Waziri Jerry Silaa-Shilingi bilioni 4.2 kujenga shule ya Ghorofa Juhudi Sekondari.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, ambaye ni Waziri wa Habari na Mawasiliano amesema shule ya sekondari Juhudi iliyopo Gongolamboto wilaya ya Ilala inatarajia kujengwa shule ya kisasa ya golofa ya Serikali.
Mbunge Jery Silaa alisema hayo, wakati wa Mahafari ya nane ya wahitimu wa kidato cha sita shuleni hapo ambapo alikabidhi vyeti kwa wahitimu 343 wa kidato cha sita mwaka huu wanatarajia kufanya mitihani yao hivi karibuni.
"Shilingi bilioni 4.2 zitatumika kujenga shule kisasa ya sekondari ya golofa Juhudi kwa ajili ya kukuza sekta ya elimu katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, sekta ya Elimu ni kazi kubwa imefanywa na Rais wetu katika kutuletea miradi ya maendeleo " alisema mbunge Jery .
Alimwagiza Afisa Elimu Sekondari Mwl,Mussa Ally wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam kuharakisha mchoro wa ujenzi wa shule ya kisasa kama iliyopangwa kujengwa Kitunda .
Aidha katika hatua nyingine Mbunge Jery amefunga chumba maalum mtandao wa Intranet ambapo kwa sasa Mtaala mpya watapata kupitia mfumo huo wa TEHAMA.
Alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Shule ya Juhudi Sekondari Mwalimu Haappy Pallangyo na uongozi wake wa shule kwa kukuza taaluma kwa ajili ya kuongeza ufaulu shuleni hapo ambapo kila mwaka shule hiyo inafanya vizuri sekta ya elimu na sekta ya michezo mpaka ngazi ya Taifa.
Afisa Elimu Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Mwalimu Mussa Ally ,alisema Halmashauri hiyo ina shule 61 za sekondari, na hivi karibuni wanatarajia kusajili shule zingine tatu katika halmashauri hiyo shule zake zote kitaaluma zinafanya vizuri .
Akizungumzia Sekondari ya Juhudi alisema sekondari ya Juhudi kitaaluma ipo vizuri hivi karibuni inatarajia kujengwa shule nyingine Juhudi ACADEMY Complex Serikali imeelekeza milioni 350 kwa ujenzi wa shule ya golofa.
Mwalimu Mussa alipendekeza katika shule hizo ibaki moja ya kidato cha tano na sita pia Juhudi Sekondari iwepo ndani yake shule Teule ya vipaji maalum.

Comments
Post a Comment