RC CHALAMILA AMTAKA MKANDARASI BARABARA YA KITUNDA, KIVULE, MSONGOLA KUANZA KAZI MARA MOJA

 


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Machi 24, 2025 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Kitunda, Kivule Msongola na Majohe njia 4 ambayo toka mkataba wa ujenzi usainiwe mwaka jana mpaka sasa Mkandarasi amejenga Camp tu na vifaa vya ujenzi havionekani licha ya kuwa alishalipwa sehemu ya fedha za kuanza ujenzi huo.


RC Chalamila amemtaka Mkandarasi kuanza ujenzi huo mara moja, atakapokuja tena aone mabadiliko makubwa la sivyo hatakuwa na uvumilivu tena vilevile amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya llala kumuandalia Mkutano wa hadhara ili aweze kuongea na wananchi wamueleze kero zao. 



"Serikali ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri katika kuboresha huduma mbalimbali za jamii ikiwemo barabara ili kuwa na jamii venye ustawi hivyo wakazi wa eneo hilo wakae mkao wa kula" Alisema Chalamila.



Vilevile RC Chalamila amesisitiza Mkoa wa Dar es Salaam kuwa ni wa kipekee kila kitu kihitaji pesa na ili upate pesa lazima uhangaike muda wote na kuhangaika kunahitaji amani hivyo kila mmoja ana kila sababu ya kuilinda amani kwa nguvu zote.



Naye Meneja TARURA Mkoa Mhandisi Jofrey Mkinga amesema kwa mujlbu wa mkataba Mkandarasi huyo mpaka sasa yuko nje ya muda kwa miezi miwili kitu ambacho amekifanya eneo la mradi hadi sasa ni kujenga Camp tu hivyo utekelezaji wa mradi uko chini



Kwa upande wa Mkuu wa Wilaya ya llala Mhe Edward Mpogolo amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa hufanya ziara katika Wilaya hiyo ambapo amesema changamoto za wakazi wa eneo hilo ilikuwa ni barabara pamoja Vituo vya Afya hivyo anamuomba Mkuu wa Mkoa kumpelekea salaam za wana llala Mhe Rais kwa kutoa pesa za ujenzi wa barabara na kituo cha afya ambacho ujenzi wake unaendelea.



Mwisho mwenyekiti wa Mtaa wa Mbondole Bwana Thomas Nyanduli amesema anajisikia furaha kuona mkuu wa Mkoa amekuja kukagua mradi huo hivyo ameshukuru na kupongeza kwa dhati.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.