Shule ya Sekondari Kisutu wajivunia mafanikio kuongezeka kwa ufaulu ndani ya miaka mitatu.


SHULE ya Sekondari ya wasichana Kisutu wajivunia mafanikio ya kitaaluma kwa kufanya vizuri katika kipindi cha miaka mitatu mfululizo huku ufaulu wa wanafunzi wanaohitimu kidato cha sita ukipanda mwaka hadi mwaka. 


Hayo yalisemwa na Mkuu wa shule hiyo Chiku Jumanne Mhando  katika mahafali ya saba  ya kidato cha sita iliyofanyika katika shule hiyo iliyopo Dar es salaam, ambapo wahitimu  318 walitunukiwa vyeti vya kidato cha sita. 


"Shule yetu ya Sekondari Kisutu tunajivunia ufaulu mwaka hadi mwaka, 2022 jumla ya watahiniwa walikuwa 262 waliofanya mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha sita, watahiniwa 40 walipata daraja la kwanza, watahiniwa 135 walipata daraja la pili, watahiniwa 84 walipata daraja la tatu, watahiniwa watatu walipata daraja la nne na hakuwepo mtahiniwa aliyepata daraja sifuri mwaka 2023, jumla ya watahiniwa walikuwa 249 ambapo katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita uliofanyika mwezi Mei mwaka 2023, watahiniwa 68 walipata daraja la kwanza, watahiniwa 134 walipata daraja la pili, watahiniwa 47 walipata daraja la tatu haya yote ni mafanikio kitaaluma katika shule yetu " alisema  Chiku


Aidha alisema mwaka  2024 kulikuwa na jumla ya watahiniwa 293, ambapo katika mtihani wa kuhitimu elimu ya kidato cha sita uliofanyika mwezi Mei 2024, watahiniwa 94 walipata daraja la kwanza, watahiniwa 144 walipata daraja la pili, watahiniwa 54 walipata daraja la tatu, kwa bahati mbaya mtahiniwa mmoja alipata daraja la nne lakini hakuwepo mtahiniwa aliyepata daraja sifuri. 


Mwalimu Chiku, alisema ufaulu huo unatokana na kazi kubwa inayofanywa na uongozi wa shule hiyo ,Wazazi na wanafunzi pamoja pia kumtanguliza Mwenyezi Mungu na kuwapa wanafunzi mitihani ya upimaji mara kwa mara kwa ajili ya kuwaandaa na mitihani ya kitaifa. 


Alisema matarajio yao walimu na uongozi wa shule  katika mtihani wa kuhitimu kidato cha sita utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu 2025 hakutakua na mwanafunzi atakayepata daraja la nne wala daraja sifuri badala yake kuwa na wanafunzi wengi watakaopata daraja la kwanza na la pili huku wanafunzi wachache watakaopata daraja la tatu.


Pia alisema kitaaluma, wanafunzi wa Kisutu  hushiriki katika shughuli nyingine za kijamii yaani extra-curricular activities ambapo hushiriki katika program mbalimbali zinazobuniwa na kuanzishwa na taasisi mbalimbali za kijamii hapa nchini kama vile Apps & Girls Tanzania ambayo hutoa mafunzo ya ujasiriamali na TEHAMA kwa lengo la kumjengea mtoto wa kike uwezo wa kutatua matatizo mbalimbali ya kijamii kwa kutumia TEHAMA na mbinu mbalimbali za ujasiriamali.


Alisema shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu ni moja kati ya shule kongwe hapa nchini,awali shule hii ilikuwa ni shule ya msingi, ilijengwa na jamii ya Kihindu iliyojulikana kwa jina Arya Samaji na ilifunguliwa rasmi mwaka 1926. 


Mwalimu Chiku alisema  baadaye ilibadilishwa jina na kuitwa D.A Girls' Secondary School, jina lililotokana na jina la Bi. Denkuvar Arya ambaye alipambania elimu ya mtoto wa kike kipindi hicho.


"Baada ya Tanganyika kupata uhuru  mwaka 1961, D.A Girls' Secondary School ilitaifishwa na serikali na kuitwa Shule ya Sekondari ya Wasichana Kisutu ikidahili wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 2017, serikali iliibadilisha na kuwa shule inayodahili wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita pekee kwa tahasusi mbili za CBG na HGL " alisema 


Aliongeza kuwa kwa sasa shule ina jumla ya wanafunzi 679 wote wakiwa ni wasichana ambapo kidato cha sita ni 318 na kidato cha tano ni 361 masomo  wanayofundishwa shule ya Kusutu  ni sita ambazo ni PCM, PCB, CBG, HGL, HGK na HKL.




Comments

Popular posts from this blog

RC CHALAMILA AWATAKA WENYEVITI NA WATENDAJI KATA NA MITAA DAR KUSIMAMIA ULINZI NA USALAMA.

MAHAFALI YA NANE SHULE YA AWALI NA MSINGI SAI YAFANA, WAZAZI WATAKIWA KULEA WATOTO KATIKA MISINGI YA MAADILI MEMA.