MEYA KUMBILAMOTO KUTATUA KERO YA MAJI VINGUNGUTI.
MEYA wa Halmashauri ya jiji La Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti amesema anatatua kero za maji kata ya Vingunguti kwa kufunga matanki makubwa ili kumtua ndoo kichwani mama.
Meya Kumbilamoto amesema hayo katika kikao cha kuelezea mikakati ya maendeleo na kutatua kero huku akiweka kipaumbele chake cha kusambaza maji ili aweze kumtua ndoo kichwani mama.
"Hichi kikao changu cha viongozi wa chama pamoja na wajumbe wa mashina dhumuni la kikao hichi kuondoa changamoto za maji kwa jamii ili nimtue ndoo kichwani mama katika kuakikisha maji yanapatikana kwa urais upo mpango wa muda mfupi ambapo kwa kushirikiana na DAWASA wataleta matanki makubwa ya maji safi ambayo yatasambazwa kila mtaa"alisema Kumbilamoto
Meya Kumbilamoto alisema wakati mpango huo unaandaliwa wa kuleta matanki unasubiriwa mpango mkubwa wa kufufua visima pamoja na ule wa kuunganishwa kwenye mfumo mkubwa wa maji ya Ruvu.
Aidha alisema kwa muda mrefu Vingunguti wamekuwa wakinunua ndoo moja ya maji safi na salama kwa shilingi 1000 kupitia mpango huo watanunua ndoo moja kwa shilingi 100 .
Aliwaomba wawakilishi wa wananchi waliohudhuria mkutano huo waende wakashirikiane na DAWASA ili waweze kufanikiwa mradi huo kupata maji safi na salama kwa urais.
Kwa upande wake Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata mhandisi Gilbert Masawe, alisema hatua hiyo ni ya dharura lakini kuna mpango mkubwa ambao upo kwenye hatua ya awali ya utekelezaji ikiwemo kufufua visima vyote vilivyotelekezwa, pia kuangalia namna ya kusambaza maji kupitia mradi mkubwa wa Ruvu ambao kwa kiasi kikubwa unatumiwa na wakazi wa mkoa wa Dar es salaam.
"Wananchi hawa wanauziwa maji kwa gharama kubwa lakini tunavyo visima vyetu humu, tutavifanyia tathimini ili tujue vinahitaji nini ili tuviboreshe viweze kufanya kazi, lakini lazima tujihakikishie usalama wa maji na kiasi gani kipo " alisema Masawe.



Comments
Post a Comment