Walimu watakiwa kuwasaidia watoto wenye ulemavu.


MKUU wa Shule ya Sekondari Juhudi Happynes Pallangyo, amewataka Walimu kutenga muda kwa ajili kusaidia watoto wa makundi maalum na yatima kwa ajili ya kutatua changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo.


Mwalimu Pallangyo alisema hayo wakati wa futari maalum aliyoandaa kwa ajili ya Walimu  wake ambapo walifuturu pamoja shuleni hapo kama sehemu ya utaratibu wake endelevu kila mwaka anakula futari na walimu wake.


"Nawaomba walimu wangu tujenge tabia ya kusaidia watoto wa makundi maalum na watoto yatima kwa ajili ya kuwasaidia na wao waweze kujiona sawa kama jamii nyingine wenye Wazazi waweze kufurahi"alisema Pallangyo.  


Alisema kila mwaka analisha futari walimu wake ni sehemu ya mikakati ya kazi kujenga mahusiano pamoja na kushirikiana katika kuongeza ufaulu shuleni ambapo walimu wana kutana pamoja kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamano. 


Alisema kila mwaka katika shule ya sekondari Juhudi ufaulu unaongezeka miaka mitatu mfululizo wanafunzi wanafaulu kwa asilimia 100.


Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Ukonga Hayubu  Msalika ,alisema kwa niaba ya Mbunge jery silaa, ambapo alisema Mbunge Jery Silaa anatarajia kufunga mfumo wa TEHAMA kwa shule kumi za Jimbo la Ukonga ambapo kila shule zitafungwa kompyuta 20 za Walimu na Wanafunzi.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.