SALMA FUMBWE AWATAKA WANAWAKE UWT TABATA KUSIMAMA IMARA.


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi kutokea Umoja Wanawake( UWT) Wilaya ya Ilala Salma Fumbwe, amewataka wanawake wa UWT kata ya Tabata kusimama imara kuhamasisha watu kuanzia ngazi ya mashina mpaka Katakwenda kujiandikisha katika maboresho ya Daftari la Mpiga kura kuanzia March 17 mwaka huu. 


Mjumbe Salma Fumbwe aliyasema hayo Kata ya Tabata alipokua mgeni rasmi katika mkutano wa Wanawake kwa ajili ya kutoa elimu kwa ajili ya kushiriki katika Daftari la mpiga kura ambapo mkutano huo uliandaliwa na Umoja wanawake UWT Kata ya Tabata ambapo zaidi ya wanawake 500 walishiriki katika mkutano huo .


"Wanawake wezangu muda umefika sasa wa kutafuta dola kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Rais,Wabunge na Madiwani mwaka 2025 huku tukihakikisha Chama cha Mapinduzi kinashika dola kupitia Rais wetu mwanamke mwezetu Dkt.Samia Suluhu Hassan anashinda kwa kishindo pamoja na Mbunge wetu wa jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ,pamoja na Diwani wote kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi "alisema Salma


Salma Fumbwe aliwataka wanawake kusimama imara kuhamasisha kuanzia ngazi ya mashina na familia zao wote wakashiriki kujiandikisha ili waweze kupata haki ya kupiga kura katika uchaguzi mkuu ili CCM iweze kushika dola.


Alisema Wanawake ni jeshi kubwa kila mmoja achukue familia yake baba ,Mama na watoto nyumbani siku ya kujiandikisha ikifika ili kuweza kupata wapiga kura wengi watakao mchagua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ambaye ametekeleza Ilani kwa vitendo na kuongeza fursa za uchumi wa Viwanda.


Alitumia fursa hiyo kuwapongeza Wanawake wa UWT kata ya Tabata kwa kuitikia kikao hicho cha kupeana elimu ya Daftari la maboresho ya mpiga kura ambapo alipongeza uongozi wa UWT, Zena Ally Kengera Mwenyekiti na Katibu wake Tatu Lazaro kwa kusimamia jumuiya ya wanawake vizuri .


Aliwataka wanawake wa UWT kutembea kifua mbele kwani  wanawake ni jeshi kubwa kwenda kusemea maendeleo ya Kata ya Tabata yaliofanywa na Mbunge wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, na Diwani wa Kata ya Tabata Omary Matulanga. 


Aliwataka wanawake UWT Tabata kuwathamini wanawake wa Tabata na kujenga umoja na mshikamano kwa kushirikiana pamoja


Katibu wa CCM kata ya Tabata Haluna Alphonce,alisema CCM Tabata ipo salama na Chama kitaibuka kidedea katika kura za Rais,Wanunge na madiwani. 


Mwenyekiti wa UWT kata ya Tabata Zena Ally Kengera aliwataka wanawake wa UWT Tabata kujenga umoja na mshikamano muda ukifika waweze kumpigia kura za kishindo Dkt Samia Suluhu Hassan.



Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.