KIVUKO CHA MV KILINDONI CHASITISHA HUDUMA MAFIA.

 Kivuko MV. KILINDONI kinachotoa huduma kati ya Mafia Wilayani Mafia na Nyamisati Wilayani Kibiti Mkoani Pwani kitasimama kutoa huduma katika eneo hilo kuanzia siku ya leo Tarehe 12 Februari, 2025 ili kupisha matengenezo pamoja na kufungwa injini mpya.


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha masoko na uhusiano TEMESA kivuko MV. KILINDONI kimewasili leo kikiwa na abiria pamoja na mizigo eneo la Nyamisati kikitokea Wilayani Mafia. 


Kivuko hicho kinatarajiwa kupekekwa Mkoani Dar es Salaam ambako kitakuwa huko kwa muda wa wiki moja kikifanyiwa matengenezo hayo ili kukiongezea ufanisi kiweze kurejea kikiwa bora na salama kwa watumiaji. 


Wakala wa Ufundi na Umeme Tanzania (TEMESA), unawaomba radhi abiria wote kutokana na usumbufu watakaoupata kutokana na kukosekana kwa huduma ya kivuko hicho.







Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.