Afya ya kinywa ni msingi wa afya bora kwa ujumla. Watu wengi hupuuza matatizo ya meno bila kujua kuwa yanaweza kusababisha maumivu makali, matatizo ya lishe, na hata kuathiri afya ya akili. Kupitia huduma hizi za bure, tunataka kuwaelimisha wananchi na kuwapa fursa ya kupata matibabu mapema,”  amesema Dkt. Mpango Kwa upande wake Daktari bingwa wa kinywa na meno wa Amana Hospitali Dkt. Amimu Kilomoni amesema matatizo ya kinywa kama vile kuoza kwa meno na magonjwa ya fizi yanaweza kuzuilika kwa kufuata kanuni bora z...

DKT. BITEKO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI KUPUNGUZA UPOTEVU WA MAJI.

Image
  Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua taarifa ya Utendaji wa Mamlaka za maji kwa mwaka 2023/24 na kusema upatikanaji wa huduma za maji ni haki ya msingi hivyo ni muhimu kulinda vyanzo vya maji kuwezesha upatikanaji wake. Dkt. Biteko amesema hayo jijini Dar es Salaam Machi 19, 2025 ambapo amesema pamoja na jitihada zinazoendelea jamii ina wajibu wa kuhakikisha usafi wa mazingira, kupanda miti na kuhifadi misitu ili kuendelea kupata na kutumia rasilimali maji. “Tusipotunza vyanzo vya maji na kuhifadhi mazingira tutajikuta katika mtanziko mkubwa (water Stress),” amesema na kuongeza kukosekana kwa rasilimali maji kwa baadhi ya watu kinaweza kuwa chanzo cha migogoro na machafuko katika jamii husika. Ili kukabilikana na hali hiyo na kumwezesha kila Mtanzania kupata huduma za maji na usafi wa mazingira, Dkt. Biteko amezielekeza mamlaka za maji kupunguza kiwango cha upotevu maji ili kuepusha hasara ya shilingi bilioni 114.12 iliyotokana na upotevu huo kw...

PAC YAPONGEZA UJENZI NYUMBA 109 KWA WAATHIRIKA WA MAPOROMOKO YA TOPE HANANG.

Image
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imepongeza Serikali kwa ujenzi wa nyumba 109 kwa waathirika wa maporomoko ya tope yaliyotokea Desemba 2023 mkoani Manyara. Kamati imetoa  pongezi hizo tarehe 17 Machi, 2025 wakati wa ziara yao katika kitongoji cha Waret kilichopo wilayani Hanang Mkoani Manyara  kwa ajili ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, ikiwemo ujenzi wa nyumba 109 kwa waathirika pamoja na ujenzi wa shule mpya ya msingi iliyojengwa katika kitongoji hicho. Akizungumza mara Baada ya ukaguzi wa eneo hilo , Mwenyekiti wa kamati hiyo na Mbunge wa Vwawa, Mhe. Japhet Hasunga, amesema wameridhishwa na utekelezaji wa miradi iliyopo pamoja na thamani ya fedha iliyotumika unaakisi ubora wa kazi. "Kwanza tunampongeza Daktari Samia Suluhu Hassan ambaye aliona hili pamoja na viongozi wengine wote waliosimamia mradi huu, tumeona fedha za umma zikitumika kwa ufanisi, na hii ni ishara nzuri ya usimamizi mzuri wa miradi ya kimaendeleo hivyo tuhakikishe tunailin...

BILIONI 60 KULIPA FIDIA WANANCHI WALIOPITIWA MRADI WA RUHUDJI NA RUMAKALl.

Image
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeishauri Serikali kutafuta fedha za kuwalipa fidia wananchi waliopitiwa na Miradi ya kufua Umeme ya Ruhudji na Rumakali, ili wananchi hao wapishe maeneo hayo na waweze kuendelea na shughuli zao za kila siku wakati miradi hiyo ikisubiri kutekelezwa. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye ni Mbunge wa Same Mhe. David Mathayo baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa miradi ya umeme katika Mkoa wa Njombe, tarehe 16 Machi 2025. Mhe. Mathayo amesema, Serikali itafute fedha za kuwalipa fidia wananchi walioathiriwa na miradi hiyo ili wananchi hao wapishe na meneo hayo na waendelee na shughuli zao zingine wakati serikali ikiendelea kutafuta fedha za kutekeleza miradi hiyo. “ Tayari tathmini imeshafanyika kwa wananchi watakaopitiwa na mradi huo na gharama za kuwalipa zimefahamika,na wananchi wanayo hiyo taarifa, ni vyema sasa serikali ikatafuta fedha za kuwalipa fidia wananchi hao ili wakaendelee na Maisha yao mengine wakati j...