Rais Samia: “Ahsanteni nyote kwa salamu za upendo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani”
Rais Samia Suluhu Hassan awashukuru Watanzania kwa salamu za kheri, umoja na upendo katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Amesema Nchi imepiga hatua kubwa katika kuufikia usawa wa kijinsia ikiwa ni sehemu ya kazi ya kujenga Tanzania jumuishi yenye ustawi, haki na isiyo na ubaguzi kwa sababu zozote zile ziwe za kidini, kikanda, kiitikadi au kijinsia.
Rais Samia amesema Siku ya Wanawake Duniani pia ni fursa kwetu kutathmini mafanikio makubwa tunayoendelea kuyapata katika sekta mbalimbali, yanayohakikisha kila msichana na mwanamke anapata nafasi ya kufikia ndoto zake.
Amesema Mafanikio hayo ni pamoja na hatua kubwa ambayo nchi imepiga katika sekta ya elimu na sekta ya afya, ambazo zimeweka msingi imara na mwanzo madhubuti katika safari ya mafanikio.





Comments
Post a Comment