D KT. YONAZI AONGOZA KIKAO CHA KUJADILI UJENZI WA HOSPITALI BINAFSI MJI WA SERIKALI MTUMBA.




Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameongoza kikao cha kujadili pendekezo la Kampuni ya Istogen ya Afrika Kusini kuhusu ujenzi wa hospitali Binafsi Mji wa Serikali Mtumba Dodoma.

Kikao hicho kimefanyika kwa njia ya mtandao (Online meeting) tarehe 3 Machi, 2025 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wajumbe akiwemo Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Istogen Investments Holdings kutoka Afrika Kusini Bw. Anele Nene.

Wajumbe wengine waliohudhuria Mkutano huo ni Mkurugenzi wa Idara ya Uwezeshaji Kiuchumi na Maendeleo ya Sekta Binafsi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Condrad Millinga,Bw. Amani Tenga, Bw. Omary Hassan pamoja na Bw. Mussa Maghibi.


(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.