Wajasiriamali 800 wa Kata ya Kisukuru wapokea mtaji wa vifaranga kutoka kwa Diwani Lugome.
DIWANI LUCY LUGOME AGAWA KUKU KWA WAJASIRIAMALI.
Na Mwandishi Wetu.
DIWANI wa Kata ya Kisukuru Wilayani Ilala,Lucy Lugome amegawa mitaji ya kuku kwa Wafugaji 800 wa kata ya Kisukuru ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Diwani Lucy, alisema lengo la kugawa kuku kwa wajasiriamali waliopo katika kata yake ni kuwawezesha kujikwamua kiuchumi waweze kukuza mitaji yao.
"Wananchi wangu 800 leo nimewapatia mtaji kwa kuwapa kuku wa biashara waweze kujikwamua kiuchumi kuku hawa wanagaiwa kwa mtu yoyote Mjasiriamali bila kuchagua vyama vyao "alisema Lucy.
Diwani Lucy Lugome alisema anaunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kufungua fursa ambapo alisema kata hiyo ina mitaa mitatu yote imepata kuku wa biashara.
Kwa upande wake mmoja wa wakazi wa Kata ya Kisukuru Chritina Gabriel alimpongeza Diwani wao kwa kuwawezesha kiuchumi Wanawake, vijana na wajasiriamali mbalimbali kwa kuwapatia mitaji.
Christina aliwataka Wananchi wa Kisukuru kuunga mkono juhudi za Diwani Lucy Lugome za kuwakwamua kiuchumi na kuwafungulia fursa wananchi wake.



Comments
Post a Comment