Mwenyekiti Serikali Mtaa Mji Mpya Kata ya Mnyamani Anuary Mlugu aeleza mafaniko ya mtaa wake kwa kipindi cha miezi mitatu ikiwemo ujenzi wa vyoo vya mtandao wa DAWASA.
Mwenyekiti wa Serikali Mtaa Mji Mpya Kata ya Mnyamani Anuary Mlugu , kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali CCI imewezesha kujenga vyoo vya mtandao wa DAWASA katika Mtaa wa Mji Mpya kata ya Mnyamani wilayani Ilala.
Mwenyekiti Anuary Mlugu, alisema katika kwa mkutano wa wananchi wa miezi mitatu uliokuwa ukielezea mapato na matumizi ya ofisi ya Serikali za mitaa pamoja na kuelezea mambo ya maendeleo yaliofanyika.
Alisema kwa kushirikiana na DAWASA kwa ajili ya kuboresha Mazingira wameweza kuboresha miundombinu ya hivyo wananchi wanaishukuru Serikali ya Mtaa Mji Mpya kwa kazi nzuri
"Changamoto ya eneo la mji mpya vyoo Serikali ya Mtaa imeshirikiana na shirika la CCI kwa sasa vyoo vipo chini ya DAWASA ambapo Ofisi yetu imekuwa ikiamasisha suala la usafi na mazingira kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya kuunga mkono kampeni ya usafi na mazingira "alisema Mlugu.
Alisema dhumuni la mkutano huo ni kuwasomea mapato na matumizi kila baada miezi mitatu kwa mujibu wa sheria ambapo katika mtaa huo kwa sasa kipaumbele Chao maji safi na salama ya DAWASA pamoja na usafi wa mazingira.
Mwenyekiti Anuary alisema sekta ya Elimu wanamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, na Diwani wa Kata ya Mnyamani Shukuru Dege, kwa kuleta shule ya msingi ya kisasa katika kata hiyo na sasa wanafunzi wanasoma.
Akizungumzia Mafanikio alisema wameweza kumrudisha Ofisi ya Serikali ya Mtaa na kwa sasa wanafanya ukarabati itakapokamilika watarudi pale pale kwa awali
Aidha Akizungumzia ulinzi na Usalama alisema mji mpya kata ya Mnyamani ipo salama zone zote mbili Polisi Jamii wanalinda kwa kushirikiana na Polisi Kata.
Aliwataka wananchi wa Mji mpya kulipa ada ya tozo ya taka na tozo ya ulinzi vyote ni kwa mujibu wa sheria kwa maendeleo ya mtaa wetu wananchi wanatakiwa kulipa.
Akizungumzia mikakati ya mji mpya kuendelea kuhamasisha wananchi kushiriki shughuli za ujasiriamali ili wajikwamue kiuchumi Serikali yetu ya Dkt samia suluhu Hassan imeshaleta fursa na mikopo ya asilimia kumi imefunguliwa..
Kwa upande wake Polisi Kata Mnyamani Steven Itanga alisema sekta ya ulinzi ina mambo mengi kama sekta ya afya ambapo aliwataka wananchi wachangie kulipa tozo ya ulinzi wakishindwa ni wajibu wao kulinda .
Akizungumzia maswala ya ukatili Steven alisema ni changamoto amewataka Wazazi wafuatilie mienendo ya watoto wao wakati wa kwenda shule na kurudi nyumbani kwani mtoto wa mwezako ni wako hivyo ni jukumu letu sote kuwalinda.



Comments
Post a Comment