SERIKALI YAAHIDI KUSHIRIKIANA NA TNCC KUTENGENEZA MAZINGIRA RAFIKI KWA WAEKEZEZAJI NA SEKTA BINAFSI.


Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara yaahidi kushirikiana na Chemba ya Taifa ya Biashara Tanzania (TNCC) kutoa mazingira rafiki kwa wawekezaji na sekta binafsi, hatua inayolenga kufanikisha dira ya taifa ya mwaka 2050 ya kuwa na uchumi imara, shindani na jumuishi.


Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb),wakati wa ziara yake katika Ofisi za TNCC Desemba 22, 2025, jijini Dar es Salaam, huku akisisitiza kuwa Serikali inalenga kuachana na uchumi unaotegemea rasilimali asilia na kuelekea kwenye uchumi unaojengwa juu ya uzalishaji, kuongeza thamani ya bidhaa za ndani, na kushindana kimataifa.


Aidha, Mhe. Kapinga aliongeza kuwa ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na sekta binafsi, kupitia TNCC, ni muhimu katika kuimarisha uzalishaji wa ndani, kuvutia uwekezaji, na kuhakikisha sekta binafsi inapata mazingira yanayochochea ushindani na ukuaji endelevu.


Kwa upande wake, Rais wa TNCC, Bw. Vicent Minja, alisema chemba hiyo imeendelea kuwa nguzo muhimu kwa wafanyabiashara nchini, ikihamasisha ushirikiano na Serikali katika kutatua changamoto za biashara, kuchochea ukuaji wa viwanda, na kushiriki katika ajenda ya kitaifa ya ajira endelevu.


Aidha, baadhi ya wawakilishi wa TNCC kutoka mikoa mbalimbali wameishukuru Serikali kwa kuendeleza mazingira wezeshi ya biashara na kuhimiza wafanyabiashara kujiunga na Chemba ili kushirikiana katika kufanikisha dira ya taifa ya mwaka 2050.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.