POLISI DAR ES SALAAM WACHUNGUZA KIFO CHA MMILIKI WA KIWANDA CHA XIL LI


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linaendelea kuchunguza tukio la kifo cha Bhaozang Ge (50), raia wa China na mmiliki wa kiwanda cha kuchakata chupa cha XIL LI, aliyefariki dunia baada ya kushambuliwa na walinzi binafsi wa kiwanda chake.


Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema tukio hilo lilitokea Mei 16, 2026 majira ya saa 8:00 usiku katika eneo la Mabibo, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.


Amesema upelelezi wa tukio hilo unaendelea ili kubaini chanzo cha tukio pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote waliohusika.


Jeshi la Polisi limewataka wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama ili kusaidia upatikanaji wa taarifa zitakazosaidia uchunguzi huo.


Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.