RC Chalamila ameagiza TBA kufatilia mikataba ya Wapangaji Magomeni Kota.


MKUU wa Mkoa Dar es Salaam Albert John Chalamila, amemwagiza Mkurugenzi wa TBA kufatilia mikataba ya Wapangaji  katika nyumba za Magomeni Kota  kwa kipindi cha mwezi mmoja Wapangaji wote wakamilishe mikataba yao.


Mkuu wa Mkoa Albert Chalamila ,alisema hayo wakati wa uzinduzi wa ofisi ya Wamachinga wa Mkoa Dar es Salaam na Wasafirishaji wa Bodaboda ambayo imejengwa wilayani Kinondoni iliyogharimu shilingi milioni 500 fedha kutoka Ofisi ya Rais Tawala  za Mikoa (TAMISEMI.)


"Nasikia malalamiko mengi katika nyumba hizi za Magomeni Kota zikiwemo kushindwa kulipa tozo ya takataka na kukamilisha mikataba yenu ya nyumba malalamiko yamekuwa mengi katika watu 640  ambao wapo katika nyumba hizi waliokamilisha mikataba yao na kulipa zaidi ya Wapangaji 100 wengine mpaka sasa wanasumbua, Serikali  inaagiza kwa Mkurugenzi wa TBA kwa kipindi cha mwezi mmoja wote wawe wamekamilisha mikataba yao" alisema Chalamila. 


Awali kabla kujengwa nyumba za mradi wa Magomeni kota kulikuwa na nyumba za wananchi waliokuwa wakiishi eneo hilo baadae Serikali walichukua eneo hilo kwa kuliboresha kujenga nyumba za kisasa kisha wale Wapangaji waliokuwa katika nyumba za awali  walipangishwa katika mradi huo wa nyumba za Magomeni kota ambazo zimejengwa kwa Gholofa na Wakala wa Majengo TBA. 


Wakati huo huo Mkuu wa Mkoa Chalamila alitoa agizo kwa viongozi wa Dini  wa mkoa Dar es Salaam Wanaume wakiitaji kuoa mke wa pili watoe Benki Statiment zao ndio wakubaliwe kuoa kinyume cha hapo marufuku kuongeza mke kwa ajili ya familia mpya.


Akizungumzia wamachinga wa mkoa wa huo na Wasafirishaji maarufu Bodaboda alimwagiza Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, kuweka vifaa vya thamani katika ofisi hizo ili waweze kuzitumia ikiwemo fenicha ..


"Rais Samia ataki sifa anataka watu wake wafanye kazi na kukuza uchumi wamachinga wa Dar es salaam na Bodaboda tunataka mkuze uchumi ofisi hii ilete maendeleo makubwa katika kujenga Tanzania ya uchumi wa Viwanda. 


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Saady Mtambule, alimpongeza Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kujali makundi ya Machinga na Bodaboda kwa ajili ya kuaajengea ofisi ya kisasa.


Mkuu wa wilaya Kinondoni Saady alisema kujengwa kwa ofisi hiyo kutakuza uchumi kwa kukusanya mapato ya kujenga shule ,B

barabara, vituo vya afya ,alutumia fursa hiyo akitoa wito kwa wamachinga ns bodaboda kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwataka Machi 17 mwaka huu  makundi hayo yakajiandikishe katika daftari la maboresho ya mpiga kura ili waweze kupata haki kupiga kura katika uchaguzi wa mkuu mwezi October mwaka huu kwa ajili ya kuchagua Rais, Wabunge na madiwani. 


Mwenyekiti wa Machinga Mkoa Dar es Salaam Yusuph Namoto alisema wamachinga wa Mkoa huo kura zote mwezi October kwa chama cha Mapinduzi kumpigia Rais Dkt.Samia sababu Dkt Samia amefanya mazuri katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi na kuongeza fursa za kiuchumi.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.