Dkt.Mandai na Mbunge Giga washiriki mbio za hisani za Bunge.
Mjumbe wa Baraza la Wazazi Taifa Dkt.Ally Mandai,na Mbunge wa Wazazi (MNEC)ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji Bi.Najma Murtaza Giga ,wameshiriki mbio za hisani kwa ajili ya kuwakilisha Jumuiya ya Wazazi CCM.
Akizungumza mara baada kumaliza Matembezi hayo ya hisani kwa ajili ya kuchangia fedha za ujenzi wa shule ya Bunge Wavulana ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa ,Dkt ,Ally Mandai alisema Jumuiya ya Wazazi ni injini ya chama cha Mapinduzi CCM katika shughuli zote za chama Wazazi wamesimama mstari wa mbele.
"Jumuiya ya Wazazi CCM tupo mstari wa mbele kusaidia shughuli za chama katika kumsaidia Mwenyekiti wa CCM Taifa Dkt.Samia Suluhu Hassan na ushiriki wetu katika michezo pia tupo mstari wa mbele kwasababu michezo inajenga afya na kujenga mahusiano ndani ya jamii”Dkt Mandai.
Aidha Dkt.Ally Mandai alisema Jumuiya ya Wazazi katika kuisaidia Serikali ipo mstari wa mbele kwenye baadhi ya mambo yakiwemo ya kuisaidia Serikali katika sekta ya afya, sekta ya Elimu na utunzaji mazingira hapa nchini.
Mbunge wa Wazazi MNEC ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji, Najma Murtaza Giga, aliipongeza Serikali katika kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kukuza sekta ya michezo na sekta ya Elimu hapa Nchini.
Kwa upande wake Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aliwahakikishia, watanzania kuwa fedha zilizokusanywa katika mbio za hisani zinaenda kutumika kama zilivyokusudiwa katika kuchangisha fedha za ujenzi wa shule ya sekondari Bunge Wavulana.
Aidha Waziri Mkuu Majaliwa alisema shule hiyo ya kidato cha tano na sita itajengwa katika eneo la kikombo jiji la Dodoma karibu kidogo na shule ya Wasichana iliyojengwa na wabunge wanawake mwaka 2020.

Comments
Post a Comment