KAMPUNI YA MZURI AFRIKA NA GRAMI AFRIKA YAJA NA TEKNOLOJIA YA KISASA YA KUMUINUA MKULIMA KIUCHUMI.



Katika kuunga mkono Juhudi za Serikali katika kuleta mapinduzi kwenye sekta ya kilimo hapa nchini Kampuni ya Mzuri World imezindua mashine za kisasa za kulimia, kupanda, na kunyunyiza dawa shambani. 


Akizungumza na waandishi wa habari, leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Mzuri Afrika, Shaban Mgonja, amesema lengo kuu la hatua hiyo ni kuboresha kilimo cha Tanzania kwa kutumia teknolojia za kisasa ambazo zitapunguza gharama za uzalishaji na kuongeza tija kwa wakulima.



“Kwa kuwa mimi ni Mtanzania, na kwa kutambua kuwa kilimo ni uti wa mgongo wa taifa letu, nimeona ni muhimu kuleta teknolojia hii ambayo itasaidia wakulima kuongeza uzalishaji wao kwa ufanisi mkubwa,” Amesema Mgonja.

“Mashine za Mzuri si za kawaida, Zimebuniwa ili kuchanganya hatua tatu muhimu za kilimo: kulima, kupanda mbegu, na kuweka mbolea kwa wakati mmoja”


Mgonja amesema Teknolojia hiyo sasa inapatikana katika nchi 50 duniani, na Tanzania ni moja ya nchi zinazofaidika nayo kwani Mbali na za kilimo pia kampuni hiyo inazalisha mbolea za kimiminika na tayari imesajili aina 11 za mbolea hapa nchini.

Amesema Mashine hizo zinapatikana katika ukubwa tofauti na zina uwezo wa kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ambapo Mashine ya mita 3: Inalima heka 6 kwa saa moja, Mashine ya mita 4: Inalima heka 10 kwa saa moja na Mashine ya mita 6: Inalima heka 15 kwa saa moja.

Aidha amesema kwa uwezo huo, mashine za Mzuri zinapunguza muda wa kazi, gharama za uendeshaji, na kuhakikisha kilimo kinakuwa cha kisasa na chenye tija zaidi.


Kwa upande wake Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Mzuri World, Marek Rozniak, amesisitiza kuwa lengo la kampuni sio kuuza mashine tu, bali pia kutoa msaada kwa wakulima ili waweze kutumia teknolojia hii kwa ufanisi. 



“Teknolojia ya Mzuri inasaidia wakulima kutumia raslimali zao kwa ufanisi mkubwa”alisema


Ameongeza kuwa kwa kutumia mashine hizo, mkulima anaweza kupunguza gharama za uzalishaji huku akiongeza mavuno yake kwa kiwango kikubwa na kubadili mfumo wa kilimo kutoka wa jadi na kuhamia kwenye kilimo cha kisasa hali itakayoitasaidia kuongeza uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara.


Hata hivyo Katika kutoa elimu Kwa vitendo na kuwapa wakulima uelewa wa kina kuhusu manufaa ya teknolojia hiyo pia kampuni hiyo imeandaa shamba maalumu lenye ukubwa wa heka 300 lililopo Vigwaza, Kibaha – Pwani ambapo wakulima watapata fursa ya kuona kwa vitendo jinsi mashine hizo zinavyofanya kazi na manufaa yake katika kilimo cha kisasa.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.