MASABURI KUCHANGIA MILIONI 10 BENKI YA JUKWAA LA WANAWAKE CHANIKA .

NAIBU MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Ojambi Masaburi ,ambaye ni Diwani wa kata ya Chanika amesema atachangia shilingi milioni kumi Benki ya Wanawake wa Kata ya Chanika siku ya ufunguzi Mei mwaka huu 2025.


Naibu Meya Masaburi , alisema hayo leo katika ufunguzi wa Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi la kata ya Chanika lenye mitaa minane.


"Jukwaa la wanawake Chanika nimesikia SACCOS yenu mnakopeshana wenyewe kwa wenyewe kwa hisa zenu mmepiga hatua kubwa katika juhudi za kumsaidia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kuwezesha wanawake kiuchumi mfungue Benki yenu mtoke katika SACCOS muwe na benki uchumi wenu utakuwa zaidi na mimi nitawachangia shilingi milioni kumi siku ya Ufunguzi wake" alisema Masaburi. 


Aliwataka washikamane wawe wamoja katika jukwaa la Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi kata ya Chanika ili malengo yao yaweze kutimia ambapo kauli mbiu ya siku ya mwanamke Duniani kata ya Chanika unasema"kuzaliwa mwanamke sawa na digrii moja ya chuo kikuu"


Aliwataka wanawake wa Chanika kujikwamua kiuchumi wafikie uchumi wa kati waweze kukuza mitaji yao na kusomesha watoto. 


Katika siku ya Wanawake Chanika Naibu Meya Ojambi Masaburi alikata keki ya wanawake kwa shilingi 500,000/=  na kuwaahidi wanawake waliotimiza taratibu za mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri watapata shilingi milioni 100 kupitia vikundi vyao.


Kwa upande wa risala ya Jukwaa la wanawake Chanika iliyosomwa na Katibu wa Jukwaa hilo Frola Chacha ,alisema Jukwaa la Chanika lilizinduliwa mwaka 2023  likiwa na wanachama 200 kwa sasa lina wanachama 300  dhumuni la Jukwaa la wanawake Chanika kujenga uwezo katika nyanja mbali mbali zinazohusiana na mwanamke, kijamii, kiuchumi,na kisiasa yakilenga malezi bora.


Akizungumzia mafanikio Frola alisema wamefanikiwa kuwaunganisha wanawake wamekuwa mstari wa mbele katika uhamasishaji wa ushiriki katika maendeleo ya kijamii, kiuchumi pia wameweza kuwaunganisha wanawake vijana na watu wenye mahitaji maalum kujiunga katika vikundi ambapo hadi sasa vikundi 50 kutoka kata ya Chanika vimesajiliwa kati ya hivyo vikundi 35 vimeshaomba mikopo na tayari mchakato vyote vimekaguliwa vinasubiri mikopo ya Serikali. 




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.