TBS YAJIVUNIA SAFARI YA MIAKA 50 YA KUCHOCHEA UBORA NA USALAMA.
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 50 ya shirika hilo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Ashura Katunzi,alisema safari ya nusu karne imekuwa na mafanikio makubwa yaliyosaidia kuimarika kwa sekta ya viwanda na biashara nchini.
Alisema TBS imeendelea kuboresha mifumo ya kazi ikiwemo miundombinu ya maabara, matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano (TEHAMA) pamoja na kuimarisha ushirikiano na taasisi za viwango za kimataifa.
Aidha, alisema mafanikio hayo yameiwezesha Tanzania kuongeza ushindani wa bidhaa zake katika masoko ya kikanda na kimataifa huku yakichochea ukuaji wa uchumi.
“TBS imekuwa mhimili muhimu katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinazozalishwa na kuuzwa nchini zinazingatia viwango vinavyokubalika,” alisema.
Shirika hilo limesema maadhimisho ya miaka 50 yataambatana na matukio mbalimbali ikiwemo Viwango Marathon, Jukwaa la Biashara la Viwango, shughuli za kurudisha kwa jamii (CSR) pamoja na kilele cha maadhimisho kitakachowakutanisha wadau wa sekta ya biashara.
Hata hivyo Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Miaka 50 ya Kuchochea Ubora na Usalama kwa Maisha Bora.”



Comments
Post a Comment