CWT MANYARA YATOA WITO KWA WALIMU KUJITOKEZA KUPIGA KURA KESHO
Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Mkoa wa Manyara kimetoa wito kwa walimu wote mkoani humo kujitokeza kwa wingi kushiriki katika zoezi la kikatiba la kupiga kura litakalofanyika kesho, Oktoba 29, 2025, kwa ajili ya kuwachagua viongozi wanaowataka.
Mwenyekiti wa CWT Mkoa wa Manyara, Mwalimu Theofil Joseph Amo, ametoa wito huo leo, akisisitiza umuhimu wa walimu kutumia haki yao ya kidemokrasia kwa amani na utulivu.
Amo amewataka walimu kupuuza waraka unaosambaa mitandaoni unaodaiwa kutoka kwa chama hicho, akibainisha kuwa ni taarifa potofu na si kauli rasmi ya uongozi wa CWT.
Ameongeza kuwa chama hicho kinaamini katika misingi ya uwazi, umoja na ushiriki wa kila mwanachama katika maamuzi muhimu, ikiwemo uchaguzi wa viongozi wao.

Comments
Post a Comment