Kumbilamoto Cup yadhamiria kuwafikia wananchi wa Kata zote za Ilala.

 Meya wa Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amesema awamu ya pili ya Michuano ya Kumbilamoto Cup itawafikia wananchi wa kata nyingine za wilaya ya ilala ili kuendelea kutoa fursa za vijana wengi kuonesha vipaji vyao.

Mhe Meya ameyasema hayo jana katika viwanja vya Msikate tamaa vilivyopo Vingunguti ambapo ulichezwa mchezo wa fainali ya michuano hiyo kati ya Bajaji Fc dhidi ya Saigon Fc huku timu ya Bajaji ikiibuka Mabingwa wa michuajo hiyo kwa kuifunga Saigon magoli 2 - 0.


"Tunampango wa kuboresha viwanja vya Michezo ndani ya Jiji letu tumeanza na uwanja wa shule ya Benjamin mkapa tayari mkandarasi amepatikana pia tutatanua wigo wa michuano hii kufika kata nyingine ili kuongeza fursa za vijana kuonesha vipaji vyao" 


Michuano ya Kumbilamoto Cup ambapo Bingwa Bajaji Fc amepata Kikombe, fedha kiasi cha Tsh Milioni moja pamoja na Ng'ombe mmoja, huku mshindi wa pili akipata Mbuzi wawili, Jezi na mipira.








Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.