MAJALIWA:HAKIKISHENI BIDHAA ZINAZOZALISHWA NCHINI ZINAKIDHI VIWANGO.



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameziagiza taasisi za

kudhibiti viwango nchini zihakikishe uzalishaji wa bidhaa

zote zinazozalishwa zikiwemo za afya zinakidhi ubora

unaotakiwa na kuweza kushindana katika masoko ya kimataifa.


Ametoa agizo hilo leo (Alhamisi, Machi 20, 2025) baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa mitambo ya kuzalisha oksijeni kwa matumizi ya hospitali, ambapo amesisitiza kuwa soko linatakiwa liwe na bidhaa salama, bora, na zinazokubalika kimataifa. 


Mitambo hiyo inajengwa katika

ofisi za TOL Gases, Temeke Dar es Salaam.

Amesema mradi huo utakapokamilika utazalisha lita milioni 4.1 za oksijeni ya matibabu kwa mwaka kuanzia mwaka

2026. 


"Hatua hii itaboresha upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na vituo vya afya, pamoja na kupunguza gharama za oksijeni ya matibabu kwa asilimia 35 katika hospitali na vituo vya afya kote chini, hivyo kuimarisha huduma za afya

kwa wananchi".



Aidha, Waziri Mkuu amesema mradi huu unaunga mkono juhudi endelevu za Serikali za kuhakikisha oksijeni kwa ajili

ya matibabu inapatikana kwa urahisi katika kila kituo cha huduma za afya nchini.


"Mradi huu utaongeza upatikanaji wa oksijeni katika hospitali na zahanati nchini na kupunguza vifo vitokanavyo na

magoniwa ya kupumua ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo

vya akina mama na kuokoa ya watoto wa Taifa hili."


Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godfrey Mollel amesema mradi huo ni muhimu kwa sababu oksijeni inayozalishwa kwa njia hiyo inakuwa na viwango vya ubora,

hivyo itasaidia kuimarisha huduma za afya zitolewazo nchini

pamoja na kupunguza vifo.


Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TOL Gases, Daniel Warungu ametumia fursa hiyo kuipongeza Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu

Hassan kwa kujidhatiti katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa Watanzania.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.