JUHUDI SEKONDARI YAJIVUNIA UFAULU WA WANAFUNZI KWA ASILIMIA 100 KWA MIAKA MITATU MFULULIZO.




SHULE ya Sekondari ya Serikali Juhudi iliyopo Gongolamboto wilaya ya Ilala, inajivunia mafanikio kitaaluma kwa miaka mitatu matokeo ya kidato cha sita matokeo ya Taifa (NECTA )imefaulisha kwa asilimia 100 kuanzia mwaka 2022 mpaka 2024.


 Hayo yalisemwa na Mkuu wa shule hiyo Happiness Pallangyo ,wakati wa Mahafari ya nane ya kidato cha sita ambapo jumla ya wanafunzi 343 walikabidhiwa vyeti vyao wanaotarajia kufanya mitihani yao mwezi Mei mwaka huu .


 "Shule yetu ya Juhudi kwa kipindi cha miaka mitatu  Takwimu za kitaaluma matokeo ya kidato cha sita wanafunzi ufaulu asilimia 100   mwaka,2022   wanafunzi 200 walifanya mtihani kati yao wanafunzi 37 walipata daraja la kwanza  149 walipata daraja la pili na daraja la tatu walipata 16 mwaka 2023  wanafunzi 216 walifanya mtihani daraja kwanza 65 daraja la pili 118 na daraja la tatu 32" alisema Pallangyo. 



Aidha alisema mwaka 2024 matokeo ya NECTA Taifa Division one wanafunzi 96 kati ya wanafunzi 270 waliofanya mtihani  daraja la pili  wanafunzi 148 na daraja la tatu wanafunzi 25 hayo ni mafanikio makubwa katika shule hiyo ambapo alisema wanapata ushirikiano mkubwa wa Wazazi Walimu na jitihada  kuwasimamia wanafunzi.


Alisema wahitimu wa kidato cha sita mwaka huu 2025 kwenye mitihani ya TAHOSSA waliweza kupata daraja la kwanza 147 daraja la pili 121 na daraja tatu  28 hapakuwa na daraja la nne wala 0  na mwaka huu wamepanga kuondoa daraja la tatu,daraja la nne na 0.


Akizungumzia shule hiyo alisema shule hiyo ipo  Kata  ya Gongolamboto Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam shule ya Serikali ambayo imejengwa kwa nguvu za wananchi ilianzishwa mwaka 2002  ikiwa na vyumba vinne na wanafunzi 90 wa kidato cha kwanza. 


Alisema kwa sasa shule ina wanafunzi wa kidato cha kwanza mpaka cha sita ambapo jumla ya wanafunzi 4333 kati yao wavulana 2036 na wasichana 2297  na walimu 82 .


Alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa utekelezaji wa Ilani ya chama vizuri ambapo katika sekta ya elimu Rais amefanya mambo makubwa na hivi karibuni Juhudi wanajenga shule ya sekondari ya kisasa ya ghorofa ikiwa hayo ni maendeleo makubwa katika nchi hasa katika sekta ya elimu.





Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.