Mwenyekiti CCM Ilala aongoza Matembezi ya Jogging Bonyokwa kwaajili ya kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika Daftari la Mpiga kura.
MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde, ameongoza matembezi ya vijana wa Jogging kata ya Bonyokwa kwa ajili ya kuwahamasisha waweze kushiriki kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la mpiga kura linaloanza March 17 mwaka huu ili waweze kushiriki kuchagua Rais wabunge na madiwani katika uchaguzi mkuu.
Mwenyekiti Sidde aliongoza Matembezi hayo ya Jogging ya vijana wa Bonyokwa kuanzia Kanada mpaka Bonyokwa standi kuekekea Bonyokwa kisiwani yakiongozwa na mratibu sliyoandaa Matembezi hayo Diwani wa Bonyokwa Tumike Malilo, na viongozi wa Umoja wa vijana kwa ajili ya kutoa elimu hiyo watu kujiandikisha
Akizungumza katika Matembezi hayo Mwenyekiti wa ccm wilaya ya Ilala Said Sidde alisema mazoezi hayo ni afya,pia usaidia kuondoa maradhi yasioambukiza .
Sidde alisema Serikali inatumia gharama kubwa kwa kugaramia matibabu ya wananchi wake wapatao maradhi ya Kisukari na shinikizo la damu (presha)ila wakifanya mazoezi yanasaidia kuwaepusha na magonjwa yasio ambukiza na kuwaweka kuwa na afya wakati wote
"Nawaomba wananchi wa Bonyokwa siku ya Machi 17 mwaka huu zoezi la kujiandikisha katika Daftari la maboresho ya mpiga kura linaanza rasmi ili uweze kupata haki ya kupiga kura kazima ujiandikishe hivyo Nawaomba wananchi wa Bonyokwa na Wilaya ya Ilala kwa ujumla wote kujiandikisha katika Daftari hilo "alisema Sidde.
Aliwataka Wananchi wakajiandikishe katika Daftari hilo wale waliohamia na wengine ambao kwa sasa wametimiza miaka 18 waweze kupata haki ya kupiga kura kuchagua viongozi kwa ajili ya kushika dola.
Wakati huo huo aliwataka waliopewa pikipiki za chama na Chama cha Mapinduzi CCM Makao makuu wakazigomboe waanze kazi za chama waende katika matawi kuhamasisha watu waweze kwenda kujiandikisha ndio moja ya kazi ya pikipiki hizo
Diwani wa Kata ya Bonyokwa Tumike Malilo alisema dhumuni la Matembezi hayo ya Jogging Bonyokwa umoja wa Vijana wake kujenga afya pia kuhamasisha Vijana, wananchi pamoja na Jumuiya zote waweze kushiriki kwenda kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura Machi 17 mwaka huu .
Alisema Mazoea hayo ya Jogging ni endelevu kila Jumamosi watakuwa wanafanya kwa ajili ya kujenga afya zao.
Mwenyekiti wa umoja wa Vijana Bonyokwa Shamimu Jabir alisema Bonyokwa ina vijana wa UVCCM 3500 wote watahamasisha wende kujiandikisha katika Daftari la mpiga kura.



Comments
Post a Comment