AMANA HOSPITAL YANG’ARA KITAIFA, YAPOKEA TUZO YA HUDUMA BORA.

 


AMANA HOSPITAL YANG’ARA KITAIFA, YAPOKEA TUZO YA HUDUMA BORA




Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Amana imeibuka mshindi wa kwanza katika utoaji wa huduma bora za matibabu nchini, kati ya hospitali 28 za Rufaa, na kutunukiwa Tuzo ya Huduma Bora ya Matibabu Tanzania.


Tuzo hiyo ilitolewa Aprili 8, mwaka huu, katika hafla rasmi iliyohusisha wawakilishi kutoka Wizara ya Afya, ambapo ilielezwa kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya maboresho ya miundombinu, usimamizi madhubuti na juhudi za watumishi wa hospitali hiyo chini ya Mganga Mfawidhi, Dkt. Brayson Kiwelu.


Akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam,Dkt. Toba Nguvila, alimpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuboresha sekta ya afya nchini.


“Hospitali yetu ya Amana inafanya kazi kubwa, chini ya usimamizi wa Dkt. Kiwelu ambaye amekuwa mbunifu wa mikakati mbalimbali ya kuboresha huduma ambapo sasa tuna vifaa tiba vya kisasa, madaktari bingwa na wauguzi wenye weledi jambo ambalo limepelekea malalamiko kutoka kwa wagonjwa kupungua kwa kiasi kikubwa,” alisema Dkt Nguvila.



“Hospitali yetu ya Amana inafanya kazi kubwa, chini ya usimamizi wa Dkt. Kiwelu kupitia uongozi wake na ubunifu wa mikakati mbalimbali ambapo huduma zimeimarika, malalamiko ya wagonjwa yamepungua, vifaa vya kisasa vimepatikana, na wauguzi wameboreshwa,” alisema Nguvila.


Aliongeza kuwa kwa sasa Amana inatoa huduma kwa kutumia madaktari bingwa wa kisasa, wauguzi mahiri, na vifaa tiba vya kisasa, na kwamba mafanikio hayo ni matunda ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan.


Pamoja na mafanikio hayo, Katibu Tawala alitaja baadhi ya changamoto zinazokabili hospitali hiyo, ikiwemo uhaba wa eneo la upanuzi ambapo alisema Serikali ya Mkoa ipo kwenye hatua ya kuwasilisha ombi kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, ili kuomba kupewa eneo la Shirika la Nyumba (NHC) kwa ajili ya kupanua huduma za hospitali hiyo.




Kwa upande wake, Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Amana, Dkt. Brayson Kiwelu alisema ushindi huo ni matokeo ya mshikamano na juhudi za pamoja za watumishi wa hospitali hiyo katika utendaji kazi wao wa kuwahudumia wagonjwa.


“Tuzo hii ya kitaifa inatupa nguvu mpya,Tunajipanga sasa kuingia kwenye ushindani wa kimataifa kwa kuhakikisha tunatoa huduma bora zaidi kila siku na shukrani zote tunazirudisha kwa Mh. Rais Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa na kuimarisha sekta ya afya nchini” alisema Dkt. Kiwelu.


Naye Mjumbe wa Bodi ya Hospitali ya Amana, Bi. Idda Luhanga, alipongeza watumishi wa hospitali hiyo kwa niaba ya watoto njiti na wagonjwa wote wanaopokea huduma, akisisitiza kuwa bodi imeweka mkakati wa kukusanya maoni ya wateja ili kuimarisha zaidi huduma zinazotolewa na kuendelea kushinda tuzo kila mwaka.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.