WAZIRI MHAGAMA AZINDUA BODI YA USHAURI YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA - AMANA.
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Amana imezindua rasmi Bodi yake ya Ushauri katika hafla iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa sekta ya afya ambapo Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa ni Waziri wa Afya, Mheshimiwa Jenista Mhagama, ambaye alisisitiza umuhimu wa bodi hiyo katika kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.
Alisema Uzinduzi wa bodi hiyo ni hatua muhimu katika kuimarisha usimamizi na uboreshaji wa huduma za afva kwa iamii.
"Natoa wito kwa Bodi ya washauri Kutatua changamoto na kubuni njia mpya za kuboresha Utoaji wa huduma bora za Afya katika Hospitali ya Amana, Pia Bodi hii iweze kua mfano kwa wengine kwenye utendaji wa kazi zake"alisema Waziri Mhagama
Bodi hiyo itaongozwa na Mwenyekiti mteule Dr. David Sando, kwa kushirikiana na wajumbe wengine, wakisaidiana na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dr. Bryson Kiwelu.
"Ni matarajio yangu mimi pamoja na Bodi ya washauri kushirikiana na serikali, Taasisi pamoja na wadau mbalimbali wa afya kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya afya Hususani Hospitali ya Amana, pamoja na kuhakikisha tunafanikisha Utoaji wa huduma bora kwa wananchi wote." Alisema Dr Sando.
Pamoja na hayo katika hafla hiyo ya uzinduzi wa bodi ya ushauri katika Hospitali ya Amana Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama amepokea hundi ya fedha kiasi cha Shilingi Milioni 100 kutoka katika Club ya Young Africans iliyokabidhiwa na Rais wa Club hiyo Eng.Hersi Said ambazo zitasaidia katika uboreshaji wa miundombinu pamoja na huduma za afya katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa - Amana.





Comments
Post a Comment