RC Makonda avipongeza Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Arusha kwa kuimarisha usalama.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mheshimiwa Paul Christian Makonda  amevipongeza vyombo vya ulinzi na usalama  Mkoani humo kwa namna ambavyo vinaimarisha ulinzi na usalama wakati wote bila kuchoka.


Mkuu huyo wa Mkoa ametoa pongezi hizo leo Machi  01,2025 wakati akiongea na maafisa na askari wa vyombo vya ulinzi na usalama baada ya kumaliza mazoezi ya kutembea (route Match) katika barabara mbalimbali za Jiji la Arusha 


Mheshimiwa Makonda Pamoja na kuvipongeza vyombo hivyo vya ulinzi na Usalama, Pia ametumia fursa hiyo kuwaarika maafisa hao na askari katika shamrashamra za kuelekea siku ya wanawake duniani ambayo yanafanyika kitaifa Mkoani Arusha kuanzia leo machi 01 hadi tarehe 08, 2025.


Nao wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama Mkoani humo  kwa Pamoja wamewataka maafisa na askari kuwa na utaratibu wa kufanya mazoezi mara kwa mara kwani pamoja na kuimarisha afya za miili yao pia yanajenga ushrikiano mzuri miongoni mwao.






Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.