DKT. MWIGULU AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS WA IFAD
Waziri Mkuu wa Tanzania *Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba*, amekutana na Rais wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo ya Kilimo (IFAD), *Ndg. Alvaro Lario* na kufanya mazungumzo juu ya ushirikiano katika sekta ya kilimo na uwezeshaji wa wananchi kiuchumi.
Katika kikao hicho kilichofanyika jijini Nairobi leo *Jumatatu Mei 11, 2026*, *Dkt. Mwigulu* amesema kuwa Tanzania itaendelea kushirikiana na *IFAD* katika maeneo mbalimbali ikiwemo kilimo himilivu cha tabianchi, maendeleo ya kilimo biashara, mapinduzi ya kidijitali katika sekta ya kilimo, kuongeza uzalishaji wa alizeti ili kusaidia upatikanaji wa mafuta ya kula nchini pamoja na uwezeshaji wa vijana na wanawake kiuchumi.
Aidha *Mhe. Waziri Mkuu* amesema kuwa Tanzania imedhamiria kuendelea kutoa ushirikiano katika kuendeleza mazao ya mchanganyiko ambayo katika miaka ya nyuma ilikuwa inachukuliwa kuwa ni mazao ya chakula pekee lakini kwasasa mazao haya yanatimika kama mazao ya biashara pia ambapo Tanzania huyatumia kukuza ushirikiano wa biashara na mataifa mengine.
*Mhe. Dkt. Mwigulu* ameongeza kuwa Tanzania inatarajia kuendelea kushirikiana na *IFAD* katika sekta ya mifugo na mazao ya baharini kwa upande wa Zanzibar.
Kwa upande wake Rais wa IFAD *Ndg. Alvaro Lario*, amesema kuwa wataendelea kuhakikisha mipango na utekelezaji wa *IFAD* vinaendana na malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Tanzania ya mwaka 2050
Hii ni hatua nyingine inayomtambulisha *Dkt. Mwigulu* kama kiongozi mwajibikaji asiyelala kwa ajili ya kumsaidia *Mhe. Rais* kutimiza ndoto yake ya kuwaletea watanzania maendeleo.

Comments
Post a Comment