DC ILALA EDWARD MPOGOLO AJITOJEZA KUJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA MPIGA KURA.
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo leo, ameshiriki zoezi la kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la mpiga kura Kata ya Ilala mtaa wa Karume.
Mkuu wa Wilaya Edward Mpogolo alifika Mtaa wa Karume saa tatu asubuhi ambapo alipanga foleni kama mwananchi wa kawaida na kisha kujiandikisha katika daftari hilo.
"Wananchi wangu wa Wilaya ya Ilala nawaomba tuweze kujitokeza katika mitaa yetu na kata zetu kwa ajili ya kwenda kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura mkoa Dar es Salaam tumepewa wiki moja tuwe wote tumejiandikisha tuje kumpigia kura Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan pamoja na Wabunge wake na madiwani katika uchaguzi mkuu mwaka huu 2025^alisema Mpogolo
Mkuu wa Wilaya alisema ili uweze kupata haki yako ya kupiga kura kila mmoja wetu awe amejiandisha kwa kufuata taratibu eneo analoishi awe ameenda kujiandikisha
Aliwataka Wenyeviti wa Serikali za mitaa pamoja na Wajumbe wa Serikali za Mitaa kushirikiana kwa pamoja kwenda kuhamasishana wananchi waende kujiandikisha katika vituo vyao.
Daftari la maboresho ya mpiga kura mkoa Dar es Salaam limezinduliwa Machi 17 mwaka huu ambapo zoezi hilo linatarajia kumalizika Machi 23 /2025 .
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu inatarajia kufanya uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani ambapo uchaguzi huo unafanyika kila baada miaka mitano ambapo kabla uchaguzi kufika wanachi wake lazima wawe wamejindikisha katika Daftari la mpiga kura.
MWENYEKITI wa Serikali ya Mtaa Karume Hajji Bechina alisema katika eneo la mtaa wake zoezi linaenda vizuri siku ya ufunguzi mpaka leo watu wanajitikoza kujiandikisha.
na yeye na Wajumbe wake wamejipa vizuri kutekeleza maagizo ya Serikali kwa ajili ya Kuhamashisha wananchi na kutoa elimu.



Comments
Post a Comment