Ziara ya Rais Samia yafanikiwa kwa asilimia 100 Mkoani Tanga.
Serikali imesema ziara ya Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan mkoani Tanga imefanikiwa kwa asilimia 100.
Hayo yamebainishwa na Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Dar ed salaam ambapo amesema idadi ya wahudhuriaji mikutano, wingi wa miradi iliyokaguliwa na tathmini iliyofanywa imeonesha kuwa ziara hiyo imefanikiwa.
Msigwa amesema akiwa mkoani Tanga, Rais Samia alitembelea miradi kadhaa, ikiwemo mradi wa ujenzi wa Bwawa la Mkomazi unaotekelezwa kwa ruzuku ya Serikali ambao unagharimu Sh bilioni 18.2.
Aidha Msigwa amesema mradi huo umefikia asilimia 35 na utakapokamilika utawanufaisha wakulima zaidi ya 20,000 kutoka vijiji 28 na kata saba mkoani humo.
Hata hivyo Takwimu zinaonesha ziara ya Mhe. rais Samia Suluhu Hassan imeangaliwa na watu milioni 16 mubashara kwenye televisheni na mitandao ya kijamii.

Comments
Post a Comment