Mfanyakazi wa ndani ashikiliwa na Polisi akijaribu kumtorosha mtoto mchanga mwenye umri wa miezi mitatu

 


Jeshi la Polisi Mkoani Tabora linamshikilia Binti mmoja aitwaye Christina Nashoni mwenye umri wa miaka 15 Mfanyakazi wa ndani Mkoani Tabora ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Malagarasi Wilaya ya Kasulu Mkoani Kigoma kwa tuhuma ya kujaribu kutorosha Mtoto mchanga wa kike mwenye umri wa miezi mitatu kutoka kwa Mwajiri wake (Boss wake) aitwaye Beatrice Kiboma Mkazi wa Cheyo B Manispaa ya Tabora.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Tabora Richard Abwao amesema tukio hilo limetokea jana March 19, 2025 ambapo Binti huyo alitoka nje na Mtoto kwa ajili ya kuanika nguo lakini hakufanya hivyo na badala yake alitoka nje ya geti ya nyumba hiyo na kujaribu kutoroka huku taarifa ya awali ya Jeshi la Polisi ikisema kuwa Binti huyo alitorosha Mtoto ili arudi nae kwao kwani wakati anaondoka kwao Kasulu alidanganya kuwa ni Mjamzito.


RPC amesema "March 19,2025 majira ya saa tisa na robo katika maeneo ya kituo cha mafuta, Kata ya Kanyeye Mtuhumiwa Christina Nashoni alikamatwa na Wananchi wakishirikiana na Polisi akiwa anatoroka na Mtoto aitwaye Daniele Dotto mwenye umri wa miezi mitatu na wiki moja Mtoto ambaye alimchukua kwa Boss wake katika nyumba anayofanya kazi za ndani"


"Juzi March 18,2025 majira ya saa saba mchana ndio siku ambayo Mtuhumiwa alifika hapa Kigoma akiwa na Rafiki yake kwa ajili ya kufanya kazi ya ndani huku kwa maelezo yake akisema alidanganya kwao kuwa ni Mjamzito hali iliyopelekea Wazazi wake kuchukizwa na kuondoka nyumbani kwao kuja kufanya kazi za ndani na sababu hiyo aliitoa ili asikatazwe kuondoka kwao lakini baada ya kufika katika eneo la kazi amefanya kazi siku moja tu akaona kazi ni nyingi hivyo akaamua kuondoka na kutoroka na Mtoto huyo, tukafanikiwa kumkamata kabla ya kutoroka nje ya Tabora”


“Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa jambo hili na kujua kwa kina sababu za kutorosha Mtoto huyo kama kuna sababu nyingine tutaibaini"

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.