Katibu wa Taasisi ya vijana ya sisi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Ndg, Liaison Kayanda Awaasa vijana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

 KUELEKEA UCHAGUZI MKUU 2025 , KATIBU WA TAASISI YA VIJANA YA SISI TANZANIA MKOA WA DAR ES SALAAM NDG; LIAISON KAYANDA AWAASA VIJANA KUACHA  KUWAOGOPA WAZEE NA  KUCHUKUA FOMU ZA KUWANIA NAFASI MBALIMBALI ZA UONGOZI.


Katibu wa Taasisi ya vijana ya sisi Tanzania mkoa wa Dar es Salaam Ndg, Liaison Kayanda amewaasa vijana kuachana na  nidhamu ya uoga  na mitazamo hasi waliyonayo  kwa kuhofia kuchukua fomu za uongozi ifikapo uchaguzi mkuu 2025 kwa   kuwaogopa wazee (Viongozi) ambao wamekuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi kwa kipindi cha miaka Mingi  wakihofia kuwa ni ngumu kuwatoa katika nafasi hizo kutokana na mifumo waliyonayo na kipindi cha mda mrefu cha uongozi walichokaa madarakani.


Ndg. Liaison Kayanda alisema kuwa kama kijana umejipima na umejidhatiti na umeona unaweza twendeni tukachukue fomu tuingie kwenye nafasi mhimu za  kufanya maamuzi kwa ajili ya vijana wenzetu, Kwahiyo  Vijana tujihusishe katika Siasa na pia  hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi ambapo tunakwenda kuchagua viongozi, Viongozi ambao wataamua hatima yetu ndani ya miaka mitano ijayo.


Kayanda ameyazungumza hayo  leo akiwa katika kipindi cha "Starter" kinachorushwa na  Redio ya Bongo FM alipokuwa akielezea Kampeni yao ya "JIANDIKISHE, SHIRIKI UCHAGUZI"  yenye lengo la  kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi la Kujiandikisha katika Daftari la kudumu la mpiga kura,  ambalo kwa mkoa wa Dar es Salaam, linatarajia kuanza siku ya jumatatu ya tarehe 17/03/2025 na kumalizika siku ya Tarehe 23/03/2025.


Kampeni yao hiyo wanatarajia  kuifungua siku ya kesho jumapili ya Tarehe 16/03/2025, ambapo  yataambatana na matembezi mafupi ya hiari yatakayoanzia kituo cha mwendokasi cha magomeni mapipa mpaka Viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 12:00 Asubuhi.

Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.