NAIBU WAZIRI KAPINGA AZINDUA NAMBA 180 YA KUPIGA BURE KWA WATEJA WA TANESCO.

 

Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga leo Machi 12, 2025 amezindua namba mpya ya huduma kwa wateja (mchongo 180) itakayotumiwa na wateja bure bila malipo ili kupata huduma mbalimbali kupitia kituo cha miito ya simu cha Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).


Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa namba hiyo 180 ya huduma kwa wateja TANESCO Waziri Kapinga amesema Kuanzishwa kwa namba hiyo inafuatia agizo lililotolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko la kuwataka TANESCO kuhakikisha wanakuwa na namba ya bure bila malipo kwa wateja ili kuboresha utoaji huduma kwa wateja na kupunguza malalamiko yasiyo ya lazima.



“Naomba  niwahakikishie kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imekusudia watanzania wapate umeme  wa uhakika na Wizara yetu ya Nishati itaendelea kuisimamia TANESCO na taasisi nyingine chini ya  Wizara kuhakikisha sekta ndogo ya umeme  inakuwa na kuleta maendeleo kwa Watanzania”amesema Kapiga



Pamoja na hayo Waziri Kapinga amewaagiza Mameneja wa Mikoa na wilaya wa TANESCO kuwasimamia watoa huduma huku akiwaasa watanzania kutumia namba hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa na si vinginevyo.




 Awali akizungumza katika hafla hiyo Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TANESCO,  Balozi Zuhura Bundala amesema mapinduzi kwenye utoaji huduma kwa wateja ni moja ya masuala ya kipaumbele ili kuchochea uchumi wa Nchi na kuongeza kuwa shughuli za uchumi zinategemea sana uwepo wa umeme wa kutosha na wa uhakika.


Amesema bodi imejipanga kutekeleza maagizo mbalimbali yanayotolewa na Wizara na  iko tayari kuhakikisha TANESCO inafanya kazi kwa bidii kwa kutoa huduma bora kwa wateja ili kupunguza kero na changamoto za masuala mbalimbali katika sekta hiyo.


Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mha. Gissima-Nyamo Hanga amesena dunia ya sasa ya biashara na ushibdani wa kibiashara unategemea uwepo wa huduma bora ya uneme na kutatua changamoto kwa wakati


Aidha, Mha. Gissima amesema licha ya kujipanga kutoa huduma bora kwa wateja pia wamekuwa wakitekeleza kwa vitendo uhamasishaji wa matumizi bora ya nishati kwa kutumia umeme.


Hafla hiyo imehudhuriwa na wawakilishi kutoka Wizara ya Nishati, bodi ya wakurugenzi ya TANESCO na wadau mbalimbali wa Sekta ya Nishati.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.